Mwandishi Wetu,
Watoto wachanga wanaozaliwa na tatizo la tundu kwenye moyo, linalosababishia kudumaa katika ukuaji wao na hata kuwa na matatizo ya moyo wanashauriwa kupata matibabu ya kuziba tundu hilo kwa njia ya mrija bila kufanyiwa upasuaji. Hayo yamesemwa na DK.C.S Muthukumaran, mtaalamu wa magonjwa ya moyo kwa watoto kutoka hospitali za Apollo.
Watoto wachanga wanaozaliwa na tatizo la tundu kwenye moyo, linalosababishia kudumaa katika ukuaji wao na hata kuwa na matatizo ya moyo wanashauriwa kupata matibabu ya kuziba tundu hilo kwa njia ya mrija bila kufanyiwa upasuaji. Hayo yamesemwa na DK.C.S Muthukumaran, mtaalamu wa magonjwa ya moyo kwa watoto kutoka hospitali za Apollo.
(VSD) ni tundu katika ukuta unaotenganisha ventriko ya upande wa kulia na kushoto katika moyo. Ni tatizo linalotokea mara nyingi wakati wa kuzaliwa kwa mtoto na linaweza tokea lenyewe au kama ugonjwa.
Ni kawaida kwa watoto wote kuzaliwa na tundu dogo katikati ya atria mbili na mara nyingi tundu hilo huziba ndani ya wiki chache. Mara nyingi hakuna tundu kati ya ventiko hizo mbili, ila baadhi ya vichanga huzaliwa na tundu hilo ambalo linakuwa ni chanzo cha magonjwa ya moyo na ndio sababu kubwa ya watoto wachanga wengi kuonana na wataalamu wa magonjwa ya moyo.
Imezoeleka mara zote kuziba tundu hili kwa upasuaji wa moyo (operesheni), ambao unahusisha kupasua kifua, kupitisha mashine na kuziba tundu hilo. Kwa mujibu wa DK.Muthukumaran kwa miaka 10 iliyopita kumekuwa na maendeleo makubwa ya kutibu tatizo hili ambapo hospitali za Apollo wamegundua njia ya kuziba tundu hilo kwa kutumia njia ya “pini kwenye tundu” (angiogram) bila kovu lolote kifuani. Licha baadhi ya aina za tundu hilo kwenye moyo kama lile lililopo chini ya valvu za moyo ni lazima lizibwe kwa upasuaji. Makala hii inaonyesha jinsi gani tundu hilo katika moyo linaweza kuzibwa bila upasuaji au wowote.
Mtoto wa kike wa umri wa miaka 12 amekuwa na tatizo la moyo. Aligundulika akiwa na tundu katika moyo akiwa na umri wa miaka miwili. Madaktari walishauri afanyiwe upasuaji kwa sababu tundu lilikuwa karibu sana na valvu hivyo ingeweza kuharibu valvu ya moyo. Wazazi wake waliogopa suala la binti yao kufanyiwa upasuaji huo ambao ungeweza kusababisha apoteze maisha lakini pia kuwa na kovu kubwa kifuani. Waliahirisha upasuaji huo mpaka pale binti alipofikisha umri wa miaka 14. Kwa umri huo tayari lile tundu lilikuwa limeshaanza kuharibu ile valvu iliyokuwa karibu nalo.
Wazazi walikwenda hospitali ya watoto Apollo kwa ajili ya ushauri mwezi Septemba 2014. Baada ya utafiti wa kwanza madkatari walisema wanashauri tundu lile lizibwe kwa njia ya “pini” bila kufanya upasuaji. Baada ya wazazi kuelewa, walimchukua mtoto kwa ajili ya maandalizi. Hatua za maandalizi zilifanywa mtoto akiwa katika nusu kaputi (local anaesthesia). Hatua hizo zilichukua nusu saa tu. Tundu hilo lilizibwa kwa mafanikio makubwa kwa njia ya pini na katheta na mgonjwa aliruhusiwa kutoka hospitalini siku iliyofuata. Familia ilifurahi sana, kwa jinsi walivyotua mzigo mkubwa wa tatizo hilo la binti yao wa miaka 14.
