Quantcast
Channel: Mdimu's Blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1295

FID Q: Open Mic sio biashara, ni harakati

$
0
0
Msanii nguli wa muziki wa kizazi kipya toka mji wa miamba, Fareed Kubanda a.k.a Fid Q ameweka wazi kwa wadau wa muziki wa kizazi kipya kwamba mpango wake wa kutoa nafasi kwa wasanii wasio na majina unaojulikana kwa jina la Open Mic sio wa kibiashara, ni harakati zake za kuhakikisha kwamba wasanii wadogo wanaohangaika kupata majukwaa ya kuonesha kazi zao wanapata nafasi.

Akiongea chana huu katika kipindi cha Ladha 3600 cha Efm, Fid Q ameeleza sababu ya kuanzishwa kwa mpango hum ambao kwa sasa jukwaa lake huwa wazi kila Alhamis, ni idadi kubwa ya wasabi wachanga waliokuwa wakimfuata kumuomba awasaidia kusogeza sanaa yao ya muziki mbele kwa kutumia jina lake kubwa katika medani ya muziki wa kizazi kipya.

"Kiukweli mimi sikuwa na msaada mkubwa wa kuwapa kwa sababu mimi mwenyewe msanii na nahitaji kusogea hatua moja kadri siku zinavyoendelea, lakini nikaona nikianzisha hili jukwaa mimi na wao kwa pamoja tutaonekana, na tutapiga hatua pamoja", akabainisha.

Hatua ya kwanza akatafuta eneo, na kazi ikaanza ambapo sasa Open Mic Thursday ni jukwaa kubwa la Hip Hop amble hufanyika Latina mimi miiili mikubwa, ambayo ni Dar es Salaam na Arusha. Lengo likiwa ni kuukuza muziki wa Hip Hop kwa kuwapa vijana nafasi ya kuonesha walichonacho

Viewing all articles
Browse latest Browse all 1295

Trending Articles