Ramani mpya iliyotolewa na Tanzania ambayo inaonyesha kuwa inaamiliki nusu ya Ziwa linalozozaniwa la Malawi au Nyasa, imezua mzozo Upya na Malawi ambayo inasema kuwa ramani hiyo si sahihi.
Ramani ya Tanzania inaonyesha kuwa eneo hilo lote ni lake.
Malawi imeomba Umoja wa Mataifa, Muungano wa Afrika na mashirika mengine ya kimataifa kuingilia kati.
Msemaji wa wizara ya mashauri ya nchi za kigeni nchini Malawi, Rejoice Shumba amesema kuwa Malawi imeandika barua kwa mashirika makuu duniani ikiyataka kutupilia mbali ramani ya Tanzania.
chanzo:bbc