Quantcast
Channel: Mdimu's Blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1295

Chelsea na Manchester City wapigwa faini

$
0
0
Chelsea wamepigwa faini ya £100,000 na Manchester City wamepigwa faini ya £35,000 baada ya wachezaji wao kuhusika katika vurugu uwanjani wakati wa mechi ya Ligi ya Premia.
Hisia zilipanda na wachezaji wakakabiliana mechi hiyo iliyochezewa uwanjani Etihad ilipokaribia kumalizika baada ya Sergio Aguero wa City kufukuzwa uwanjani kwa kumchezea visivyo beki wa Chelsea David Luiz.
Fernandinho pia alifukuzwa uwanjani kwa kumkaba koo Cesc Fabregas wachezaji wa klabu hizo mbili walipokabiliana baada ya kisa hicho.
Chelsea walishinda 3-1.
Blues walikuwa awali wametahadharishwa kwamba wanaweza kupokonywa alama kwa utovu wa nidhamu.
Viongozi hao wa Ligi ya Premia wamepigwa faini mara sita tangu Februari 2015 kwa kushindwa kuwadhibiti wachezaji.
Chanzo.BBC

Viewing all articles
Browse latest Browse all 1295

Trending Articles