Chansela wa Ujerumani Angela Merkel ameamua kuahirisha ziara yake nchini Algeria iliyopangwa kuanza Jumatatu wiki hii, kutokana na matatizo ya kiafya ya rais Abdulaziz Bouteflika wa Algeria.
Rais Bouteflika mwenye umri wa miaka 80 anapona baada ya kukumbwa na kiharusi mwezi Aprili mwaka 2013, ambacho kilitatiza mwendo wake na kuathiri shughuli zake za kikazi.
Rais Bouteflika aliingia madarakani mwaka 1999 na alichaguliwa tena mwezi Aprili mwaka 2014 kuwa rais wa Algeria kwa muhula wa nne wa kipindi cha miaka mitano.
Rais Abdulaziz Bouteflika wa Algeria