Staa wa filamu nchini, Msanii Elizabeth Michael amehukumiwa kwenda jela miaka miwili baada ya kupatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba, katika hukumu iliyosomwa na Jaji wa Mahakama Kuu Mheshimiwa Sam Rumanyika.
Kwa muda wa miaka mitano mfululizo Lulu alikuwa akikabiliwa na kesi ya kumuua mpenzi wake Steven Kanumba bila kukusudia, kinyume cha kifungu cha 195 cha kanuni za adhabu (PC), Aprili 7, 2012, Sinza Vatican jijini Dar es Salaam kufuatia ugomvi wa kimapenzi ulioibuka baina yao.