Wakati wa ufuatiliaji wa maendeleo kwa muda wa mwaka mmoja, binti alikuwa akiendelea vizuri, hakukuwa na uvujaji wowote wala tatizo katika aortic na valvu za upumuaji. Tiba hii ya siku moja imemwezesha binti huyu kuepuka upasuaji katika mfumo wake wa upumuaji, kovu kubwa la maisha yake kifuani na siku 5-6 za kulala hospitali kwa ajili ya upasuaji.
Uzibaji wa tundu katika moyo umekuwa ukifanywa kwa mafanikio kwa muda wa miongo miwili. Ufuatiliaji wa maendeleo kwa muda mrefu umeonyesha kuwa uzibaji wa tundu katika moyo kwa njia hii mpya ijulikanayo kitaalamu kama ‘Transcatheter’ ni mbadala bora wa kuepuka upasuaji. Kwa kipindi kirefu upasuaji umekua njia pekee ya kuziba tundu katika moyo. Ila ina kuwa hatarishi mara kadhaa hasa moyo kuziba kabisa, baada ya kufanyiwa upasuaji zaidi ya mara moja na hata vifo. Zaidi ya yote, matatizo ya maambukizi, mfumo wa fahamu na mapigo ya moyo kwenda kasi zaidi (tachyarrhythmia). Baada ya kufanyiwa upasuaji, kovu litadumu maisha yote. Hivyo kwa njia ya hii mpya ya kuziba tundu ni bora na salama kwa afya ya baadae.
Dk. C.S Muthukumaran ametoa maoni yake kwamba, kurithi ni moja kati ya sababu kubwa za kusababisha tundu katika moyo. Kwa mfano, mzazi mwenye tatizo la tundu kwenye moyo ana nafasi kubwa ya kupata mtoto mwenye hali hiyo zaidi ya mazazi asiye na tatizo hilo. Watoto wenye maradhi ya kurithi kama utindio wa ubongo mara nyingi huwa na tundu katika moyo. Uvutaji sigara kipindi cha ujauzito kwa mama kumehusishwa pia kama chanzo cha matatizo haya ya tundu katika moyo wa mtoto.
Kama tatizo hilo la tundu katika moyo lisipopatiwa matibabu huwa linaweza kusababisha matatizo ya moyo, anasema Dk. Muthukumaran. Ukuaji wa tundu hilo katika moyo inaweza kusababisha moyo kushindwa kuendelea kusukuma damu, au kuwa na mapigo yasiyo sahihi, kudumaa kwa mwili hasa kwa watoto wachanga. Mtoto anashindwa kula sawa sawa na hivyo kuathiri ukuaji wake. Na matokeao yake mtoto anapungua uzito au asikue kabisa.
Katika hospitali ya watoto ya Apollo uzibaji wa tundu katika moyo kwa njia ya Transcatheter umefanywa kwa zaidi ya watoto 300 kwa miaka 5 iliyopita kwa kutokuwa na matatizo yoyote makubwa. Zaidi ya 50% ya matatizo ya tundu la saizi ndogo mpaka yale ya wastani yamezibwa kwa njia hiyo kuingiza katheta. Ujuzi mkubwa wa madaktari, uchaguzi sahihi wa wagonjwa, mipango sawia ndio ufunguo wa mafanikio katika njia hii ya kisasa.
Kuhusu Hospitali ya Apollo
Hospitali za Apollo ni za kwanza katika eneo Asia Pacific kutoa huduma za upasuaji kwa kutumia mfumo huu wa Robot, ambayo ni aina ya upasuaji isiyokuwa na madhara. Taasisi ya upasuaji kutumia Robot iliyopo hospitalini hapo wamejitoa kipekee katika kutoa huduma bora kwa wagonjwa. Taasisi ina wataalamu waliobobea kwenye mafunzo ya upasuaji, upendo katika utoaji wa huduma vifaa vya matibabu vya kisasa vinavyolenga kutoa uzoefu bora kwa mgonjwa. Vifaa hivyo ni pamoja na vifaa Robot ya Da Vinci inayotumika katika upasuaji.
Mfumo huu wa upasuaji hutumika katika teknolojia ya upasuaji wa magonjwa yanayohusiana na mfumo wa mkojo (Urology), magonjwa ya wanawake (Gynaecology), moyo, utumbo, na magonjwa ya watoto na matatizo ya uti wa mgongo