Quantcast
Channel: Mdimu's Blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1295

DARASA HURU: Urafiki wa jinsia tofauti kwa vijana, ni jambo la kawaida?

$
0
0
Kaka na dada zangu, hii ni makala nyingine niliyowahi kubuni ambayo nimeona ni vema niilete mtandaoni tuendelee kuelimika kwa majadiliano ya hapa na pale.

Imani niliyonayo ni kwamba cadre tnavyoenelea kuishi, ndivyo changamoto za kimaisha zinavyoendelea kutupa somo la maisha yetu ya kila siku. Sasa karibuni tuendelee kujifunza na kuelimika kupitia blog hii, mwandishi wa makala hii naitwa Henry Mdimu ambaye ndio mmiliki wa Blog hii.

Salamu za kheri zikufikie popote pale ulipo na pia shukrani za dhati kutoka kwangu kwa kuamua kuanza kusoma makala yangu hii, bila shaka utaupenda muendelezo wa darasa huru ambao wanachama wapya wapatikana. Ahsanye kwa kuwa mmoja wa wasomaji.

Sisi hapa twapeana darasa kuhusiana na maisha yetu ya kila siku. Mambo tunayokutana nayo na jinsi ya kukabiliana nayo lakini pia kuna angalizo ambalo kila kukicha yabidi nilikumbushe na sijui kama mwalizingatia kaka na dada zangu.

Ni hivi:
…mwandishi wa makala hizi ni binadamu tu wa kawaida ambaye kuna wakati hukosea, sasa basi si lazima uamini kila analoandika, baada ya kumaliza kusoma makala hii waweza amua mwenyewe lipi la kuchukua na lipi la kuacha na ndio sababu ya darasa hili kuitwa huru.

Upo mwenzangu?
Haya...
Leo kuna moja kubwa lakini zuri kulijadili na lahusiana na urafiki wa mtoto wa kiume na kike, bila kuingiza mapenzi, we wadhani yawezekana?

Muda wako ni muhimu sana katika hili naomba twende pamoja tuone mtazamo wangu na wewe utaupima utachanganya na mawazo yako kisha utajua mwisho wa siku, mchele u wapi, na pumba ni zipi au sio jamani?

1. Kwani lazima?
Eti jamani kwani urafiki wa mtoto wa kiume na kike kwani lazima? Hatuwezi kupotezeana tu tukaja kukutana kwenye ndoa huku jamani?

Hili swali niliwahi kujiuliza kipindi fulani lakini nikashushuka, ujue ki vipi? Nilikuja kugundua kwamba nimejiuliza swali ambalo halina maana kwani jibu lake liko wazi. Jibu lake limekaa hivi, katika maisha yako ya kila siku, bado unajifunza ujue, na utaendelea kujifunza mpaka siku ambayo utaingia kaburini, huo ndio utakuwa mwisho wako.

Sasa kama marafiki wangekuwa wanajibagua, kwamba watoto wa kiume marafiki zao ni watoto wa kiume wenzao na watoto wa kike, marafiki zao wakiwa watoto wa kike wenzao tungepata wapi kujuana vizuri?
Umeona?

Kwa hiyo kuna haja ya kuwa na marafiki wa jinsia tofauti ili kujua vizuri maisha ya mtoto wa kike lakini mkijibagua siku ukiwa naye itakuwa ngumu kumsoma na kumjua mwenzio, maana huna uzoefu nao aidha awe wa kike au wa kiume si ndio jamani?

2. ...na haya mambo ya mapenzi sasa?
Mpaka leo watu wanashindwa kujua inakuwaje mpaka marafiki wa kawaida ambao mwanzoni kwa lugha ya ujana twaweza kuwaita ni washkaji tu mwisho wa siku unakuta washaingia kwenye dimbwi ziiito la mahaba, huwa inatokea nini?

Wakati mwingine ni ukaribu wa kupitiliza ambapo watu hujikuta wamezoeana kupita kiasi na wakati mwingine wanakuwa labda wamepitia misuko suko mbali mbali na kujikuta wakifarijiana, sasa zile faraja ndio mwisho wa siku zinakuja kugeuka mapenzi na wakati mwingine basi tu, kuna watu nilikwakuta wamejikuta tu, tayari!

Sasa hili ni tatizo ujue na mapenzi yakianza urafiki unakuwa hamna tena, yanakuwa mapenzi ambayo mara nyingi kama mlikuwa mnafanya kitu cha maana, kama marafiki hata kama ni mradi hv ujue utapotea ghafla na mtajikuta mkiangalia mapenzi kuliko hata lile jambo ambalo ni muhimu kwenu wote pengine.

..halafu mwisho wa siku mnakuja kumtafuta aliyewaroga wakati wachawi ni nyie wenyewe wawili, mmechanganya madawa!

3. Mipaka vipi?
Mjue jamani hakuna linaloshindikana chini ya jua kwa kweli, binadamu aliyeumbwa na Mungu akiamua lake kiukweli kabisa kutoka moyoni huwa linawezekana kwa asilimia nyingi tu.
Unanielewa?

Sasa kwangu mimi kama Henry Mdimu tu wa kawaida urafiki na mtoto wa kike naweza kikubwa hapa ni kujiwekea mipaka tu kwamba huku tusifike, urafiki wetu ni katika hili na hili na lile, baaaas...
Au mwaonaje wad?

Mkitaka kuwa karibu ile kupita kiasi ndio matatizo yanapoanzia sasa, mara mmepelekeana zawadi, mara "ooh nimekumisi", mara sijui kutembeleana, mara tutoke tukapate kinywaji, hapo ndio mnajenga na mambo mengine maana kuna siku mtasingizia pombe au mtajikuta mko mahala wawili tu na wapweke, unafikiria kifuatacho nini?
..sema...

…kwa hiyo ipo haja ya kuwekeana mipaka ili mwisho wa siku muwe katika maadili mliyojipangia tangu awali, naomba kuishia hapa kwa leo tuonane wiki ijayo au sio jamani, ila mawasiliano yapo

+255 787 000 880
Mdimuz@gmail.com

Viewing all articles
Browse latest Browse all 1295

Trending Articles