
Serikali ya Kenya na Ubalozi wa China nchini Kenya wamefanya hafla ya kuwaaga wanafunzi 55 wa kikundi cha pili wanaokuja China kuendelea na masomo.
Wanafunzi hao watasoma kozi ya reli kwa miaka minne katika chuo kikuu cha mawasiliano cha Beijing chini ya ufadhili wa kampuni ya reli ya China CRBC.
Waziri wa mawasiliano wa Kenya Bw. James Macharia, naibu waziri Irungu Nyakera, balozi wa China nchini Kenya Bw. Liu Xianfa na wazazi wa wanafunzi hao 35 wamehudhuria hafla hiyo.