Quantcast
Channel: Mdimu's Blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1295

Ujerumani Yakosoa Sheria Ya Kibaguzi Ya Marekani

$
0
0

Kansela wa Ujerumani amekosoa hatua ya Rais wa Marekani Donald Trump kupasisha sheria ya kuwazuia wakimbizi na raia wa nchi saba za Kiislamu kuingia Marekani.

Angela Merkel, amesema jitihada za kimataifa za kupambana na ugaidi hazifai kutumiwa kama kisingizio cha kuhalalisha sheria hiyo ya kibaguzi.

Merkel ameyasema hayo katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na Trump na kumkumbusha rais huyo mpya wa Marekani kuhusu umuhimu wa kuheshimiwa Mkataba wa Geneva, unaoitaka jamii ya kimataifa kuheshimu haki za wakimbizi katika misingi ya ubinadamu.

Naye  Steffen Seibert, msemaji wa Kansela wa Ujerumani amesema kuwa, kupambana na ugaidi hakuipi nchi yeyote sababu ya kumshuku na kumbagua mtu kwa misingi ya imani yake ya kiroho.

Wakati huohuo, chama cha Green Party cha Ujerumani kimekosoa sheria hiyo ya kibaguzi ya Marekani na kubainisha kuwa, Donald Trump sio mshirika wa kutegemewa tena na Ujerumani.


Ijumaa iliyopita, Trump ilipasisha sheria ya kutoruhusiwa nchini Marekani kwa muda wa miezi mitatu wakimbizi na watu kutoka nchi zenye idadi kubwa ya Waislamu, ambazo ni Iran, Iraq, Libya, Somalia, Sudan, Syria na Yemen, kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 1295

Trending Articles