Quantcast
Channel: Mdimu's Blog
Viewing all 1295 articles
Browse latest View live

AMINA MOLLEL: Wazazi msiwafiche watoto wenye ulemavu

$
0
0



Wazazi hususa ni jamii ya kimasai wametakiwa kuachana na zana ya kuwatenga na kutowapeleka shule watoto wa kike na wale ambao ni walemavu badala yake wawapeleke mashuleni kwani wao ndio viongozi wa baadae

Hayo yamebainishwa na mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Amina Mollel wakati alipokuwa akizungumza kama mgeni rasmi katika sherehe za kupandisha ngazi rika kutoka katika rika la kurianga kuingia katika rika la Nyangulo, sherehe ambazo zilifanyika katika Kijiji cha Oldenderet Kata ya Nduruma mkoani Arusha

Alisema kuwa kunabaadhi ya wazazi wamekuwa wakiwaficha watoto wao kisa ni walemavu jambo ambalo linawakosesha haki zao ikiwemo ya kupata elimu kutokana na kufichwa huko.

“Kwa kweli wazazi wanavyoficha watoto wao hususan walemavu wanawanyima haki yao mfano kama mimi ningefichwa leo kweli ndugu zangu ningeweza kuwa kiongozi hivyo napenda kuwasihi wazazi wasiwafiche watoto hawa kwani wakiwapeleka shule kupata elimu itakuwa vizuri kwani pale watakapomaliza shule wanakuja kuwasaidia “alisema Amina

Aidha pia aliwataka wazazi hawa wa jamii ya kimasai na hata wale wa makabila mengine kuacha kuwaozesha watoto wakike mapema kwani watoto hao wakike nao wana haki ya kupata elimu kwani elimu ni bure, kuanzia ngazi ya msingi hadi sekondari hivyo ni vyema kama wazazi wakawasimamia watoto hususa ni wa kike wakaenda shule

Aliongeza kwa kuwasihihi watoto wa kike kuweka kipaumbele swala la elimu kwani elimu ndio kila kitu katika maisha yao na iwapo watasoma kwa bidii wanaweza kuwa viongozi wakubwa wa serikalini hapo baadae

Alisema kuwa kunabaadhi ya watoto wa kike wamekuwa wanaacha kusoma kisa wanakimbilia maisha kitu ambacho sio kizuri kwani wanaweza kukimbilia maisha yakawapiga hivyo ni muhimu sana kama watasoma kwanza halafu maisha watayapata baadae baada ya kumaliza kusoma na kupata kazi zao nzuri.

PICHANI JUU: mbunge wa viti maalumu CCM Amina Mollel akiwa anacheza ngoma ya kimasai pamoja na baadhi ya wamasai waliojitokeza katika sherehe za kupandisha ngazi ya rika kutoka katika rika la kurianga kuingia katika rika la Nyangulo.
 Mbunge akiwa na wananchi walioudhuria katika sherehe hizo
Mbunge wa viti maalumu CCM Amina Mollel akiwa anasalimia na moja na mzee aliyekuwa rika la kurianga ambae kwa sasa ameingia katika rika  la Nyangulo   




PICHA ZA tiGOFIESTA: Show ya Morogoro

$
0
0

Wasanii Ben Pol na Jux wakishirikiana kuimba wimbo wao NAKUCHANA kwenye jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro juzi.

Country Boy akiimba na maelfu ya mashabiki waliojitokeza katika Tamasha la Tigo Fiesta

Rich Mavoko akitumbuiza katika jukwaa la Tigo Fiesta mkoani Morogoro mapema usiku wa kuamkia jumatatu.

MimiMars akiimba katika jukwaa la Tigo Fiesta mapema usiku wa kuamkia jumatatu mkoani Morogoro.

Barnaba akitumbuiza kwa maelfu ya mashabiki waliojitokeza kwenye Tamasha la Tigo Fiesta mkoani Morogoro.

NedyMusic aktumbuiza katika jukwaa la Tigo fiesta mapema juzi katika viwanja vya Jamhuri mkoani Dodoma.

