Quantcast
Channel: Mdimu's Blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1295

Rais Wa Gambia Awaachia Huru Wafungwa 174

$
0
0
Tokeo la picha la Adama Barrow

Rais Adama Barrow wa Gambia amewaachia huru wafungwa 174 kutoka kwenye gereza la taifa lililoko katika kitongoji cha Banjul, mji mkuu wa nchi hiyo.

Hatua hiyo inachukuliwa kama ishara ya urafiki kutoka rais Barrow, ambaye aliapishwa jumamosi iliyopita kuwa rais wa tatu wa nchi hiyo, wakati wa maadhimisho ya miaka 52 ya uhuru wa nchi hiyo.

Maadhimisho ya siku ya uhuru na sherehe ya kuapishwa kwa rais zilishuhudiwa na viongozi wa nchi sita za Afrika na wajumbe kutoka nchi za nje ya bara la Afrika, ikiwemo China na Marekani.

Wafungwa hao wameachiwa chini ya wiki moja baada ya kuibuka kwa hasira za umma kuhusu video moja iliyoonesha hali ya magereza wakati waziri mpya wa mambo ya ndani alipotembelea magereza hayo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 1295

Trending Articles