Mtafiti wa mambo ya kale wa Ujerumani na mwenzake waliotekwa nyara Jumatano wiki iliyopita na watu wenye silaha wasiojulikana katika kijiji cha Jenjela, jimbo la Kaduna kaskazini mwa Nigeria, wameachiwa huru.
Msemaji wa jimbo hilo Samuel Aruwan amewapongeza waokoaji kwa mafanikio ya operesheni ya uokoaji.
Mtafiti huyo amesema kikundi chake chenye watu wanne kutoka Chuo Kikuu cha Frankfurt cha Ujerumani kinashirikiana na tume ya Nigeria inayoshughulikia jumba la makumbusho na mabaki ya binadamu pamoja na mashirika mengine ili kufanya utafiti wa utamaduni wa Nok nchini Nigeria.
Wateka nyara waliwahi kuwasiliana na wenzake Profesa huyu na kudai pesa dola laki 1.8 za kimarekani ili kuwaachiwa huru.