WAZIRI wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba amewaagiza wamiliki wa viwanda vya chai nchini kununua chai ya Wakulima wadogo kwa kuzingatia bei elekezi ya serikali na sio bei wanayojipangia wao ya kuwanyonya Wakulima wadogo wa zao hilo la chai nchini Kuwa serikali imedhamilia kuwakomboa Wakulima wadogo wa zao la chai hapa nchini kama njia ya kukuza soko la bidhaa zitokanazo na chai hapa nchini ya duniani ,hivyo njia pekee ni kuona Wakulima wadogo wanaendelea kuhamasika kuongeza kasi ya kilimo hicho cha chai ili kuviwezesha viwanda vya chai nchini kuzalisha chai kwa wingi na ubora zaidi.
Alisema kuwa zao la chai ni moja kati ya mazao yanayopelewa kipaumbele kama mazao ya biashara hapa nchini na kuwa zao la chai pekee huliingizia Taifa wastani wa dola za kimarekani milioni 50 na kutoa ajira kwa watu milioni 2 kwa mwaka hivyo ni zao lina lina fursa kubwa ya kuongeza wigo wa kiuchumi nchini pamoja na kuendeleza kilimo cha zao hilo.
Waziri Dkt Tizeba aliyewakilishwa na mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza katika ufunguzi huo wa mkutano mkuu wa wadau wa chai nchini uliofanyika katika ukumbi wa taasisi ya utafiti wa chai (TRIT) Gwazi Mufindi leo alisema kuwa uzalishaji wa chai nchini kwa upande wa majani makavu ni wastani wa tani 35 kwa mwaka wakati kwa wakulima wadogo wanazalisha wanazalisha kilo 1000 kwa hekta kwa mwaka na Wakulima wakubwa ni wastani wa kilo 2000 za majani makavu kwa hekta kwa mwaka ukilinganisha takwimu za nchi ya Kenya ambayo tija ni kwa mkulima mdogo ni wastani wa kilo 2500 kwa hekta takwimu ambazo zinaonyesha sekta ndogo ya chai nchini ipo nyuma ukilinganisha na Kenya.
“Ukuaji wa sekta ndogo ya chai Tanzania ni mdogo sana ukilinganisha na nchi kama Rwanda na Uganda ila kuna uwezekano mkubwa wa kuongeza uzalishaji wa tija ya chai ya Tanzania kwa kuwa nia ya kuendeleza zao la chain a ardhi ipo ….naomba kutoa rai kwenu wadau kuweka mipango ya kuendeleza kilimo hiki na serikali ipo nyuma yenu “
Alisema kuwa serikali imedhamilia kushirikiana na wadau wa chai kwa kuongeza ardhi kwa maeneo yanayolima chai hadi kufikia hekta 27000 kuwa mwaka 2021/2022 hekta kutoka 22721 kwa sasa pia kuongeza uzalishwaji wa chai kavu kutoka wastani wa tani 32 kwa mwaka hadi kufikia zaidi ya tani 50,000 mwaka 2021/2022 na kuongeza uzalishaji wa tija kutoka kilo 1000 kwa mwaka hadi zaidi ya kilo 2000 za majani makavu.
Awali mwenyekiti wa mkutano huo spika wa bunge la jamhuri ya muungano ya Tanzania (mstaafu) Anne Makinda ambae ni mwenyekiti wa boi ya chai nchini alisema kuwa kero kubwa ya Wakulima wadogo wa chai ni mbolea kwa ajili ya kukuzia zao hilo kwani zao hilo Wakulima hawana ruzuku ya serikali Kuwa mbolea inayotumika kwa zao la chai ni tofauti na ile ya mazao ya mahindi japo changamoto hiyo wanaendelea kuijadilia pamoja na serikali huku akidai kuwa chai ya Tanzania inauzwa kwa bei ndogo sana kutokana na ubora wake kuwa duni ukilinganishwa na chai ya Wakulima wadogo wa Rwanda ambao walikuwa katika vita leo wamefikia chai kavu zaidi ta tani 20,000 lakini Tanzania ambayo ilipata uhuru miaka 50 iliyopita chai haina ubora
“ Yawezekana wenzetu kwa kuwa ni Wakulima wapya wanatumia vikonyo vipya na maeneo mapya ndio maana wanatuzidi ila sisi bado tunatumia vikonyo vya zamani na ardhi iliyochoka “
Makinda alisema migogoro midogo midogo inayoanzishwa na viongozi katika maeneo ya Wakulima wa chai ni changamoto ya kurudisha nyuma kasi ya uzalishaji wa zao la chai nchini hivyo zinahitajika jitihada za kuondoa migogoro hiyo ili kukuza zao la chai nchini