Watu wasiopungua 30 wameuawa katika shambulizi la bomu lililotegwa kwenye gari lilitokea jana katika soko moja lenye watu wengi Mogadishu.
Idara ya usalama ya Somalia NISA imesema wahanga ni pamoja na askari na raia. Wpiganaji wa Al-Shabaab waliwalenga raia wasio na hatia wanaofanya biashara kwenye soko hiyo.
Mpaka sasa hakuna kundi lolote lililotangaza kuhusika na shambulizi hilo, ambalo ni kubwa zaidi kutokea tangu uchaguzi mkuu ufanyike tarehe 8 mwezi huu.
Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Michael Keating amelaani shambulizi hilo na kulitaja kama kumbukumbu ya kikatili ya mkakati wa magaidi unaorudisha nyuma maendeleo yaliyopatikana nchini humo.