Mjumbe wa Umoja wa Afrika anayeshughulikia mambo ya rasilimali watu, sayansi na teknolojia Martial De-Paul Ikounga amesema, pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" litasaidia kuimarisha ushirikiano kati ya Afrika na China katika kuendeleza rasilimali watu barani Afrika.
Akihojiwa na waandishi wa habari huko Addis Ababa Ikounga amesema Afrika inatakiwa kuongeza uwekezaji katika vijana, ili kuvumbua na kutekeleza miradi ya maendeleo endelevu.
Pia amesema Afrika inahitaji pendekezo la China na "Ukanda MMoja na Njia Moja" na pande hizo mbili zinatakiwa kuimarisha ushirikano katika kutoa mafunzo kwa vijana wa Afrika, ili Afrika iweze kujiendeleza yenyewe.
Ikounga amedokeza kuwa, Umoja wa Afrika unapanga kuzindua mradi wa kuwaunga mkono vijana, ambao utatoa mwongozo kwa nchi wanachama kuhusu njia ya kuwekeza kwa ufanisi zaidi na kuwavutia vijana kujihusisha katika sekta za afya, elimu na ajira.