Aliyekua Rais wa FC Barcelona Joan Laporta amaibwatukia bodi ya klabu hiyo kwa kitendo cha kuchukizwa na kibano cha mabao manne kwa sifuri, kilichotolewa na mabingwa wa soka nchini Ufaransa PSG usiku wa kuamkia jana.
Laporta amefikia hatua hiyo, kufuatia kitendo cha rais wa sasa wa FC Barcelona kushindwa kutoa kauli yoyote inayohusiana na tukio hilo ambalo anaamini limeidhalilisha Barca.
"Nimeshangazwa na jambo hilo, inawezekana vipi kwa kiongozi wa juu anashindwa kuzungumza lolote kuhusu aibu iliyotufika, jambo hili linatoa tafsiri tofauti na ilivyozoeleka miaka ya nyuma.
"Hii bodi ya viongozi imekua chanzo cha kuifikisha timu hapa ilipo, ni aibu kuona mambo haya yanatokeo na sikudhani kama kiongozi wa juu atashindwa kuwapoza hata mashabiki ambao waliandamana na timu yao hadi mjini Paris-Ufaransa.
"Ni hatari kwa Barça na aibu kwa kila mmoja wetu, hata tunapoangaliwa na wenzetu, ambao walituamini kutokana na soka letu tunacheza kwa ushindani mkubwa."
Laporta aliongeza: "Jambo hili limenikera na katu sitoweza kulisamehe."