Quantcast
Channel: Mdimu's Blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1295

Kenya Yaandikisha Wapiga Kura Wapya Milioni 3.78

$
0
0
Tokeo la picha la Wafula Chebukati

Tume ya uchaguzi ya Kenya IEBC imetangaza kuwasajili wapiga kura wapya milioni 3.78 katika zoezi la usajili wa wapiga kura lililomalizika hivi karibuni.

Mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati amesema lengo la asilimia 62 limetimizwa tangu kipindi cha mwisho cha usajili wa wapigaji kura kianze katikati ya mwezi Januari.

Pia amesema, mpaka sasa tume hiyo imewasajili wapiga kura 135 wanaoishi Uganda, Tanzania, Rwanda, Burundi na Afrika Kusini.

Ameongeza kuwa usajili wa wapiga kura katika magereza utaanza leo katika magereza 118, unaowalenga wafungwa 5,952 na watuhumiwa 2,246 waliowekwa rumande.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 1295

Trending Articles