Quantcast
Channel: Mdimu's Blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1295

Droo Ya Fainali Kombe La Dunia - Russia 2018 Kufanyika Desemba Mosi

$
0
0

Shirikisho la soka duniani FIFA limethibitisha kuwa Droo za kupanga Makundi na Mechi za Fainali za Kombe la Dunia la Mwaka 2018 itafanyika Ijumaa Desemba mosi huko Kremlin Jijini Moscow.
Wakati tarehe ya Droo ilikuwa ishajulikana, mahali pa kuifanyia palikuwa bado hapajatangazwa hivyo kwa kuichagua Kremlin, Russia imeonyesha jinsi inavyoipa kipaumbele fainali hizo.
Russia walishinda Kura za kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la Dunia za Mwaka 2018 zilizofanyika Desemba 2010 kwa kuwabwaga Wagombea wengine ambao ni Ubelgiji. Uholanzi (Waliotaka kuwa Wenyeji wenza), Uingereza na Hispania Waliotaka kuwa Wenyeji wenza.
Kuanzia Juni 17 na Julai 2 Mwaka huu, Russia watakuwa Wenyeji wa Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara, FIFA CONFEDERATION CUP, ambalo washindani wake ni Russia, kama Mwenyeji, Mabingwa wa Dunia Germany na Mabingwa wa Mabara 6 Duniani amvao ni Australia, Chile, Mexico, New Zealand, Portugal na Bingwa wa AFCON 2017, Kombe la Mataifa ya Afrika ambazo Fainali zake zinaendelea hivi sasa huko Gabon.
 Ni desturi kwa Mashindano hayo kufanyika kwa Nchi Mwenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia Mwaka mmoja kabla Fainali zenyewe ili kupima uwezo wao kuandaa Mashindano makubwa.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 1295

Trending Articles