Quantcast
Channel: Mdimu's Blog
Viewing all 1295 articles
Browse latest View live

HIVI ULIGUNDUA? Akaunti ya twitter ya Rais Trump ilipotea kwa muda jana

$
0
0
Akaunti ya mtandao wa Twitter ya Rais Donald Trump  wa Marekani, ilipotea kwa muda jana lakini, ikarudishwa baadaye, kampuni ya twitter imekiri.
Twitter imesema kuwa akaunti hiyo kwa jina @realdonaldtrump iliondolewa na mfanyikazi mmoja na baadaye kuelezea kuwa ilikuwa siku yake ya mwisho kazi.
Akaunti hiyo iliondolewa kwa muda wa dakika 11 na sasa kampuni ya Twitter inachunguza.
Bwana Trump ambaye ni mtumizi wa mtandao wa Twitter wa mara kwa mara akiwa na wafuasi milioni 41.7 hajatoa tamko lolote kuhusu swala hilo.
Siku ya jana jioni, wale waliotembelea akaunti ya rais Trump waliona ujumbe uliosema ''pole ukurasa huu hauko kwa sasa!''
Baada ya akaunti kurejeshwa , ujumbe wa kwanza wa bwana Trump ulikuwa kuhusu ule mpango wa Republican wa kupunguza kodi.
Hatahivyo@POTUS ambayo ndio akaunti rasmi ya rais Trump haukuathiriwa.
Rais Donald Trump amekuwa mtumiaji mkubwa wa mtandao huo kwa kukuza sera zake mbali na kuwashambulia wapinzani wakeHaki miliki ya pichaTWITTER
Image captionRais Donald Trump amekuwa mtumiaji mkubwa wa mtandao huo kwa kukuza sera zake mbali na kuwashambulia wapinzani wake
Twitter imesema kuwa inachunguza tatizo hilo na kuchukua hatua za kuhakikisha kuwa kisa kama hicho hakitokei tena.
Kampuni hiyo ilisema katika ujumbe wake kwamba wamebaini katika uchunguzi wao kwamba kisa hicho kilifanywa na mfanyikazi anayewahudumia wateja ambaye alifanya hivyo katika siku yake ya mwisho ya kazi.
Bwana trump alijiunga na mtandao wa twitter mnamo mwezi Machi 2009.
Amekuwa mtumiaji mkubwa wa mtandao huo kwa kukuza sera zake mbali na kuwashambulia wapinzani wake wakati wa kampeni za urais 2016 na hata baada ya kuchukua mamlaka mnamo mwezi Januari.
- BBC Swahili

MARUFUKU: Wanawake kupiga ngoma Burundi

$
0
0
Serikali ya Burundi imepiga marufuku upigaji wa ngoma katika mikutano isiokuwa rasmi ikiwemo sherehe za kitamaduni na harusi katika jaribio la kuhifadhi mila hiyo ya zamani ambayo inajuliakana kimataifa.

Makundi yote yanayotaka kufanya tamasha za kitamaduni sasa yatalalizimika kujisajili na wizara ya Utamaduni na hayataruhusiwa kupiga ngoma kando na mikutano rasmi ya serikali bila ruhusa , agizo ambalo limetiwa saini na rais Pierre Nkurunziza.

Agizo hilo pia linapiga marufuku wanawake kupiga ngoma.

Hairuhusiwi kwa wanawake kupiga ngoma.

Hatahivyo wanaweza kushiriki katika kucheza densi za kitamaduni wakiandamana na ngoma hizo, kulingana na chombo cha habari cha AFP kilichonukuu agizo hilo.

Hilo ni jaribio la kusitisha na hatua mpya ya wanawake wa Burundi kupiga ngoma.

Kitamaduni wanawake hawakuruhusiwa kupiga ngoma nchini Burundi.

Ngoma inaonekana kama yenye umbo la mwanamke.

Agizo hilo pia linasema kuwa kundi lolote litakalotaka kupiga ngoma katika nchi za ugenini litalazimika kupata ruhusa kutoka kwa wizara.

Densi ya Burundi inatambulika na shirika la Umoja wa mataifa kuhusu Utamaduni Unesco kama urithi wa utamaduni isioonekana.

Mila hiyo inasemekana kuamsha roho za mababu na kufukuza pepo wabaya.


- BBC Swahili

Everton yatolewa Europa

$
0
0
Everton iliosalia na wachezaji 10 uwanjani walitolewa katika kombe la ligi ya Yuropa baada ya kushindwa na Lyon huku matumaini ya kocha David Unsworth ya kupewa kandarasi ya kudumu kama meneja yakipata pigo kubwa.

Kushindwa huko mbali na sare ya 1-1 kati ya klabu ya Atalanta na Apollon Limassol kunamaanisha kwamba The Toffees hawaezi kusonga mbele huku ikiwa imesalia mechi mbili.

Unsworth, ambaye alipandishwa daraja kutoka taasisi ya soka ya klabu hiyo kama kaimu mkufunzi baada ya kufutwa kwa Ronald Koeman sasa amepoteza mechi zote tatu allizosimamia.

Mchezaji wa zamani wa Chelsea Bertrand Traore alianza kufunga kunako dakika ya 68 baada ya kuwashinda kasi mabeki wa Everton na kumfunga kipa Jordan Pickford.

Bao lao la pili lilijiri dakika 14 baadaye kabla ya kukamilika kwa mechi hiyo baada ya mchezaji wa ziada Houssem Aouar kumwacha bila jibu kipa huyo wa Uingereza.

