Quantcast
Channel: Mdimu's Blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1295

SOMA: Kuhusu panga pangua ya Dk Magufuli jioni hii, amtoa Msajili wa Hazina, Ole Sendeka aula!

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli jioni ya leo amefanya mabadiliko katika safu zke za utendaji na likiwemo la kuteua Msajili mpya wa hazina, ambapo amemteua Dk Oswarkd J. Mashindano kushika nyadhifa hiyo nyeti ambayo awali ilikuwa ikishikiliwa na Lawrence Mafuru.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu iliyosambazwa kwa vyombo vya habari, Bw Mafuru atapangiwa kazi nyingine, na mabadiliko mengine ni kama haya yafuatayo:

Prof Faustin Kamuzora ambaye alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, mmekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Mathew Mtigumwe amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo, nafasi ambayo ilikuwa ikishikiliwa na Dk Florence Turuka ambaye amepelekwa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa kuwa Katibu Mkuu.

Dk Maria sasabo, eye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi ambako Mhandishi Angelina Matete ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu.

Aisha Rais Magufuli amemteua Dk Aloyce Nzuki kuwa Naibu atibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii. 

Katika hatua nyingine, Bw Christopher Ole Sendeka ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe kujaza nafasi ya Dk Rehema Nchimbi ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida. Dk Nchimbi anajaza nafasi ya Mhandisi Mathew Mtigumwe aliyeteuliwa kuwa katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 1295

Trending Articles