
Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa FAO limetoa ripoti ikisema, mabadiliko ya hali ya hewa yamekuwa moja ya vikwazo katika kukidhi mahitaji ya chakula duniani, wakati idadi ya watu ikiendelea kuongezeka, na kutarajiwa kufikia watu bilioni 10 katikati ya karne hiyo.
Ripoti imesema mamilioni ya watu wanategemea kilimo na wanakabiliwa na ukosefu wa usalama wa chakula. Mabadiliko ya hali ya hewa yameleta athari kwa kila upande wa uzalishaji wa chakula.
Ripoti pia imesema kilimo ni moja na vyanzo vikuu vya hewa inayosababisha ongezeko la joto duniani, ikifuata uzalishaji wa nishati, na kueleza kuwa utoaji wa hewa hiyo kutokana shughuli za kilimo umeongezeka maradufu katika miaka 50 iliyopita.