Lakini mambo yaliendelea kuwa mabaya zaidi kwa wageni hao wakati waliposalia wachezaji kumi baada ya Morgan Schneiderlin kupata kadi ya njano ya pili kwa kumchezea visivyo Maxwel Cornet.

Na huku ikiwa imesalia dakika mbili mchezaji wa Man United Memphis Depay alifunga bao la tatu na la mwisho kupitia kichwa akiwa maguu sita karibu na goli.



- BBC Swahili

Marekani yaanza mazoezi ya pamoja ya kijeshi kwenye Peninsula ya Korea.

$
0
0
Jeshi la anga la Marekani linaeleza kwamba limeanzisha mazowezi ya pamoja ya kijeshi kwa kutumia ndege mbili aina ya B-1B kutoka kambi ya jeshi ya Guam zikisindikizwa na ndege za kijeshi kutoka Korea Kusini na Japan Alhamisi kuelekea kwenye Peninsula ya Korea.

Shirika la habari la serikali la Korea Kaskazini-KCNA Ijumaa limekosoa vikali mazowezi hayo na kuyaeleza ni mazowezi yanayotazamiwa kufanya shambulizi la kushtukiza la nyuklia.

KCNA limeeleza kwamba ukweli unadhihirisha wazi wahuni kama mabeberu wa Marekani wanaharibu zaidi hali katika peninsula ya Korea na kutaka kuanzisha vita vya nyuklia.

Mazowezi hayo yanaanza siku moja kabla ya kuanza ziara ya siku 12 ya rais Donald Trump huko Japan, Korea Kusini, China, Vietnam na Ufilipino, huku jeshi la anga limeeleza safari ya ndege hizo haikuanza kwa sababu ya tukio lolote lile kwa hivi sasa.

- VOA Swahili


KUHUSU NDOA YA IRENE UWOYA: Dogo jana avunja ukimya

$
0
0
Abdulaziz Chende 'Dogo Janja' kutoka Ngarenaro, leo ametinga studio za Clouds FM Radio kupitia kipindi cha Leo tena akiambatana na `Mama yake' Khadija Shaaban ak.k.a Keisha kuwathibitishia watanzania kwamba ni kweli, ameoana na star wa BongoFlava Irene Uwoya amable kwa sasa amebadili dini na kuwa muislam, na sasa anaitwa Sheila.

Dogo Janja imem'bidi kufanya hiyo mchana huu kutokana na maneno yaliyozagaa mtaani kwamba si kweli kwamba wameoana na staa huyo bali ni video ya mwanadada Keisha ambayo Kiko njiani judoka, video ambayo Keisha ameiruka mita miamoja na kusema haipo.

Utata kuhusiana na video hiyo ulikuja baada ya Keisha kuweka picha ya harusi ya Dogo Janja mtandaoni na kueleza kuhusiana na kurudi kwake kwenye muziki hivi karibuni.

Kupitia Leo tena ya Clouds FM Dogo Janja ameuhakikishia umma wa watanzania kwamba amepata baraka zote kutoka kwa Mama cake, alipomwambia kuhusiana na kumuoya staa huyo wa filma na kwamba aliwahi kwenda naye mpaka kwao na mama yace alimfurahia sana.

Amesema wanaomsema kuhusiana na umri wa mkewe, hata stumme aliwahi kula mkt mkubwa, kwa hiyo sio sala geni duniani, kijana modo kuoa mtu aliyemzidi umri, kikubwa ni mapenzi na maridhiano.

Amekiri kwamba mpaka kuja kuamua kuoana, yeye na mkewe walidumu katika uhusiano kwa mwaka mzima, na kuna wakati ilibidi amkane kwenye vyombo vya habari ili kuweka usiri kwa usalama wa uhusiano tao na husuda za watu.

Dogo janja amekiri pia kwamba haikuwa rahisi kumpata mwanamama huyo, amepitia maguu mengi sana, mapa wakawa patoja, latino odio jambo alilolifurahia sana kwani mahusiano yake, ameyapambania.

Amesema ameba kwa kufuata taratibu zote za nodal, na ana nodal halali., 



NYARAKA ZIMETHIBITISHA: Iran ilisaidia al Qaida

$
0
0
CIA imechapisha nyaraka zilizopatikana katika operesheni ya kumkamata kiongozi wa al Qaida, Osama bin Laden, mwaka 2011. Nyaraka hizo zimeibua maswali kuhusu Iran kuunga mkono kundi hilo la kigaidi.

Maafisa wa kijasusi wa Marekani pamoja na waendesha mashtaka kwa muda mrefu wamekuwa wakisema kwamba Iran tangu mwaka 1991 imekuwa na uhusiano na kundi la al Qaida. Hiyo ni moja ya taarifa zilizopatikana katika ripoti ya kurasa 19 iliyoandikwa kwa lugha ya Kiarabu na ambayo ni sehemu ya nyaraka 47,000 zilizochapishwa na CIA.


Iran kwa upande wake daima imekuwa ikikanusha uhusiano wowote na al Qaida. Hata hivyo, ripoti iliyochapishwa na CIA inaonyesha namna ambavyo bin Laden, aliyekuwa mtu mwenye itikadi kali za Kisunni na aliyetokea Saudi Arabia, nchi ambayo ni hasimu mkuu wa Iran, aliweza kuvuka mgawanyo wa kidini na kutafuta mshirika kwa Wairan wa Kishia, kwa lengo la kumlenga adui yao wa pamoja ambaye ni Marekani.

Ripoti inaeleza Iran iko tayari kumsaidia mtu yeyote anayetaka kuipiga Marekani. Shirika la habari la Marekani, AP, lilipatiwa nakala ya ripoti na nyaraka nyingine zilizokamatwa na CIA. Miongoni mwa mambo mengine, zinajumuisha pia video za harusi ya mtoto wa bin Laden, Hamza. 

