Baada ya kupuumzika kwa siku mbili katika kituo cha Horombo kwa ajili ya kuzoea hali ya hewa ,safari ya kuelekea kituo cha mwisho cha Kibo ikaanza .
Safari ilivyoendelea hali ya hewa ilibadirika arikadhalika uoto wa misitu mifupi ulianza kutoweka kadri safari ilivyoenedelea.
Eneo hili ndilo la mwisho katika Mlima Kilimanjaro kuona maji yakitiririka wakati wa safafri ya kupanda Mlima Kilimnjaro.
Kutokana na kubadirika kwa hali ya hewa ,washiriki wengine walivalia vizuia upepo,wenyewe walivipa jina "Shilawadu".
Baadae uoto wa misitu ukatoweka kabisa ,safari ikawa ni ya kupita katika eneo la jangwa likijulikana kama Saddle.
Washiriki wakapata picha ya pamoja kabla ya kupata mapumziko kujiandaa na safari ya kuelekea Kileleni itakayofanyika majira ya saa 5 usiku.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii aliyekuwa katika safari hiyo.