Kenya, Uganda na Rwanda zimeanzisha mradi wa mtandao wa Internet unaolenga kuunganisha soko la utalii la nchi hizo ili kuvutia zaidi watalii kutoka nje.
Habari zinasema, nchi hizo zinapanga kujenga jukwaa kwa wafanyabiashara wa utalii wa Afrika Mashariki ili waweze kutangaza na kutoa huduma ya utalii katika nchi hizo tatu kwa wakati mmoja.
Hivi sasa soko la utalii la Afrika Mashariki sio tu linakabiliwa na ushindani mkali na maeneo mengine ya Afrika, bali pia linashindana na Mashariki ya Kati, eneo la Caribbean na Latin America.