Kundi la Al Shabaab la Somalia limeshambulia kambi ya jeshi la Kenya ambalo ni sehemu ya kikosi cha Tume ya kulinda amani ya Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM, iliyopo kusini mwa Somalia.
Maofisa wa usalama wa Kenya na Somalia wamethibitisha kuwa wana usalama wameteketeza magari mawili yaliyokuwa na mabomu ya kujitoa mhanga, yaliyokuwa yanatumiwa na wapiganaji wa kundi la Al Shabaab.
Shambulizi hilo limetokea katika eneo la Kulbiyow, ambako hali ya usalama kwa sasa imeimarishwa, na vikosi vya usalama vimewazingira washambuliaji.