Video hizo hazijawahi kuonyeshwa hadharani na ni mara ya kwanza kwa Hamza kuonekana akiwa mtu mzima. kabla ya hapo, picha na video zilizokuwa zimesambaa zilimwonyesha akiwa bado mtoto. Inaaminika kuwa Hamza bin Laden anaandaliwa kuwa kiongozi mpya wa al Qaida.

Iran yakanusha madaiCIA awali iliweka nyaraka za al Qaida mtandaoni lakini baadaye ikaziondoa, ikisema pamekuwa na hitilafu za kiufundi. Nyaraka hizo zinaelezea kile kinachoaminiwa kuwa historia ya uhisiano baina ya al Qaida na Iran. 

Inaonyesha kwamba Iran ilijitolea kuipa al Qaida fedha, silaha na kingine chochote ambacho kundi hilo lingehitaji. Iran pia ilikuwa tayari kuwapa magaidi mafunzo katika kambi za kundi la Hezbollah nchini Lebanon. Al Qaida kwa upande wake ilitakiwa kushambulia mali na miundombinu ya Wamarekani nchini Saudi Arabia.

Taarifa hiyo inaendana na ripoti ya serikali ya Marekani iliyoandikwa na kamisheni ya kupeleleza mashambulio ya kigaidi ya World Trade Center na Pentagon mwaka 2001. Ripoti hiyo inasema maafisa wa Iran walikutana na viongozi wa al Qaida nchini Sudan mwaka 1991 ama 1992. 
Kamisheni hiyo ileleza pia kuwa wanamgambo wa al Qaida baadaye pia walipatiwa mafunzo Lebanonon kutoka kwa kundi la wanamgambo wa Kishia, Hezbollah. Mpaka leo hii, Iran inaiunga mkono Hezbollah.

Hata hivyo, shirika la habari la Iran lisilo rasmi, Fars, leo limekanusha madai yote ya CIA, likisema huo ni mpango dhidi ya serikali ya Iran.

Mwandishi. Elizabeth Shoo wa AP

Mohammed Dewji apongeza jitihada za Rais Magufuli kufufua viwanda

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mohammed Enterprises (MeTL Group), Mohammed Dewji (Pichani juu) amepongeza uamuzi wa Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda kwa kufufua viwanda ambavyo vilikuwa havifanyi kazi.
Dewji ametoa pongezi hizo wakati akizungumza katika mkutano wa siku mbili wa Global Business Forum 2017 (GBF) kuhusu Viwanda kwa Nchi za Afrika uliofanyika Dubai, Falme za Kiarabu (UAE).
Mfanyabiashara huyo ambaye anamiliki viwanda 41 alisema uamuzi aliochukua Rais Magufuli ni mzuri hasa katika kipindi hiki ambacho Tanzania inaelekea katika uchumi wa kati.

Dewji alisema kampuni yake ya MeTL Group itaendelea kushirikiana na serikali na katika kipindi cha miaka kadhaa ijayo amejipanga kuhakikisha anatoa ajira kwa Watanzania 100,000 jambo ambalo litasaidia kukuza uchumi wa nchi na kwa wananchi..
 “Nianze kwa kumpongeza Mhe. Rais John Pombe Magufuli kwa shabaha yake ya viwanda, ni nzuri sababu kuna ongezeko la thamani lakini pia watu wanaweza kupata ajira na pia hizi biashara zitalipa kodi ambazo zitaisaidia serikali kuwekeza kwenye mambo ya afya na maji na huduma za jamii. Mimi shabaha yangu kwenye miaka saba au nane ijayo MeTL Group tunataka tuajiri watu 100,000,” alisema Dewji.
Dewji ambaye kwa mujibu wa jarida la Forbes ni tajiri namba moja nchini aliongeza kuwa utendaji wa Rais Magufuli ni wa kasi hivyo anategemea kuwa katika kipindi cha miaka michache ijayo uchumi wa Tanzania utakuwa umekuwa  sana.
“Mimi naona kwa kasi ya Mhe. Rais kwenye miaka miwili au mitatu ijayo tutakuwa tumefika mbali sana, uchumi wetu kwasasa ni asilimia sita au saba lakini kama tukitaka kuondoa umaskini lazima nchi yetu ukuaji wa uchumi uanze kukua kwa zaidi ya asimilia 10, mimi nina muamini sana Mhe. Rais na shabaha yake kwahiyo Mungu atutangulie na sisi tupo nyuma yake tutafika hivi karibuni,” alisema Dewji.
Pia Dewji alizungumzia umuhimu wa mkutano wa GBF ambao umekutanisha watu kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika wakiwepo viongozi wa serikali za nchi za Afrika na wawekezaji alisema ni nafasi ya kipekee kwani pamoja na kujadili viwanda pia amepata nafasi ya kuwaelezea washiriki wa mkutano fursa za uwekezaji zilizopo hapa nchini.
“Umuhimu ni mkubwa sana nakuja hapa kama MO lakini pia nawakilisha nchi yangu Tanzania, nimeitangaza nchi yangu ili watu waje na wawekeze, nimewaeleza mazingira yetu ya uwekezaji ni mazuri, tuna malighafi na tunahitaji viwanda angalau watu wetu wa Tanzania wapate ajira na serikali ipate kodi,” aliongeza Dewji.
CAPTION: Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji akizungumza katika mkutano wa Global Business Forum 2017 kuhusu Viwanda kwa Nchi za Afrika, mkutano huo wa siku mbili umefanyika Dubai, UAE na kuhudhuriwa na watu 5860 wakiwepo viongozi wa serikali za nchi za Afrika na wafanyabiashara. (Picha na Clouds Media)

