
Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group) imesema itaendeleza sera yake ya kutoa ajira bila kufanya ubaguzi wa kijinsia baina ya wanawake na wanaume.
Hayo yamesemwa na mwakilishi wa MeTL Group, Catherine Decker wakati wa kongamano la kuadhimisha siku ya wanawake lililoandaliwa na Shirikisho la Wafanyakazi nchini Tanzania (TUCTA).Catherine amesema kampuni ya MeTL imeamua kuweka utaratibu huo wa kuweka usawa kwa wafanyakazi kati ya wanaume na wanawake ili kuwapa nafasi wanawake kushiriki katika shughuli za maendeleo lakini pia kuepusha matukio ya unyanyasaji wa kijinsia kazini.


