Quantcast
Channel: Mdimu's Blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1295

TIGO YATOA DOLA 40,000 KUENDELEZA MIRADI YA WAJASIRIAMALI-JAMII

$
0
0

Dar es Salaam, -Kampuni ya Tigo ikishirikiana na shirika lisilokuwa la kiserikali la Reach for Change wametoa jumla ya dola 40,000 kwa washindi wawili wa shindano la ubunifu kwa wajasiriamali wanaotumia teknolojia ya kidijitali. Kila mshindi amepewa dola 20,000.

Shindano hilo ambalo ni la nne tangu lilipoanzishwa mwaka 2012, lina lengo la kuwawezesha wajasiriamali wanaobuni miradi ya teknolojia ya kidijitali inayosaidia kutatua changamoto mbalimbali za kijamii.

Washindi wa mwaka huu ni Neema Shosho ambaye kwa kupitia kampuni yake ya Afya Slices, amebuni mfumo wa teknolojia ya kidijitali unaotoa taarifa kuhusu lishe kwa watoto na Bihage Edward, aliyebuni mradi wa kutunza vifaa vya elimu kidijitali unaosaidia kutokomeza ajira kwa watoto na kusambaza taarifa kwa njia ya ujumbe mfupi kwa kutumia simu za mkononi na kutengeneza programu ya Mp3 mahsusi kwa kutoa uelewa kuhusu ajira kwa watoto kwa jamii nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Afisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Shavkat Berdiev alisema: “ni furaha kubwa kwetu kuwatangaza washindi wa mwaka huu wa shindano la ubunifu la Tigo Digital Change-Makers. Kwa muda wa miaka minne sasa shindano hili limewanufaisha zaidi ya watoto 10,000 nchini na tunaamini kuwa ongezeko la washindi wawili litaleta mabadiliko zaidi kwa watoto na kusaidia kuifanya Tanzania kuwa mahala pazuri pa kushi.

Berdiev alifafanua kwamba maisha ya kidijitali yanakuza teknolojia yenye mawazo ya kuleta mabadiliko endelevu. “Teknolojia ya kidijitali haibadilishi tu jinsi tunavyofanya biashara ila pia inasaidia kukuza biashara barani Afrika na vilevile kuleta mapinduzi ya jinsi ya kutatua matatizo  mbalimbali yanayohusu maendeleo ya kijamii kwa ujumla”, alisema Berdiev.

Huu ni mwaka wanne ambapo Tigo na shirika la Reach for Change wanazindua washindi wa shindano hili ambapo washindi huchujwa kutoka kwenye washindani vijana ambao wana mwamko wa kubuni miradi inayotumia ya kiditali ili kutatua matatizo mbalimbali ya vijana na watoto katika jamii ya Watanzania.

Afisa Mkuu wa Biashara huyo alisifia kazi mbalimbali za washindi waliotangulia na kuwatia moyo wengine ili waendelee kubadilishana mawazo.

“Tumepata mafanikio makubwa sana katika kuwapa msukumo wajasiriali-jamii. Kwa sasa tunasasidia waleta mabadiliko saba ambao kati yao, watano wana miradi inayoshughulika na masuala ya kidijitali”. Kwa mfano, Carolyne Ekyariisma anafundisha masomo ya awali ya kompyuta ili kuwapa uwezo vijana wa kike wenye umri kati ya 10 na 18 ujuzi wa awali katika kutumia kompyuta na amefanikisha kuwapa ujuzi takribani wanafuzi 500 kwa mwaka 2014 pekee.

Mwingine ni Joan Avit ambaye amejikita katika kutoa elimu bora ya awali ya watoto kwa kuieneza kupitia njia ya michezo ya kidijitali inayojulikana kama Grapho Game Tanzania inayowasaidia watoto kujifunza kusoma kwa haraka na kwa makini na ameweza kuwasaidia watoto 900 kwa mwaka 2014 pekee kupitia mchezo huu. Naye Faraja Nyalandu anayeendesha mradi wa shule, alibuni maarifa ya elimu kudijitali ili kuwawezesha watoto na vijana kusoma kwa kupitia mtandao wa kompyuta na huduma za simu ya mkononi. Kwa kutumia nyenzo hizi aliweza kuwaweze sha zaidi ya watoto 7,300 mwaka 2014.