PICHA ZA RAIS MAGUFULI: Mapumzikoni Chato

$
0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia picha kwenye simu pamoja na Mama yake mzazi Suzana Magufuli (katikati) pamoja na mdogo wake Asteria wa kwanza (kushoto). Rais Dkt. Magufuli yupo mapumzikoni katika Kijiji cha Lubambangwe Chato Mkoani Geita.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia picha kwenye simu aliyokuwa akioneshwa na Mama yake mzazi Mama Suzana Magufuli nyumbani kwao katika kijiji cha Lubambangwe Chato mkoani Geita.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza radio pamoja na Mama yake mzazi Suzana Magufuli wa pili kutoka (kushoto) mdogo wake Asteria wa kwanza (kushoto), na Dada yake Monica Joseph wa kwanza (kulia). Rais Dkt. Magufuli yupo mapumzikoni katika Kijiji cha Lubambangwe Chato Mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza radio pamoja na Mama yake mzazi Suzana Magufuli wa pili kutoka (kushoto) mdogo wake Asteria wa kwanza kushoto. Rais Dkt. Magufuli yupo mapumzikoni katika Kijiji cha Lubambangwe Chato Mkoani Geita. PICHA NA IKULU


Nguvu zaidi yahitajika kuwekeza katka kuokoa vifo vya akinamama

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania  Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, leo ameshiriki katika Matembezi ya Hisani ya Kilomita Nne na Nusu yenye lengo la kukusanya fedha zitakazosaidia kugharamia mafunzo ya uuguzi na ukunga. 

Akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza katika viwanja vya Green Ground- Oysterbay mara baada ya matembezi hayo, Makamu wa Rais alisema takwimu za vifo vya kina mama zimeongezeka, hivyo wazo lakusaida kuongeza idadi ya wakunga ambao watasaidia kupunguza vifo hivyo ni zuri sana. 

Makamu wa Rais alisema “nimefarijika kusikia kuwa mwaka 2016 matembezi haya ya hisani yalikusanya wastani wa shilingi milioni 290 pesa ambayo iliwekwa ​asilimia 75 katika mafunzo ya ngazi ya cheti” . Makamu wa Rais alionesha kufurahishwa na malengo yaliyowekwa kwa miaka miwili ijayo ya kukusanya kiasi cha shilingi milioni 300 kwa ajili ya kusomesha wakunga wauguzi 400 katika ngazi ya cheti na diploma kwas njia ya masafa.

Makamu wa Rais alisisitiza kuwa moja ya chanzo cha vifo vya kina mama na watoto wakati wa kujifungua ni ukosefu wa wataalam wa kuwahudumia. Takwimu za Tanzania zinaonesha kuwa zaidi ya asilimia 60 ya akina mama hawaendi kujifungua katika vituo vyetu vya kutolea huduma kutokana na kukosekana kwa wataalam wa kuwahudumia akina mama hao.

Makamu wa Rais aliwahakikishia wadau wote wa sekta ya afya kwamba serikali ipo nao bega kwa bega katika kuhakikisha wanaotaka kuwekeza katika sekta hii wanafanikisha malengo yao. Aidha, alisema serikali inaendeleza juhudi za kuinua uchumi kwa kuongeza idadi ya viwanda ikiwa ni pamoja na viwanda vya kutengeneza dawa na vifaa tiba ili kuongeza upatikanaji na uboreshaji wa huduma muhimu za afya kwa binadamu. 

Makamu wa Rais aliiagiza Wizara ya afya iusimamie kikamilifu mwongozo unaotaka kila kifo cha mama na mtoto kinachotokana na matatizo ya uzazi kijadiliwe ndani ya saa 24 katika kituo au hospitali husika kwa lengo la kubaini chimbuko la kifo hicho na kuchukua hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kuboresha zaidi huduma zinazotolewa katika kituo husika.  
Mwisho,Makamu wa Rais aliwashukuru wadau ,wahisani na wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye matembezi hayo na kuwaomba kuendelea kushiriki na kuchangia fedha kwa ajili ya kusomesha wakunga wauguzi.

PICHANI JUU: Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Ssuluhu Hassan leo ameongoza matembezi ya hisani kwa ajili ya kusomesha Wauguzi Wakunga , matembezi hayo ya kilometa 4.5 yalianzia kwenye viwanja  vya Green Grounds, Oysterbay jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Waziri mkuu wa Lebanon ajiuzulu akihofia maisha yake

$
0
0
Waziri mkuu wa Lebanon Saad al-Hariri ametangaza kujiuzulu katika hatua ya kushangaza akisema kuwa anahofia maisha yake.

Katika mkutano na vyombo vya habari katika mji mkuu wa Saudia Riyadh, bwana Hariri alilikosoa kundi la madhehebu ya Shia Hezbollah na Iran akisema kuwa hakuna eneo ambalo Iran itaelekea bila kupanda hofu na uharibifu .

Amesema kuwa hali ya sasa nchini Lebanon ni sawa na ilivyokuwa wakati babake Rafiq alipouawa 2005 na kwamba alikuwa anahisi kuna njama ya kumuangamiza.

Waandishi wanasema kuwa ni muhimu kwamba bwana Hariri hakuwa akizungumza kutoka Beirut bali kutoka Saudia ambayo ni mkosoaji mkubwa wa Iran.

