Quantcast
Channel: Mdimu's Blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1295

Man City Kutumia Mgongo Wa Guardiola Kumpata Barnat

$
0
0

Matajiri wa mjini Manchester (Man City) wanajipanga kumsajili beki wa pembeni wa mabingwa wa soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich Juan Bernat.

City wamejipanga kumsajili Bernat kwa kutumia mgongo wa meneja wao Pep Guardiola, ambaye anadaiwa kuwa na mahusiano mazuri na uongozi wa FC Bayern Munich.

Gazeti la The Mirror la nchini England limeandika kuwa, Guardiola ameshinikiza usajili wa beki huyo kutoka nchini Hispania, kwa lengo la kukiongeza nguvu kikosi chake kuelekea mwishoni mwa msimu huu.

Gazeti hilo limedai kuwa, Guardiola amewasilisha ombi la kutaka kuwasajili mabeki wawili wa pembeni, na Barnat ni miongoni mwa alio wapendekeza.

Bernat alisajiliwa na Guardiola alipokua meneja wa FC Bayern Munich akitokea Valencia mwaka 2014.

Thamani ya Barnat inatajwa kufikia Pauni milioni 20m.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 1295

Trending Articles