Quantcast
Channel: Mdimu's Blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1295

Gareth Bale Kuikosa SSC Napoli

$
0
0
Picha inayohusiana
Bosi wa kikosi cha Real Madrid Zinedine Zidane amesema katu hawezi kucheza mchezo wa kubahatisha kwa kumtumia mshambuliaji wake kutoka nchini Wales Gareth Bale, katika mpambano wa ligi ya mbingwa barani Ulaya dhidi ya SSC Napoli.
Zidane aliwaambia waandishi wa habari kwenye mkutano maalum kuelekea mchezo huo wa 16 bora wa ligi ya mabingwa barani Ulaya, baada ya kuulizwa kama ana matarajio ya kumtumia mshambuliaji huyo hii leo.
Alisema ni mapema mno kumtumia Bale katika mchezo huo, kutokana na hali yake kutorejea kwenye mustakabali wa ushindani, hivyo ni bora akasubiri.
Hata hivyo meneja huyo kutoka nchini Ufaransa amesisitiza kuwa na kikosi imara hata kama hatomtumia Bale katika mchezo wa hii leo, hivyo hana shaka na kitakachojiri ndani ya dakika 90.
Bale alirejea mazoezini kwa mara ya kwanza mwanzoni mwa juma hili, baada ya kukaa nje ya uwanja tangu mwezi Novemba mwaka jana, baada ya kuumia kifundo cha mguu.

Kwa mara ya mwisho mshambuliaji huyo aliitumikia Real Madrid katika mchezo wa hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, walipocheza na Sporting Lisbon.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 1295

Trending Articles