Nandy akiburudisha wakazi wa Morogoro katika Tamasha la Tigo fiesta mapema juzi katika viwanja vya Jamhuri










Rais Trump: Shambulio la Texas limetokana na tatizo la akili

$
0
0

Trump amesema kisa cha mtu aliyewaua watu 26 kwa kuwapiga risasi katika kanisa dogo la jimbo la Texas kilitokana na matatizo ya akili wala si mjadala kuhusu umiliki wa bunduki

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa kisa cha mtu aliyewaua watu 26 na kuwajeruhi wengine 20 kwa kuwapiga risasi katika kanisa dogo la jimbo la Texas kilitokana na matatizo ya akili na wala si suala la mjadala kuhusu umiliki wa bunduki. Trump ameyasema hayo akiwa ziarani nchini Japan, sehemu ya ziara yake barani Asia .

Akijibu swali aliloulizwa na mwandishi wa habari mjini Tokyo, kuhusu sera anazoweza kuunga mkono kuhusiana na shambulizi la risasi ambalo limesababisha vifo vya watu 26 katika jimbo la Texas, Rais Trump amejibu kwa kusema kulingana na ripoti ya awali ya uchunguzi wa tukio hilo, mtu huyo aliyekuwa na bunduki alikuwa na matatizo ya akili. Trump ambaye yuko nchini Japan, kituo cha kwanza cha ziara ya siku 12 katika nchi tano za Asia, ameongeza kuwa nchi yake inakumbwa na wakati mgumu lakini suala la umiliki wa bunduki halipaswi kulaumiwa kuhusiana na kisa hicho.

"Ninafikiri ni tatizo la akili. Tuna matatizo mengi ya akili katika nchi yetu kama ilivyo katika nchi nyingine, lakini hili halihusiani na suala la bunduki. Kwa bahati mzuri mtu mwengine alikuwa na bunduki upande wa pili na kufyatua risasi dhidi yake. Hili ni suala la tatizo kubwa la akili, ni tukio la kuhuzunisha sana. Ndivyo ninavyoiona mimi" Amesema Trump.

Tukio hilo la usiku wa kuamkia Jumapili , limejiri wiki tano tu baada ya shambulio baya zaidi la risasi katika histora ya Marekani katika miaka ya hivi karibuni.

Mtu huyo mwenye bunduki, aliwafyatulia risasi watu waliokuwa wakiingia kanisani, katika kanisa la Baptist eneo la Sutherland Springs, takriban kilomita 65 mashariki kwa San Antonio, kisha akaingia kanisani na kuendelea kuwapiga watu risasi, akawaua waumini walio na umri wa kati ya miaka 5 hadi 72.


Mshukiwa wa shambulizi hilo apatikana amekufaMaafisa wameeleza kuwa mshambuliaji huyo ambaye ametambuliwa kwingi kwa jina la Devin Kelley, mzungu mwenye umri wa miaka 26, alitoroka kwa kutumia gari lake baada ya kufyatuliwa risasi na raia aliyekuwa na bunduki. Baadaye alipatikana amekufa katika kaunti jirani.

Haikubainika moja kwa moja ikiwa mshukiwa alijiua mwenyewe au kama alipigwa na risasi. Hayo yamesemwa na maafisa.

Jeshi la angani la Marekani limesema Kelley alihudumu katika kambi ya jeshi la New Mexico kuanzia mwaka 2010 kabla ya kupewa hukumu ya kifungo cha mwaka mmoja na mahakama ya kijeshi baada ya kupatikana na hatia ya kumpiga mkewe na mwanaye.

Mwandishi: John Juma/RTRE/AFPE

Rais Mugabe amemtimua kazi Makamu wake

$
0
0
Makamu wa Rais nchini Zimabawe Emmerson Mnangagwa amefutwa kazi, kwa mujbu wa wizara ya habari nchini humo.

Bw. Mnangagwa, 75, alionyesha tabia za kukosa uzalendo, waziri Simon Kahaya Moyo alisema.

Kufutwa kwake ni ishara kuwa mke wa rais Robert Muabe, Grace, atafuata nyayo za mumeme za kuwa rais wa Zimbabwe

Mapema Grace alitoa with wa kutaka mumewe amfute kazi Mnangawa.

Bwana Mnangagwa, ambaye ni mkuu wa zamani wa idara ya ujasusi amekuwa kwenye mstari wa mbele kumrithi Rais Mugabe.

Kufutwa kwake kunakuja baada ya Rais Robert Mugabe, 93, kutisha kumfuta Bw Mnangagwa, hatua ambayo imezua uvumi kuwa anataka mke wake amrithi.

Akihutubia wanachama wa makanisa ya asili mji Harare siku ya Jumapili, Bi Mugabe alisema:

"Nyoka ni lazima apiwe kwenye kichwa. Lazima tukabiliane na nyoka mwenyewe anayehusika na migawanyiko chamani.Tuneelekea kwenye mkutano tukiwa chama kimoja."