- BBC Swahili

Wanaharakati wa kulinda mazingira waandamana Bonn

$
0
0
Klimakonferenz Bonn Demonstrationen gegen Kohle (Getty Images/S. Gallup)
Maelfu ya waandamaanji walikusanyika mjini Bonn Jumamosi kabla ya kuanza kwa mkutano wa kimataifa unaoandaliwa na Umoja wa Mataifa wa kujadili mabadiliko ya tabia nchi mjini humo.


Mkutano huo wa mazingira unaanza Jumatatu Novemba 6, na utadumu kwa wiki mbili zijazo hadi Novemba 17. Kiasi ya watu 25,000 wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo wa kimataifa.
Suala la kuachana na uzalishaji wa makaa ya mawe Ujerumani ni moja wapo ya vipengele muhimu vinavyojadiliwa katika mazungumzo ya kuunda serikali ya muungano kati ya Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na vyama vengine vya kisiasa , Chama cha walinda mazingira cha  Kijani na chama kinachoelemea upande wa biashara cha Free Democrats.
Waaandaji wa maandamano hayo wapatao 20,000 wameitolea wito serikali ya Ujerumani kutekeleza makubaliano ya mwaka 2015 yaliyofikiwa mjini Paris yenye lengo la kuhakikisha katika karne hii, uchumi wa dunia hautegemei mafuta na inachukua hatua kupunguza ongezeko la viwango vya joto duniani.
Ujerumani huenda isifikie malengo
Data za hivi karibuni zinaonesha kuwa Ujerumani itashindwa kufikia lengo lake la kupunguza kwa asilimia 40 kiwango cha gesi chafu ya Carbon Monoxide ifikapo mwaka 2020. Miongoni mwa waliondamana ni wanachama wa mrengo wa kushoto, vyama vya kisiasa vinavyolinda mazingira, vyama vya wafanyakazi na makundi yanayoipinga utandawazi.
Klimakonferenz Bonn Demonstrationen gegen Kohle (Getty Images/AFP/S. Gallup)
Utekelezaji wa mkataba huo utajadiliwa katika mkutano huo wa Umoja wa Mataifa unaofanyika mjini Bonn, utakaowaleta pamoja wajumbe wa nchi 196 wanachama wa umoja huo. Makubaliano ya Paris yaliyofikiwa 2016 yanalenga kupunguza viwango vya joto duniani hadi chini ya nyuzi mbili.
Taarifa kutoka makundi 100 ya kiraia imesema maisha ya mamilioni ya watu duniani yako hatarini kutokana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa na kuwa kuna baadhi ya visiwa huenda vikapotea kabisa kutokana na kuongezeka kwa viwango vya maji ya bahari.
Mkataba wa Paris utafikiwa?
Mashirika hayo yanataka hatua za dharura kuchukuliwa kuepusha hatari hizo ikiwemo kuanza kupunguzwa kwa kiwango cha nishati itokanayo na mafuta na pamoja na makaa ya mawe. Makaa hayo ya mawe yanachangia kwa karibu thuluthi moja ya matumuzi ya nishati duniani na inachangia asilimia 40 ya umeme unaozalishwa, hiyo ikiwa mara mbili ya ile ya gesi asilia.
Ikilinganishwa na gesi na mafuta, makaa ya mawe yanachafua mazingira zaidi. Nchini Marekani utumiaji ya makaa hayo umepungua ambako sasa matumizi ya gesi ya asilia yanashika kasi, japo sio kwa kiwango cha kuridhisha.
Mkutano huo muhimu wa kujadili mabadiliko ya tabia nchi unafanyika wakati ambapo Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza nchi yake inajiondoa kutoka mkataba uliofikiwa mwaka jana mjini Paris, Ufaransa, wa makubaliano ya kihistoria ya tabia nchi na hivyo kuibua mashaka na wasiwasi kuwa huenda hatua hiyo iliyochukuliwa na Marekani, taifa lenye nguvu duniani ikahujumu kufikiwa kwa malengo ya makubaliano hayo.
Mwandishi: Caro Robi/Afp/Reuters/dpa

Serena arudi mazoezini, yu tayari kwa ndoa

$
0
0
Baada ya likizo ya uzazi, mkali wa Tennis amerudi mazoezini kurudisha umbo lake la kimichezo huku akidaiwa kujiandaa naharusi yake anayotarajiwa kuifunga na mzazi mwenzie Alexis Ohanian. mapema mwezi Desemba mwaka huu.

Jana asubuhi, Serena amepost picha katika mtandão wa Instagram akiwa na mwanamuziki Ciara Katia chumba mala cha mazoezi.

Chanzo cha kuaminika kimeuambia mtandao wa ET kwamba Serena na Ohanian wanatarajia kufunga ndoa mwezi huu ambapo mpaka sasa hivi, kaadi za mialiko zimeshaisha na wageni wengi mashuhuri wamealikwa.

Wapendanao has walivishana Pete za uchumba mwezi Desemba mwaka jana na mwezi Septemba mwaka huu wakapata mtoto wao wa kwanza wa like ajulikanaye kwa jina la Olympia


MATA: Chelsea sio wa kuwachukulia poa

$
0
0
Juan Mata ameutaja mchezo wao dhidi ya Chelsea si wa kuuchukulia rahisi bali ni mchezo wa kuuangalia kwa umakini unaotakiwa kutumia akii nyingi.

Katika mchezo wa Leo, United watatakiwa kuutafuta ushindi wao wa one mfululizo wakati wa mchezo huu ambapo kila timu inaonekana kuwa na kazi ngumu ya kutowaangusha  wao wanaotambiana kila kona lakini pia kujiimarisha katika chati za mpira.

