Mkuu wa Huduma za Kidijitali wa Tigo, Tawonga Mpore (kushoto), akizungumza Dar es Salaam jana, kuhusu kampuni hiyo kutambulisha zana mpya ya simu na kuboresha zana ya Tigo Pesa kwa watumiaji wa Smartphone. Kulia ni Mtaalamu wa Mawasiliano kutoka Tigo, Suleiman Asilia.
Mtaalamu wa Mawasiliano kutoka Tigo, Suleiman Asilia (kulia), akisisitiza jambo katika mkutano huo.
Wanahabari wakiwa kazini. |
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali Tigo Tanzania jana imezindua zana ya kipekee, ya kibunifu na sahihi ambayo inatoa njia rahisi ya kununua vifurushi vya tigo, kuboresha akaunti za wateja, kuangalia salio na muhimu zaidi kujiweka katika mkondo wa matumizi ya data.
Kampuni hiyo pia imeboresha zana yake ya Tigo Pesa kwa kuendelea kurahisisha njia ambazo wateja wake wanaweza kufanya miamala yao ya kifedha kwa njia ya simu.
Akielezea zana hizo kwa vyombo vya habari katika ofisi ya Tigo Jijini Dar es Salaam jana Mkuu wa Huduma za Kidijitali wa Tigo, Tawonga Mpore alisema, “Zana zote za Tigo na Tigo Pesa ni ubunifu ambao unayafanya maisha kuwa rahisi na sahihi zaidi kwa wateja wetu.
Wateja wetu wote wanaotaka kutumia zana hizo ni kiasi tu cha kuwa na kadi ya simu iliyosajiliwa, simu ya kisasa (smartphone) iliyo na iOS au inayoendeshwa na mifumo ya android.
Kitu wanachotakiwa kukifanya ni kupakua zana kutoka katika jukwaa husika na kufuata maelekezo rahisi ya kuanza kutumia zana. Hakuna haja ya kukumbuka njia ya mkato ili kufanya muamala. Halikadhalika ni njia nzuri sana ya kudhibiti matumizi yako husuasni katika uhifadhi wa data.”
Mpore aliongeza kuwa Tigo pia inazundua tena zana ya Tigo Pesa iliyoboreshwa ambayo itawawezesha watumiaji nchini kuzifikia pochi zao za Tigo Pesa katika njia sahihi na rahisi zaidi kuliko ilivyokuwa awali. Wateja wanweza kutuma pesa kutoka mtandao wowote, kilipia ankara (bili), kuhamishia benki, kuongeza salio na kutoa pesa vyote hivyo kwa ktumia smartphone zao.
Akizungumzia kuboreshwa kwa zana ya Tigo Pesa, Mkuu wa Huduma za Kifedha wa tigo Raun Swanepoel alisema, “Watumiaji wa Smartphone nchini wanweza kuendelea kufurahia miamala yao ya Tigo Pesa kama kawaida kwa kasi zaidi na kwa urahisi kwa kutumia zana mpya iliyoboreshwa ya Tigo Pesa.”
Swanepoel aliongeza; “Hivi sasa unaweza kuangalia namba za mawasiliano ulizohifadhi katika simu yako unapochagua kutuma pesa kupitia zana ya Tigo Pesa na hali kadhalika kuhifadhi malipo yako ya kawaida pamoja na kuhamisha fedha kutoka benki kwa haraka hapo baadaye.”
Alisema kutambulishwa upya kwa zana hii inayofahamika kama Tigo Pesa App mteja hatatozwa kwa data jambo ambalo ni sawa na ilivyo kwa Tigo App wakati unapingia katika utumiaji wa mtandao wa Tigo.
Hali kadhalika wateja wanaweza kuzifikia kuzifikia pochi zao za tigo Pesa wakiwa sehemu yoyote duniani kupitia mtandao wa intaneti usiotumia nyaya Wi-Fi au au data nyingine za simu zilizounganishwa ili mradi wawe na akaunti ya Tigo Pesa iliyosajiliwa.
“Faida nyingine ambayo imeletwa na zana hii kwa walio na akaunti ya fedha katika simu nchini inawapa uwezo wa wa kufikia kwa urahisi na kwa usahihi pochi moja kwa kutumia zama kadhaa,” alihitimisha mkuu huyo wa huduma za kifedha.