
Zaidi ya watu 100,000 wanatarajiwa kujitokeza katika ibada ambayo itafanyika kwenye uwanja wa michezo wa Chapeco mara baada ya miili hiyo kuwasili nchini brazil.
Ni watu 6 walionusurika kwenye ajali hiyo iliotokea siku ya Jumatatu.

Rais wa Brazil Michele Temer atatoa ndege ya kijeshi ambayo itabeba maiti hizo.
Bwana Temer anatarajiwa kuwapa tuzo katika sherehe katika uwanja wa ndege wa Chapeco -nyumbani kwa wachezaji hao, Kusini mwa Brazil.
chanzo:bbc