Vile vile, tunamuwezesha  Thadei Msumanje ambaye amejikita katika kupunguza pengo lililopo kati ya watumiaji wa tehama mjini na vijijini ambapo ni watoto wachache tu wanao uwezo wa kutumia tehama mpaka sasa.

Kuna pia Leka Tingitana ambaye ni mtaalamu wa teknolojia; naye kabuni suluhisho la tatizo katika sekta ya afya ili kuinua mtandao wa wafanyakazi wa afya ambao wako mstari wa mbele katika kutoa huduma za afya kwa akina mama wajawazito”.

Balozi wa Sweden nchini Tanzania Bi. Katarina Rangnitt, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo aliahidi kutoa msaada na kuunga mkono juhudi za shindano hilo kupitia shirika la msaada la Swedish Development Cooperation Agency (SIDA), na kusema ataungana na Tigo ili kufanikisha shindano la kila mwaka la ubunifu wa miradi ya kidigitali unaofanywa na wajasiriamali-jamii wa kitanzania.

“Kwa miaka mingi sasa shirika la maendeleo la SIDA limekuwa mstari wa mbele kuunga mkono miradi mbalimbali ya maendeleo hapa Tanzania katika harakati za kupunguza umasikini uliokithiri miongoni mwa wananchi hasa vijana, watoto na akina mama”, alisema.

Alisema ya kwamba amefarijika mno kwamba sasa nchi yake itashirikiana na kampuni ya Tigo ambayo ni taasisi inayojituma kwa dhati katika kutekeleza malengo yake ya kuisaidia jamii hapa Tanzania kwa kubuni fursa mbalimbali za maendeleo ili kukusanya mawazo ya kuleta tija katika jamii ya watanzania.

pichani juu: Balozi wa Sweden nchini, Katarina Rangnitt (wa pili kulia) akikabidhi mfano wa hundi ya dola za marekani 20,000 kwa mshindi wa shindano la Tigo Reach For Change, Bihage Edward kwenye hafla ya makabidhiano iliyofanyika Dar es Salaam jana. wanaoshuhudia ni Ofisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Shavkat Berdiev (kulia) na Meneja Mkazi wa Reach For Change, Peter Nyanda (kushoto).

 Balozi wa Sweden nchini, Katarina Rangnitt (wa pili kulia) akikabidhi cheti kwa kwa mshindi wa shindano la Tigo Reach For Change, Neema Shosho kwenye hafla ya makabidhiano iliyofanyika Dar es Salaam jana. wanaoshuhudia ni Ofisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Shavkat Berdiev (kulia) na Meneja Mkazi wa Reach For Change, Peter Nyanda (kushoto). 

Balozi wa Sweden nchini, Katarina Rangnitt (wa pili kulia) akikabidhi mfano wa hundi ya dola za marekani 20,000 kwa mshindi wa shindano la Tigo Reach For Change, Neema Shosho kwenye hafla ya makabidhiano iliyofanyika Dar es Salaam jana. wanaoshuhudia ni Ofisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Shavkat Berdiev (kulia) na Meneja Mkazi wa Reach For Change, Peter Nyanda (kushoto). 

Balozi wa Sweden nchini, Katarina Rangnitt (wa pili kulia) akikabidhi cheti kwa kwa mshindi wa shindano la Tigo Reach For Change, Bihage Edward kwenye hafla ya makabidhiano iliyofanyika Dar es Salaam jana. wanaoshuhudia ni Ofisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Shavkat Berdiev (kulia) na Meneja Mkazi wa Reach For Change, Peter Nyanda (kushoto). 



Viewing all articles
Browse latest Browse all 1295

Trending Articles