Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, amevitaka vyombo vya habari kuwa huru huku akisema kuwa serikali haina uadui hivyo vyombo hivyo havipaswi kuigopa kwa sababu imebeba dhamana kubwa ya kuliongoza taifa.
Amezungumza hayo katika mkutano na wahariri na wamiliki wa vyombo vya habari Dar es Salaam na kusema vyombo vya habari vinatakiwa kuwaleta pamoja Watanzania katika uchumi wa viwanda ili kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo.
“Serikali ni rahisi sana kujisahau, ama inaweza ikaziba masikio, hivyo ni lazima pawepo na ‘very strong media’ zitakazofanya kazi ya kuiambia serikali kwa namna fulani ya heshima, lakini ujumbe unafika.”
“Najua kuna hofu na lazima tuchukue hatua tuiondoe, kwa sababu ikiendelea kuwepo watu watabaki na mafundo fundo na si vizuri katika nchi. Hivyo muwe huru, Serikali si adui, nguvu yenu ni kubwa na msiposhiriki kikamilifu tutawaacha Watanzania wengi nyuma,” alisema Nape.