Quantcast
Channel: Mdimu's Blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1295

Majimaji FC Kumsubiri Mshindi Wa Mighty Elephant Vs Shujaa FC

$
0
0

Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF) limeamuru mchezo wa mzunguuko wa nne ya Kombe la Azam Sports Federeation Cup HD (ASFC) kati ya Mighty Elephant na Shujaa ya Kigoma urudiwe Jumatano.

Hatua hiyo inafuatia TFF kuikubali rufaa ya timu ya Shujaa kupinga Mighty Elephant kupewa ushindi wa mezani.

Shujaa haikutokea kwenye mchezo dhidi ya Mighty Elephant Uwanja wa Maji Maji mjini Songea na wapinzani wao wakapewa ushindi wa mezaji, hivyo kupangwa kumenyana na Maji Maji ya Songea juzi katika Raundi ya Tano.

Hata hivyo, saa chache kabla ya kufanyika mchezo kati ya Maji Maji na Mighty Elephant juzi Uwanja wa Maji Maji, TFF ikaufuta mchezo huo.

Na lengo ni kutaka Might Elephant imenyane kwanza na Shujaa na mshindi ndiye atakwenda kucheza na Maji Maji.

Michuano ya Kombe la ASFC inatarajiwa kuendelea leo kwa Stand United kuwa wageni wa Polisi Mara Uwanja wa Karume (Musoma Mjini), Azam FC na Cosmopolitan Uwanja wa Azam Complex Chamazi na Ndanda FC dhidi ya Mlale JKT Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.



Viewing all articles
Browse latest Browse all 1295

Trending Articles