Ukiiangalia wiki mii inayoisha kwa umakini, ilikuwa wiki nzuri kwa kocha Jose Mourinho na mashabiki wake, Jumanne aliwapiga Benfica 2-0, ushindi uliokuja bade ya like gold la Anthony Martial dhidi ya Tottenham kule Old Trafford.


Sasa akiongelea hilo, Mata ndio akakubali kwamba ndio, ilikuwa wiki nzuri lakini hawa Chelsea Sio wa `kuwachukulia poa’. 

FIESTA DODOMA: Ben Pol kama kawa

$
0
0


Wabunge wa bunge la Tanzania wakicheza pamoja na msanii Ben Pol(mwenye shati nyeupe) kwenye Tamasha kubwa la Tigo Fiesta lililofanyika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma usiku wa kuamkia jana.

Msanii Ben Pol akipongezwa na Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Antony Mavunde kwenye jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika usiku wa kuamkia jana uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Msanii Mimi Mars mdogo wa Vanessa Mdee akifanya yake kwenye Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika usiku wa kuamkia jana uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Msanii Vanessa Mdee akitoa burudani kwenye Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika usiku wa kuamkia jana, uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Darassa akitoa burudani kwa maelfu ya wakazi wa Dodoma mapema usiku wa ijumaa

JUX akitoa burudani kwenye Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika usiku wa kuamkia jana, uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Msanii mkongwe Alli Kiba akiwapa burudani mashabiki wake waliofurika kwenye Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika usiku wa kuamkia jana uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.




TAARIFA: Za Dodoma Marathon ziko hapa

$
0
0
Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali, Tigo Tanzania wakiungana na Vision Sports wametangaza kuanza kwa usajili wa washiriki katika mbio za Dodoma Marathon. Mji wa Dodoma utageuzwa kuwa kitivo cha mazoezi na furaha kwa familia nzima tarehe 12 Novemba wakati shindano hilo litakapohitimishwa. 

Usajili kwa Dar es Salaam unafanyika katika vituo maalum vya Duka la Tigo Shop lililopo Mlimani City, Duka la Simply Elegant lililopo Dar Free Market, Ghorofa ya Chini ya Kibo Complex eneo la Tegeta na Duka la Imalaseko SuperMarket lilipo eneo la Posta katikati ya jiji. Kwa Dodoma, usajili unafanyika katika eneo la Dodoma Hotel, Carnival, Cape Town Complex iliyopo Kisasa na Duka la Tigo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
‘Wale watakaojisajili kwa njia ya Tigo Pesa watapata punguzo la bei la asilimia 10%. Wanaweza kufanya hivyo kwa kutuma kiasi cha shilingi 13,500/- kutoka kwenye simu zao za mkononi kwenda namba ya Tigo Pesa 0674 444 444. Hapo hapo watapokea ujumbe utakaowataarifu kujisajili na eneo ambalo wanafaa kwenda kuchukua vielelezo vyao vya usajili,’ Meneja wa Tigo, Kanda ya Kaskazini, Henry Kinabo alisema. 

Kwa upande wake,Meneja wa maendeleo wa Vision Sports, Raymondwenye tovuti ya Dodoma Marathon na katika vituo vya usajili. ‘Pia ni muhimu kwa washiriki kuhudhuria kikao cha maelezo kuhusu ushiriki na usalama wa washiriki kitakachofanyika kabla ya mbio kuanza saa kumi na mbili asubuhi, pale katika Uwanja wa Jamhuri, mjini Dodoma. 

Tigo inadhamini mbio za kilometa 21 za Tigo Dodoma Half Marathon. Dodoma Marathon pia itahusisha mbio ndefu za kilometa 42, mashindano ya kilometa 10 pamoja na yale ya kilometa 5 yatakayohusu wanafamilia na jamii yote kwa ujumla. Zawadi murwa zitatolewa kwa washiriki ikiwemo vyeti vya ushiriki, medali na zawadi za fedha kwa washindi wa mbio zote. Wanariadha mashuhuri kutoka ndani na nje ya nchi wanatarajiwa kushiriki katika mbio hizo. 

“Tuna furaha kubwa kudhamini shindano hili ambalo linahamasisha watu kuzingatia afya bora kwa kushiriki katika michezo, na pia kuinua vipaji katika michezo,” Henry Kinabo, Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini alisema. 

PICHANI JUU: Kaimu Mkurugenzi wa Tigo kanda ya kaskazini, Henry Kinabo(kulia) akizungumza na waandishi wa habari jana namna ya kujisajili mbio za Dodoma Marathon zitakazotimua vumbi jumapili ya tarehe 12 mwezi huu, ambapo utaweza kujisajili kwa Tigopesa kwa namba 0674 444 444 kwa punguzo la asilimia 10%. Pembeni ni Meneja wa Maendeleo wa Vision Sports, Raymond Mchani.


NIMEJIPANGA: ..ajigamba Fiesta Super Nyota kutoka Moro

$
0
0


MSHINDI wa shindano la kuibua vipaji la Tigo Fiesta Supa Nyota, mkoa wa Morogoro,  Salum Munga, ametamba kuibuka na ushindi katika fainali za mwaka huu. 

Kinda huyo jana aliibuka kidedea baada ya kuwapiku washiriki 106 chipukuzi waliojitojeza kuwania nafasi hiyo. 

Washindi wa mashindano ya Tigo Supa Nyota kutoka mikoa 15 ya Tanzania watashindana kwenye fainali itakayofanyika Dar es Salaam mwezi huu ili kupata mshindi wa jumla. Mshindi wa Tigo Supa Nyota, atapata nafasi ya kuendelezwa kimuziki ikiwa ni pamoja na kuingia studio.


