Quantcast
Channel: Mdimu's Blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1295

Paul Scholes: Man Utd Imechelewa Kumleta Jose Mourinho

$
0
0
Tokeo la picha la jose mourinho and Paul Scholes

Aliyekua kiungo wa kutumainiwa wa klabu ya Man Utd pamoja na timu ya taifa ya England Paul Scholes, amesema uongozi wa mashetani wekundu umechelewa kumpa majukumu Jose Mourinho.

Scholes amefunguka kuhusu meneja huyo, baada ya kuona dalili za mabadiliko ambayo yalitarajiwa kwa kipindi kifupi kufuatia kuondoka kwa Sir Alex Ferguson.

Akihojiwa na gazeti la Daily Mail, Scholes alisema kulikua na umuhimu kwa viongozi wa Man utd kumfikiria Mourinho kwanza, kabla ya mameneja wengine waliomtangulia, ambao walishindwa kuonyesha dalili za mafanikio.

 “Ana kila kitu cha kukushawishi kuamini anastahili kuwa meneja wa klabu kubwa kama Man Utd, hili ndilo lilihitajika tangu mwanzo na sio kubahatisha," Alisema Scholes.

 “Ninatamani haya ninayoana sasa, ningeyaona miaka mitatu iliyopita, hii leo Man Utd ingekua mbali kimaendeleo!

“Tulikubali kujibebesha mzigo wa kujaribu baadhi ya watu waliopita klabuni hapa, lakini tulijua mambo yangekua magumu kutokana na ukubwa wa klabu hii, na leo tumeona ukiwa na mtu anaejua majukumu yake, kuna jambo unalipata.”

Baada ya Sir Alex Ferguson kuondoka, Man Utd ilimuajiri David Moyes ambaye alitimuliwa miezi kadhaa iliyofuatia, na kisha Louis Van Gaal alikabidhiwa jukumu la kuliongoza benchi la ufundi klabuni hapo.


Van Gaal aliondoka mwishoni mwa msimu uliopita baada ya kukiwezesha kikosi cha Man utd kutwaa ubingwa wa kombe la FA.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 1295

Trending Articles