Quantcast
Channel: Mdimu's Blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1295

Mtanzania Kuongoza Kampuni Ya Filamu Marekani

$
0
0

Ernest Napoleon, ni muigizaji na mtayarishaji wa filamu kutoka Tanzania, aliyefahamika zaidi kupitia filamu ya Going Bongo, na hivi karibuni ataachia Filamu yake ya bongo movie , 'karibu kiumeni' akiwa na mastaa mbalimbali akiwemo Idris Sultan.

Ernest Napeleon amechaguliwa kusimamia kampuni ya kimataifa ya utengenezaji na usambazaji filamu, D Street Media Group, kama Rais, Kwa barani Afrika ikiwa na tawi lake Cape Town, Afrika Kusini.

D Street Media Group ni kampuni ya Kimarekani iliyozinduliwa rasmi mwaka 2003 ikiwa na malengo ya kukuza tasnia ya filamu. Ni kampuni inahusika na utengenezaji na usambazaji wa filamu za kimataifa nchini Marekani, Pia inahusika na kuandaa watengenezaji wa filamu zinazofanya vizuri katika soko la  filamu duniani.

Napoleon atasimamia zaidi kazi za kampuni hiyo upande wa Afrika na Mashariki ya Kati.

“Hii ni fursa ya kipekee katika hatua hii ya career yangu. D Street Media Group ni kampuni ya kujitegemea inayokua kwa kasi ikiwa imeshika kila upande wa dunia. Ni heshima kubwa kwangu kuendeleza biashara yetu katika masoko ya Afrika na Mashariki ya Kati ambayo nayaelewa vyema,” amesema Napoleon.

Aliendelea, “Naamini kuna fursa nyingi kwa kampuni ya Kimarekani kama D Street barani Afrika, na tukiwa na washirika sahihi kutengeneza maudhui mazuri, tutafanikiwa Afrika na hasa Marekani na nje ya nchi.”


Viewing all articles
Browse latest Browse all 1295

Trending Articles