Askari 7 wa kulinda amani wa China wameondoka Beijing kuelekea nchini Sudan Kusini ambapo watatekeleza majukumu yao kwa muda wa mwaka mmoja.
Wizara ya Usalama wa Umma ya China imesema, kikosi cha sita cha askari polisi wa kulinda amani wa China nchini Sudan Kusini kimechaguliwa na mamlaka ya polisi katika mkoa wa Zhejiang ulioko mashariki mwa China.
Askari hao wamepitia mafunzi ya ulinzi wa amani ikiwemo hali katika ukanda watakaotekeleza majukumu yao, huduma ya kwanza, lugha ya kiingereza, na mazoezi ya kulenga shabaha, pia wamefaulu mtihani wa Umoja wa Mataifa.