Meneja Mradi wa Kampuni ya Songoro Marine Transport inayojenga Kiuvko cha MV. Kazi, Bw. Major Songoro, akitoa ufafanuzi wa mashine kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, alipokagua Kivuko hicho jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (kulia), akiangalia moja ya vifaa vilivyoko kwenye chumba cha kuendeshea kivuko katika kivuko cha MV. Kazi kinachojengwa jijini Dar es Salaam. Kivuko hicho kitakabidhiwa tarehe 15 Mwezi huu. Wa pili kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA), Dkt. Musa Mgwatu.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (kulia), akifafanua jambo kwa Uongozi wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA), mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kivuko kipya cha MV Kazi ambacho kinatengenezwa jijini Dar es salaam na Kampuni ya Songoro Marine Transport.
Mafundi wa Kampuni ya Songoro Marine Transport, wakiendelea na kazi ya kufunga mashine katika Kivuko cha MV Kazi. Kivuko hicho kitakamilika na kukabidhiwa wiki ijayo na kina uwezo wakubeba abiria 800 na magari 22 kwa wakati mmoja.
Kivuko cha MV. Kazi kikiwa katika hatua za mwisho za ujenzi wake.Kiuvko hicho kitakamilika na kuanza tarehe 15 mwezi huu na kina uwezo wakubeba abiria 800 na magari 22 kwa wakati mmoja. Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.