Bw Mugabe alimtaka Mnangagwa na wafuasi wake kumuonyesha uzalendo au afutwe kazi.

Zanu-PF kinatarajiwa kuifanyia mabadiliko katiba yake wakati wa mkutano na kuweka nafasi mbili za makamu wa rais moja ikiwa ni ya mwanamke.

Nafasi hiyo inatarajiwa kujazwa na Bi Mugabe na kuongeza uwezekano wa kumrithi mume wake.

- BBC Swahili

Wanawake 26 Wanaijeria wafariki baharini Italia

$
0
0
Miili ya wanawake 26, inayoaminika kuwa ya raia wa Nigeria, imepatikana katika ufukwe wa bahari nje kidogo ya pwani ya Italia.

Wanawake hao, ambapo mdogo zaidi kwa umri anaaminika kuwa wa miaka 14, walikuwa wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterranean kutokea Libya ili kuingia Bara Ulaya.

Haijabainika mara moja kiini kilichosababisha wanawake wengi kiasi hicho kufa kwa wakati mmoja, kwani kulikuwepo pia na wanaume kwenye meli iliyokuwa ikiwasafirisha.

Kuna shaka kuwa, huenda walibakwa na kisha kuuwawa, walipokuwa wakivuka kupitia njia hiyo hatari ya bahari ya Mediterranean.

Waendesha mashtaka nchini Italia, kwa sasa wanachunguza kubaini kiini hasa kilichosababisha maafa hayo, kwani wanawahoji wahamiaji watano katika mji wa bandarini wa Salerno ulioko Kusini mwa Italia.


- BBC Swahili

PICHA ZA RAIS MAGUFULI: Katika uzinduzi wa uwanja wa Ndege Bukoba

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Andre Bald, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli  wa pili kutoka (kushoto) pamoja na viongozi wengine wa Serikali kuashiria ufunguzi rasmi wa Uwanja wa ndege wa Bukoba mkoani Kagera.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi pamoja na viongozi hao mara baada ya ufunguzi wa rasmi wa Uwanja wa ndege wa Bukoba mkoani Kagera.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mkono na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Andre Bald mara baada ya ufunguzi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Andre Bald kuashiria ufunguzi wa wa rasmi wa Uwanja wa ndege wa Bukoba mkoani Kagera.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshikana mikono na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Andre Bald, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli wanne kutoka kushoto waliokaa pamoja na viongozi wengine mara baada ya kukagua chumba cha abiria uwanjani hapo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Mke wake Mama Janeth Magufuli watatu kutoka kulia wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wabunge, viongozi wa Serikali pamoja na Viongozi wa  Dini mara baada ya ufunguzi wa uwanja huo wa Ndege.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na kumshukuru Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Andre Bald mara baada ya shughuli za ufunguzi wa Uwanja wa ndege wa Bukoba.
Wananchi wakishangilia wakati wa Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya ufunguzi wa Uwanja wa ndege wa Bukoba.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kabla ya ufunguzi huo wa uwanja wa ndege wa Bukoba mkoani Kagera. 
PICHA NA IKULU

Wataalamu wafundwa jinsi ya kuandika maandiko mafupi ya kitafiti

$
0
0




Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) imewezesha warsha ya siku 3 kuwajengea uwezo watafiti wa ndani waweze kuandika andiko bora la kuombea fedha kwa ajili ya tafiti.

Warsha hiyo iliyofadhiliwa na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Maendeleo (International Development Research Centre-IDRC) kupitia Jukwaa la Wanazuoni Wabobezi (Think Tank Initiatives), ilifanyika makao makuu ya ESRF, Dar es salaam.

Akizungumza Jijini hapa, Mtalaamu Mwandamizi wa Programu ya Think Tank Initiatives anayeshughulikia Sera za Uchumi, Dkt. John Okidi kutoka (IDRC), amesema kwamba watafiti kutoka nchini za Senegali, Tanzania, Uganda, Ghana na Kenya walikutana kwa siku tatu kujadili na kubadilishana mawazo namna ya kujenga uwezo katika kuandika maandiko thabiti ya kuomba fedha kutoka mashirika mbalimbali ya kimataifa.

Alisema kuna umuhimu wa kufanya andiko linaloeleweka ili kuweza kushawishi watoa ruzuku kutoa fedha za utafiti ili kuharakisha mapinduzi ya viwanda nchini.

