Quantcast
Channel: Mdimu's Blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1295

Cristiano Ronaldo Apinga Kushindanishwa Na Lionel Messi

$
0
0

Mshambuliaji wa klabu bingwa duniani (Real Madrid) Cristiano Ronaldo amewataka waandishi wa habari kuacha kumfananisha na Lionel Messi wa FC Barcelona.

Ronaldo aliawaambia waandishi wa habari kuhusu suala hilo, baada ya kukabidhiwa tuzo ya kuwa mchezaji bora wa mwaka 2016, baada ya kuchaguliwa na mashabiki wa soka kutoka mashariki ya mbali (China).

Mshambuliaji huyo alisema hakuna haja kwa waandishi wa habari kujisumbua kuhusu uwezo wake na ule wa Lionel Messi, kwani anaamini kila mmoja ana uwezo wa kucheza soka.

"Cristiano ni Cristiano na Messi ni Messi," Ronaldo aliwaambia waandishi wa habari.


"Sote ni wachezaji wenye viwango vikubwa kisoka na tunacheza katika klabu kubwa duniani ambazo zina malengo ya kusaka mafanikio karibu kila msimu, hivyo kila mmoja ana ubora.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 1295

Trending Articles