Sudan Kusini na Uganda zimekubaliana kuunda tume ya pamoja ya kusimamia mpaka, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kupambana na kuenea kwa homa ya mafua ya ndege iliyoripotiwa Kampala mwezi Januari.
Waziri wa mifugo na uvuvi wa Sudan Kusini James Janka Duku amesema Sudan Kusini haitapiga marufuku uagizaji wa kuku kutoka Uganda, lakini nchi hizo mbili zitaweka wataalamu wa afya mpakani kusimamia na kukagua kuku kutoka Uganda wanaoingia Sudan Kusini.
Tangu homa ya mafua ya ndege iripotiwe nchini Uganda, Kenya na Rwanda zimepiga marufuku uagizaji wa kuku kutoka Uganda, na nchi kadhaa za Afrika Mashariki zimeimarisha usimamizi wa kuku kutoka Uganda.