Mara baada ya kushinda,  Munga. alisema,  amepata nafasi,  atahakikisha anaifanyia kazi vyema na kuwapa furaha mashabiki wake wa mkoa wa Morogoro. Alisema anejipanga vyema kuhakikisha analeta taji la Tigo Fiesta Supa Nyota kwa mara ya kwanza na kuweka historia.

Alisema anatambua kuwa ataenda kupambana na wasanii kutoka mikoa mbalimbali lakini atahakikisha anafanya vizuri na kutengeneza historia mpya.
Meneja wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo,  Kanda ya kati,  John Tungaraza,  alisema kuwa lengo lao ni kuhakikisha wanaibua vipaji na kuwapatia daraja wasanii chipukizi kupata nafasi ya kufikia malengo.

"Tutahakikisha vijana wanafikia malengo kwani Tigo kwa udhamini wetu tunaibua wasanii chipukizi ili kuwaendeleza na kufikia malengo,  kwani hatutawapa nafasi wasanii wa nje", alisema. 

PICHANI JUU: Mshindi wa Tigo Fiesta Supa Nyota toka mkoa Morogoro, Salum Munga akiimba kwenye kinyang'anyiro cha kumpata mwakilishi wa mkoa Morogoro

Majaji wakiendelea na majukumu yao
Mchujo wa washiriki
Mshindi wa Tigo Fiesta Supa Nyota toka mkoa Morogoro, Salum Munga akipongezwa na washiriki wenzake.

Tarehe mpya ya uchaguzi wa urais yatangazwa DR Congo

$
0
0
Tume ya uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza kwamba uchaguzi mkuu nchini humo sasa utafanyika Desemba 2018.

Hatua hiyo hata hivyo haijaufurahisha upinzani ambao unataka Rais Joseph Kabila aondoke madarakani.

Uchaguzi ulipangiwa kufanyika mwaka huu chini ya makubaliano yaliyoafikiwa mwaka jana, lakini tume ya uchaguzi imechelewa kuandaa uchaguzi.

Awali, ilikuwa imetangaza kwamba uchaguzi unaweza tu kufanyika mwaka 2019.

Lakini sasa tume hiyo imetangaza kwamba uchaguzi wa rais, wabunge na viongozi wa serikali za majimbo utafanyika mnamo 23 Desemba, 2018.Lakini upinzani umepinga tarehe hiyo na kusema haikubaliki.

Upinzani umesisitiza kwamba ni sharti Rais Kabila(Pichani juu) aonondoke madarakani kufikia mwisho wa mwaka huu.

"Tunaikataa kalenda iliyotolewa ya uchaguzi...tunachokitaka kwa sasa hivi ni Kabila kuondoka madarakani kufikia 31 Desemba, 2017," alisema Augustin Kabuya, msemaji wa chama kikuu cha upinzani cha Union for Democracy and Social Progress (UDPS).

Afisa wa tume ya uchaguzi Jean-Pierre Kalamba amesema matokeo ya muda yatatangazwa katika kipindi cha wiki moja baada ya upigaji kura kufanyika, mnamo tarehe 30 Desemba, lakini matokeo kamili yatatangazwa tarehe 9 januari, 2019.

Rais mpya anatarajiwa kuapishwa 12 Januari, 2019.Haki miliki yKiongozi wa upinzani Moise Katumbi amepuuzilia mbali mpango huo wa uchaguzi.

"Utawala huu dhalimu unataka kuendeleza ukosefu wa uthabiti na dhiki dhidi ya wananchi," Katumbi amesema.

"Hatutakubali kalenda hii. Kabila sharti aondoke," aliandika kwenye Twitter.

Hali ya wasiwasi imekuwepo nchini humo tangu Kabila alipokosa kuondoka madarakani mwishoni mwa mwaka jana baada ya kumalizika kwa muhula wake wa pili na wa mwisho.

Tume ya uchaguzi ilikuwa imesema haiwezekani kuandaa uchaguzi kwa wakati kutokana na matatizo ya kuandaa sajili ya wapiga kura, hasa eneo lenye misukosuko la Kasai katikati mwa nchi hiyo.

Tangazo la Jumapili limetolewa siku kumi baada ya ziara ya balzoi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa

Nikki Haley ambaye aliitaka DR Congo kufanya uchaguzi mwaka ujao.

Uingereza, Ufaransa, Muungano wa Ulaya na Umoja wa Mataifa ni miongoni mwa wale ambao walitaka tarehe mpya ya uchaguzi itangazwe.


- BBC Swahili

Conte hajui hatima ya David Luiz Chelsea

$
0
0

Meneja wa Chelsea Antonio Conte amesema hafahamu iwapo beki David Luiz atasalia Stamford Bridge.

Mchezaji huyo wa miaka 30 hakujumuishwa kwenye kikosi cha Chelsea dhidi ya Manchester United Jumapili na hata hakuwekwa kwenye benchi.

Badala yake, meneja huyo alimchezesha Andreas Christensen.

Alipoulizwa kumhusu Luiz, Conte alisema: "Lazima atie bidii la sivyo atakuwa kwenye benchi au kwenye viti vya mashabiki."Kuhusu mustakabali wa Luiz, Conte aliongeza: "Sijui, Christensen ndiye sasa na siku za usoni kwa Chelsea."

Mbrazil Luiz amecheza dakika 90 katika kila mechi za Chelsea tatu walizokuwa wamecheza karibuni Ligi ya Premia na alicheza walipolazwa 3-0 na Roma Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya katikati ya wiki.David Luiz alikaa nyuma ya benchi wakati wa mechi dhidi ya Manchester United

Lakini Jumapili, aliketi nyuma ya benchi ya Chelsea, akiwa amejifunga skafu ya rangi nyeusi kichwani.

