DUBAI,
Kampuni ya flydubai yenye makao makuu Dubai imetangaza leo matumizi ya bilioni US$27 kununua ndege 225 aina ya Boeing 737 MAX kwenye harakati zake za kuchangia upanuzi wa huduma za usafiri.
Hii ni mara ya tatu kwa kampuni hiyo kununua idadi kubwa ya ndege kutoka kwa kampuni ya Boeing katika kipindi cha miaka minane. Mara za mwisho kwa kampuni hiyo kuagiza ndege zingine ilikuwa miaka ya 2008 na 2013. Ndege hizi mpya zitaimarisha huduma za usafiri ambazo kampuni hii imeendelea kupanua. Ndege hizi zinahudumia eneo lenye zaidi ya watu 2.5 bilioni.
Kufikia mwisho wa mwaka huu, kampuni hii itakuwa na ndege takriban 61 aina ya Next-Generation Boeing 737-800 na pia zingine aina ya Boeing 737 MAX 8. Kadhalika, kampuni imeagiza ndege zingine 70 ambazo zinatarajiwa kuwa tayari kufikia mwaka 2023.
Mwenyekiti wa kampuni ya flydubai, Sheikh Ahmed bin Saeed Al Maktoum, alisema haya kuhusu ununuzi wa ndege hizo: "agizo hili la ununuzi wa ndege hizi flydubai, ni dhihirisho la ufanisi mkuu wa kampuni yetu. Hali hii inaonyesha wazi mwelekeo wetu kuhusu uimarishaji wa usafiri.
Lengo letu ni kuboresha biashara na utalii ya flydubai katika sehemu zote ambazo tunahudumia kutoka eneo la Dubai. Katika kipindi kisichozidi miaka kumi, kampuni ya flydubai imeeneza huduma zake kufikia sehemu 97 katika nchi 44. Ni matarajio yetu kwamba pindi tu zitakapofika hizo ndege mwaka wa 2019 ili zitaboresha zaidi huduma zetu za usafiri."
Kufuatia tangazo hili, sasa, kampuni ina takriban ndege 320.
Msimamizi Mkuu wa kampuni, Ghaith Al Ghaith, aliongeza: "Leo ni siku muhimu mno kwenye ufanisi wetu katika huduma za usafiri. Tangu tulipoanza kutoa huduma mwaka wa 2009, kampuni ya flydubai imefungua afisi 67 katika sehemu ambazo awali hazikuwa zinapata huduma hizo. Tunakaribisha upya ushirikiano wetu na kampuni ya ndege ya Boeing. Tumeagiza aina hii ya ndege kwa vile imetupa huduma nzuri. Tangu tulipoanza huduma hizi, kampuni yetu imesafirisha takriban wasafiri milioni 44.
“Ni heshima kubwa kwetu kwamba kampuni ya flydubai imeamua kutumia ndege aina ya Boeing na itazidi kuzitumia kwa miaka mingi ijayo. Makubaliano haya maalum yanadhihirisha ushirikiano mzuri uliopo baina yetu na kampuni ya flydubai na kampuni zingine za usafiri sehemu hizi," akasema Rais na Kinara Mkuu wa Boeing Kevin McAllister.
Kwa kutegemea utendaji murua wa biashara wa kampuni ya flydubai, tunatarajia huduma bora sana kutoka kwa ndege hizi mpya za 737 MAXs zinazounganisha Dubai na sehemu zingine za ulimwengu.
Kampuni ya flydubai ilianza mwaka wa 2008 ili kutoa huduma bora za usafiri na utalii na biashara. Lengo letu ni kuimarisha usafiri kwa kutegemea ndege aina ya Next-Generation Boeing 737-800 and Boeing 737 MAX 8.