Quantcast
Channel: Mdimu's Blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1295

Taarifa Kutoka JWTZ: Utapeli Ajira JWTZ

$
0
0

JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO

Simu ya Upepo  : “N G O M E”        Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo: DSM 22150463     Sanduku la Posta 9203,
Telex                   : 41051                       DAR ES SALAAM, 20  Februari, 2017.
Tele Fax              : 2153426
Barua pepe       : ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti                  : www.tpdf.mil.tz

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limeshitushwa na kusikitishwa na taarifa za kutapeliwa wananchi kuhusu ajira za JWTZ. 

Hivi karibuni kumezuka kundi la watu wanao jiita mawakala wa kutafuta vijana wa kujiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania na mara nyingi hutumia majina ya viongozi wa JWTZ kutapeli, huwataka wananchi hao kuwapa fedha ili kuweza kuwapatia nafasi hizo.

JWTZ linapenda kuwafahamisha wananchi kuwa nafasi za ajira Jeshini hutangazwa kwa kufuata taratibu za ajira ambapo JKT imepewa mamlaka ya kuwachukuwa vijana kutoka uraiani kwa kutoa matangazo ya wito wa vijana wa kujitolea ambapo matangazo hayo hutolewa hadi ngazi ya wilaya, vijana hao hutakiwa kuwa na  nyaraka mbali mbali zikiwemo za elimu, uraia na nyaraka nyingine kama hizo ili kukidhi vigezo  vya kupatiwa mafunzo ya kijeshi.

Baada ya kumaliza mafunzo hayo wahitimu hubaki JKT kwa muda wakisubiri vyombo vya ulinzi na usalama likiwemo JWTZ kutoa ajira kulingana na hitajio la vyombo hivyo. Wananchi wanatakiwa kufuata taratibu hizo ili kuepuka udanganyifu unaoweza kusababisha kutapeliwa fedha zao. Jeshi halitahusika na madai yoyote yatakayotokana na udanganyifu huo.

Imetolewa  na  Kurugenzi  ya  Habari  na  Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P  9203,   Dar es Salaam,  Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0756-716085


Viewing all articles
Browse latest Browse all 1295

Trending Articles