Alirejea mara ya pili Chelsea kwa £34m kutoka Paris St-Germain Agostit 2016 na alikuwa kwenye kikosi kilichoshinda ligi msimu uliopita.
- BBC Swahili

PICHA ZA RAIS MAGUFULI: Ziarani Kagera

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Muleba wakati akiwa njiani kuelekea Bukoba mjini.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasikiliza wananchi wa Muleba wakati walipokuwa wakiwasilisha kero zao mbalimbali.
 Baadhi ya wananchi wa Kemondo mkoani Kagera wakiwa juu ya miti kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati akihutubia wananchi wa eneo hilo.
 Wananchi wa Kemondo wakifurahia wakati  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia.
 Wananchi wa Muleba wakifurahia wakati  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia.
 Muleba...
Rais akisalimiana na uongozi wa mkoa 
Na haps ni Biharamulo
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwananchi Maarufu wa Muleba Hassan Milanga mara baada ya kuwasalimia wananchi wa Muleba.
Baadhi ya mabango wa Wananchi wa Kemondo mkoani Kagera wakiyanyanyua wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akipita katika eneo hilo. 

ZEE LA NYETI: Blaza acha michosho, miyeyusho ina mwisho

$
0
0
Wanangu niaje?

Nimekula misaim ya kutosha judoka kwa sana kitaani wananimaindi nimechelewesha kupandisha Zee la wiki hii hewani, hivi wanangu si nilisema Jumatatu? Kwani niliwaambia na taimu? Sasa mbona mnaanza kukoroma bado mapema? Au ndio Kiu ya ishu za tauni? Msikonde basi nishamalizana nayo hii hapa ishu ya wiki hii inadondoka kama kawa.

Ujue bwana, tauni miyeyusho sana samtaimz, na ndio maana last wiki nikawa nawaambia madogo kama vipi vileji kunawahusu, hizi laifu za kufosi hizi, kuna watu zinawakosti sana, ingawa wenyewe wanaona kama poa hivi, ila sio poa wala nini, miyeyusho tu mwanangu mwenyewe.

Sasa kund yanki flani vivi saundi sana hapa tauni, mwenyewe huwa akiniona ananichukulia poa sana kumbe mtu mzima na mimi miyeyusho kitambo sana, ila kwa sababu nshakuwa zee kweli, nimeamua kukausha na kudili na ishu zilizonyooka. Haya mambo ya saundi nimeamua kuwaachia magumashi junia.

Umeona bwana?

Sasa Jamal juzikati kanijia na mchongo wake wa madini, unaona bwana? Unajua ananipa zipi? Kuna chili wake autoka Naijeria alikuja kumtembelea, akagundua kwamba shambani kwa mshua wake Kuna ishu, lakini wanatafuta mtu mwenye jina tauni ili wakachukue mkopo samwea waanze kutemesha mzigo.

Umeskia mwanangu?

Nikamuuliza mean, h\ishu yenyewe Kiko mkoa gani? Mwana bila noma wala nini akanichana kwamba ishu Dar hii hii ila Mkuranga flani hivi mshua wake anapiga ishu za matikiti. Sasa huyo mana latina misele yace amaina dizaini flani za mchanga ambo sio wa kawaida.

…machale yakanidensi….
Madini Mkuranga? Waeniona boya kiasi gani Hawa mayanki, ila nikajifanya kama Boya kweli, na mimi nikamtuliza, nikamwambia mwanangu sio ishu, ila sasa inabidi wataalam wazuke pale shamba wakapige risechi mbili tatu ili hata huko samwea tukienda kuchukua mkopo, tupeleke dokumenti zinazowapa uhakika washua kwamba mzigo upo.

Umenisoma babu?

Nikamwambia na gharama za ndani, yaani za risechi na nini inabidi mimi mwenye jina kwa sababu ndio nitakayezama kitaa kwenda kutafuta mkopo nipewe ili nikalete watu wa uhakika, niwalipe ili Kazi ianze. Umeona mwanangu mwenyewe? Hapo nikawa nishamgeuzia kibao kama alitaka anitemeshe mzigo ikawa inabidi auteme yeye sasa.

Mwana akanichekiiii, na mimi nikawa nimemkazia uso, uso wa Kazi ile ile nikamwambia ndio hivyo, mie nina wanangu akina Le Mutuz wana  koneksheni tauni lakini wanataka vitu vilivyonyooka ili na way wanyooshe dili kama kweli zipo.

Akajikata, huku nyuma sasa ndio nikabaki na maswali, huyu mchizi mimi kanichukuliaje? Madini Mkuranga? Hivi kuna watu mpaka leo mnafkiri tauni kuna washamba? Sawa wanaweza kuwepo, ndio mimi sasa Zee mwenyewe?

Ndio maana mnasema maisha magumu kudadadeki kumbe mpaka fiksi zimewaishia, na huu ndio mwisho wa miyeyusho kudadadeki, ukiona aidia za manage zinakuishia ujue mwanangu unatakiwa kuachana nazo na kurudi kwenye ishu za kunyoosha.

Sasa bora umekutana na Zee, anakubananisha na ishu, mwingine anakupa mkwanja ila ukimletea miyeyusho anakurudisha kijijini kwa kichapo, unafilisiwa kwanza, unakula kichapo, jela miaka kadhaa halafu vileji.

Kipi bora?

Jiangalie plaza


Viewing all 1295 articles
Browse latest View live