Serikali ya Kenya imesema inahitaji dola milioni 114 za kimarekani kupambana na madhara ya ukame unaoikabili nchi hiyo, wakati idadi ya watu wenye upungufu wa chakula ikiongezeka kufikia milioni 3 katika mwezi Februari mwaka huu kutoka milioni 1.3 ya mwezi Agosti mwaka jana.
Msemaji wa Ikulu ya Kenya Manoah Esipisu amesema, nchi hiyo imepata dola milioni 73 za kimarekani, dola milioni 54 kati ya hizo zimetumika katika kipindi cha kwanza cha hatua za kukabiliana na ukame.
Bw. Esipisu amesema ili kukabiliana na hali hiyo, serikali imetenga dola milioni 73 za kimarekani, na bado kuna upungufu wa dola milioni 114.