Man City imekua sehemu ya klabu zilizotinga hatua ya robo fainali ya kombe la FA, baada ya kufanya vyema kwenye mchezo wa marudio wa 16 bora dhidi ya Huddersfield Town.
Man City walilazimika kurudiana na Huddersfield Town, kufuatia matokeo ya sare ya bila kufungana, yaliyopatikana katika mchezo wa kwanza ambao uliunguruma February 18 huko John Smith's Stadium.
Mchezo wa marudio ambao umechezwa usiku wa kuamkia hii leo ulikua huko Etihad Stadium, ambapo wenyeji walichomoza na ushindi wa mabao matano kwa moja.
Mabao ya Man City yalifungwa na Leroy Sane, Kelechi Iheanacho Pablo Zabaleta na Sergio Aguero aliyefunga mawili.
Hata hivyo Man City walitangulia kufungwa bao la mapema na wapinzani wao katika dakika ya 7 kupitia kwa mshambualiaji kutoka nchini England Harry Charles Bunn.
Kukamilika kwa mchezo huo wa marudio kunaifanya hatua ya robo fainali kupata washiriki wanane ambao tayari wameshapangiwa michezo ya hatua hiyo.
Jumamosi, 11 Machi 2017
Middlesbrough Vs Manchester City
Arsenal Vs Lincoln
Jumapili, 12 Machi 2017
Tottenham Hotspur Vs Millwall
Jumatatu, 13 Machi 2017
Chelsea Vs Manchester United