Mwanasheria mkuu wa Kenya Bw Githu Muigai amesema Kenya imezindua mfumo wa app ya simu ya mkononi ili kusaidia mapambano dhidi ya uhalifu.
Amesema app hiyo itauwezesha umma kuripoti na kurekodi uhalifu wakati ukitokea.
Bw Muigai ameongeza kuwa mfumo huo wa kuripoti uhalifu utaimarisha mapambano dhidi ya uhalifu kwa kushirikisha wakenya wanaotumia simu za kisasa.
Imefahamika kwamba app hiyo inafaa kwa mifumo yote ya simu za mkononi.