Quantcast
Channel: Mdimu's Blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1295

Baraza La Usalama La Umoja Wa Mataifa Lajadili Jaribio La Kombora La Korea Kaskazini

$
0
0
Tokeo la picha la Antonio Guterres

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limekutana kujadili jaribio la kombora la Korea Kaskazini la Jumapili iliyopita, kutokana na ombi la Marekani, Japan na Korea Kusini.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameilaani vikali Korea Kaskazini kwa kufanya jaribio hilo, akisema kuwa kitendo hicho kinakwenda kinyume na maazimio ya Baraza la usalama yanayopiga marufuku Korea Kaskazini kufanya majaribio ya makombora ya masafa marefu au silaha za kinyuklia.

Rais Donald Trump wa Marekani amesema atakabiliana vikali na Korea Kaskazini na kuitaja nchi hiyo kama "tatizo kubwa", lakini bado hajadokeza atachukua hatua gani.

Jana Korea Kaskazini ilitangaza kuwa imefanikiwa kufanya jaribio la kombora la masafa ya kati aina ya Pukguksong-2.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 1295

Trending Articles