“Watafiti lazima wawe mstari wa mbele katika kushawishi wanasiasa na viongozi kutegemea zaidi tafiti katika kuleta matokeo chanya kwa wananchi na kusukuma umuhimu wa kutumia tafiti katika kufanya maamuzi kwenye ngazi zote za maamuzi,” aliongeza Dkt. Okidi

Alisisitiza umuhimu wa utafiti katika utungwaji wa sera za maendeleo ya kiuchumi hususani katika kipindi hiki ambacho Tanzania inafanya mageuzi makubwa ya kuingia kwenye uchumi wa viwanda.

Aliongeza kwamba Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Maendeleo-IDCR ina programu ya miaka kumi ambayo inatarajiwa kukamilika mwaka 2019.

Alisisitiza kwamba bila tafiti bora na makini ni vigumu kuwa na sera bora zaidi katika utatuzi wa changamoto za binadamu katika maeneo mbalimbali hasa maeneo ya vijijini.

Dkt. Okidi amesema kwamba watafiti wana umuhimu mkubwa sana katika kushiriki kwenye ukuaji wa sekta nyingi kama vile gesi, mafuta, biashara na maeneo mengine ya uwekezaji katika kuongeza tija na mafanikio ya uhakika baada ya matokeo ya utafiti.

Mtalaamu Mwandamizi wa Uwezeshaji Maendeleo na Mafunzo wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Maendeleo (IDRC) kupitia program ya TTI , Julie LaFrance, amesema kwamba ni muhimu kwa watafiti kuendelea na utafiti endelevu na wa kina ili kuweza kuleta matokeo chanya kwa jamii ya watu baada ya kupata matokeo baada ya utafiti.

Aliongeza kwamba baada ya semina hiyo watafiti wa ndani watakuwa wamepata uelewa mkubwa wa kuandika mapendeko thabiti na bora zaidi yenye kuvutia wadau wa maendeleo na mashirika ya kimataifa kuanza kuwapa fedha kwa ajili ya tafiti zenye tija nchini.
Warsha hiyo pia iliwakutanisha watafiti kutoka Taasisi ya IPAR- Senegal, Taasisi ya Takwimu, Jamii na Utafiti wa uchumi (ISSER), REPOA, ESRF, STIPRO na chuo cha Jamii kutoka Ghana.

PICHANI JUU: Mkuu wa kitengo cha Uwezeshaji na Utawala Bora wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Danford Sango akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa warsha ya siku tatu ya uwezeshaji wa maandiko bora ya utoaji ruzuku iliyoandaliwa na ESRF kwa ufadhili wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Maendeleo (IDRC) kupitia Taasisi ya Kimataifa ya Wanazuoni (Think Tank Initiatives-TTI) na kumalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mtalaamu Mwandamizi wa Uwezeshaji Maendeleo na Mafunzo wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Maendeleo (IDRC), Julie LaFrance akifungua warsha ya siku tatu ya uwezeshaji wa maandiko ya utoaji ruzuku iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

Picha juu na chini ni Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Uwezeshaji Maendeleo Afrika, Prof. Olu Ajakaiye akielezea namna bora ya utengenezaji wa maandiko kwa ufupi na kwa usahihi wakati wa warsha ya siku tatu ya uwezeshaji wa maandiko ya utoaji ruzuku kwa washiriki kutoka shirika la IPAR- Senegal, Taasisi ya Takwimu, Jamii na Utafiti wa Uchumi (ISSER), REPOA, ESRF, STIPRO na Chuo cha Jamii kutoka Ghana iliyomalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa ESRF.

