Hoja ya album imekuwa hoja pana mno, na wapiga miluzi hodari wa vipindi vya mchana wamekuwa wahubiri wazuri juu ya album hailipi mara haiuzi huku wakiwa kimya juu ya umuhimu wa msanii kuwa na album.
Vannesa ni moja kati ya wasanii walioibuka miaka ya hivi karibuni na kuweza kufanya vyema kimuziki ndani ya nchi na nje pia.
Ni ukweli usiofichika wasanii wengi wamebaki chipukizi kwa kukosa album, hivyo katika muziki wa kizazi kipya tunaendelea kuwa na chipukizi wenye majina makubwa kila leo.
Vannesa ameweka wazi mpango wake wa kutoa album ambapo amesema ‘’umefika wakati sasa wa kutoa album, binafsi nikienda nchi za watu wenzangu wanauliza kuhusu album.
Lakini licha ya kutoa album nitafanya tour na nitauza huko pia katika mitandao album hiyo itapatikana.