Msemaji wa serikali ya Kenya Eric Kiraithe amesema zaidi ya raia 90 wa Somalia na Kenya wamewasili Nairobi baada ya kufukuzwa Marekani.
Kiraithe amesema waliofukuzwa ni wanaume 90 kutoka Somalia na wanawake wawili kutoka Kenya, lakini amesema hajui ni kwa nini wamefukuzwa kutoka Marekani.
Tukio hilo limetokea kabla ya rais Donald Trump wa Marekani kusaini amri kuhusu kupiga marufuku wakimbizi na kusimamisha utoaji visa kwa raia wa Syria na nchi nyingine za Mashariki ya Kati na Afrika.