Mtaalamu wa Uwezeshaji Jinsia, Maureen Miruka akiwasilisha mada umuhimu wa jinsia kama moja ya kipengele muhimu katika kuandaa maandiko mbalimbali ya kitafiti katika kushawishi wabia wa maendeleo kutoa ruzuku za uatfiti.
Mtalaamu Mwandamizi wa Uwezeshaji Maendeleo na Mafunzo wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Maendeleo (IDRC), Julie LaFrance akifurahi jambo wakati mada mbalimbali zikiwasilishwa kwenye warsha hiyo iliyomalizika mwishoni mwa juma katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene (kulia) akichangia jambo wakati wa warsha ya siku tatu ya uwezeshaji wa maandiko ya utoaji ruzuku iliyoandaliwa na ESRF kwa ufadhili wa IDCR kupitia Think Tank Initiatives-TTI.
Prof. Peter Okidi-Lating (aliyesimama) kutoka Chuo Kikuu cha Makerere akipitia meza za vikundi kazi vya washiriki wa warsha ya siku tatu ya uwezeshaji wa maandiko ya utoaji ruzuku iliyoandaliwa na ESRF kwa ufadhili wa IDCR kupitia Think Tank Initiatives-TTI.
Mtaalamu wa Uwezeshaji Jinsia, Maureen Miruka akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa zoezi la vikundi kazi katika meza ya washirki kutoka ESRF katika warsha hiyo iliyomalizika mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam.
Pichani juu mshiriki Aldegunda Ngowi kutoka ESRF na chini ni mshiriki kutoka Ghana wakichangia mada mbalimbali kwenye warsha hiyo.
Pichani juu na chini ni sehemu ya washiriki wa warsha ya siku tatu ya uwezeshaji wa maandiko ya utoaji ruzuku kutoka Shirika la IPAR- Senegal, Taasisi ya Takwimu, Jamii na Utafiti wa Uchumi (ISSER), REPOA, ESRF, STIPRO na Chuo cha Jamii kutoka Ghana.
Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene (kulia) akibadilishana mawazo na Mtalaamu Mwandamizi wa Uwezeshaji Maendeleo na Mafunzo wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Maendeleo (IDRC), Julie LaFrance wakati warsha ya siku tatu ya uwezeshaji wa maandiko ya utoaji ruzuku iliyoandaliwa na ESRF kwa ufadhili wa IDCR kupitia Think Tank Initiatives-TTI. 

Tafiti za kilimo zafika shambani Urambo kwa mara ya kwanza

$
0
0
Na Dotto Mwaibale, Urambo Tabora
TAFITI za kilimo zinazofanywa hapa nchini na wataalamu zimewafikia wakulima wa Wilaya ya Urambo mkoani Tabora kwa mara ya kwanza.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Halmshauri ya wilaya hiyo Adamu Malunkwi wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye uzinduzi na kukabidhi mbegu bora za Mahindi ya Wema 2109 na mihogo kwa ajili ya mashamba darasa kwa wakulima wa vijiji nane vya Isongwa, Ussoke, Usisya, Kapiluka, Vumilia, Kamalendi, Muungano na Songambele.

Alisema mara nyingi tafiti zilizokuwa zikifanyika zilikuwa zikibaki kwenye makabati bila ya kuwafikia walengwa na jambo lililofanywa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kushirikiana na Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB) kuwafikishia wakulima matokeo ya tafiti hizo ni jambo zuri na limefurahiwa na kwa hapa kwetu ni mara ya kwanza kutokea.

"Tuna amini kuwa hivi sasa uchumi utastawi kuanzia ngazi ya familia, wilaya na hadi taifa na tutakuwa na chakula cha kutosha" alisema Malunkwi.

Malunkwi alisema katika wilaya hiyo walikuwa na changamoto kubwa ya kupata mbegu bora kwani wakulima wengi walikuwa wakitumia mbegu za zamani walizozizoea na kujikuta wakipata mazao kiduchu lakini kwa ujio wa mbegu hizo ni ukombozi mkubwa kwao.

Alitaja changamoto nyingine ambayo inapaswa kuangaliwa kwa karibu kuwa ni bei kubwa ya mbegu hiyo ya mahindi ambayo inauzwa shilingi 12,000 kwa kilo mbili huku kukiwa na debe moja la mahindi linalouzwa shilingi 10,000 ambalo wakulima wamekuwa wakilikimbilia kutokana na bei yake kuwa ya chini ingawa mazao yake hayana tija.

Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH ambaye ni Ofisa Mwandamizi wa COSTECH, Audax Mutagwa, alisema mbegu hiyo ya mahindi imefanyiwa utafiti na inavumilia ukame wakati ile ya mihogo ikivumilia magonjwa kama batobato na michirizi kahawia huku zikitoa mavuno mengi.

Alisema COSTECH katika mkoa huo imetoa kilo 60 za mbegu ya Wema, mihogo 40,000 na viazi lishe 75 ambapo katika wilaya hiyo vijiji nane vimenufaika kwa ajili ya kutengeneza mashamba darasa ambayo yatatoa mbegu zitakazosambazwa kwa wakulima katika maeneo mengine. 

Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora katika uzinduzi wa mashamba darasa hayo ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi Uchumi, Phillips Mtiba alisema hivi sasa mwajiriwa ni mkulima ambaye analima kilimo chenye tija na si vinginevyo na kuwa serikali siku zote imekuwa ikihimiza kilimo bora ambapo aliwataka maofisa ugani kupanga ratiba za kuwafikia wakulima.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Angelina Kwinga aliishukuru COSTECH na OFAB kwa kutekeleza ahadi ya kuwapelekea mbegu kama walivyo ahidi walipokuwa wakitoa mafunzo kwa maofisa ugani wa wilaya hiyo mapema mwaka huu.

PICHANI JUU:  Mshauri wa Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB), Dk.Nicholaus Nyange, akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Urambo mkoani Tabora, Angelina Kwinga mbegu ya mihogo inayostahimili ukame katika uzinduzi wa mashamba darasa ya mbegu hiyo ya mihogo, mahindi aina ya Wema 2109  pamoja na viazi lishe yalioanzishwa kwa ajili ya wakulima wa vijiji nane katika wilaya hiyo leo kwa ufadhili wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kushirikiana  OFAB.



 Ofisa Mtendaji wa Kata ya Ugalla, Geofrey Magambo akizungumza katika uzinduzi huo wakati akiwatambulisha viongozi mbalimbali wa Kata hiyo na Kijiji cha Isongwa.
 Ofisa Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Said Babu akizungumza katika uzinduzi huo.
 Mshauri wa Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB), Dk.Nicholaus Nyange (kulia), akizungumza kwenye uzinduzi darasa wa shamba la mahindi katika Kijiji cha Isongwa kilichopo Kata ya Ugalla Ussoke wilayani Urambo mkoani Tabora.
 Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora katika uzinduzi wa mashamba darasa hayo ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi Uchumi, Phillips Mtiba akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa huo.
 Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora katika uzinduzi wa mashamba darasa hayo ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi Uchumi, Phillips Mtiba, akikabidhiwa mbegu ya mahindi ya Wema na Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH, Ofisa Mwandamizi wa COSTECH, Audax Mutagwa.
 Wananchi wa Kijiji cha Isongwa wakisubiri kupata mafunzo ya upandaji wa mbegu ya mahindi katika shamba darasa.
 Mtafiti, Ismail Ngolinda kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga, mkoani Morogoro akitoa maelezo kwa wakulima wa Kijiji cha Isongwa jinsi ya kupanda mahindi aina ya Wema.
 Mkulima wa Kijiji cha Isongwa, Malando Malando akiuliza swali.
 Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Isongwa, Shabani Rajabu Mkokoteni akiuliza swali.
 Wanawake wakulima wa Kijiji cha Isongwa wakijumuika kwenye uzinduzi huo wakiwa na watoto wao.
 Mtafiti, Ismail Ngolinda kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga, mkoani Morogoro, akionesha uchimbaji wa mashimo kabla ya kupanda mbegu hiyo ya mahindi.
 Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Isongwa, Shabani Rajabu Mkokoteni , akichimba mashimo.
 Mtafiti, Ismail Ngolinda kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga, mkoani Morogoro, akionesha, akionesha namna ya kuweka mbolea kwenye mashimo yaliyochimbwa.
  Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora katika uzinduzi wa mashamba darasa hayo ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi Uchumi, Phillips Mtiba, akipanda mahindi.
 Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH, Ofisa Mwandamizi wa COSTECH, Audax Mutagwa, akipanda mahindi.



 Mwenyekiti wa Halmshauri ya wilaya hiyo Adamu Malunkwi, akizungumza na wakulima wakati wa uzinduzi huo.
 Mtafiti wa Mazao ya Mizizi kutoka Kituo cha Ufatiti cha Maruku mkoani Kagera, Jojianas Kibura, akiwaelekeza wakulima wa Kijiji cha Usisya namna ya kupanda mbegu ya viazi lishe.
 Wakulima wa Kijiji cha Kapiluka wakijiandaa kupanda mbegu ya viazi lishe.
Mtafiti wa Mazao ya Mizizi kutoka Kituo cha Ufatiti cha Maruku mkoani Kagera, Jojianas Kibura, akiwaelekeza wakulima wa Kijiji cha Motomoto namna ya kupanda mbegu ya viazi lishe.






SERIKALI IMETOA BURE: Mbegu, na vijatilifu kwa ajili ya kilimo cha Pamba Singida

$
0
0
 Serikali imeahidi kutoa bure pembejeo za kilimo kwa wakulima mbali mbali wa zao lapamba mkoani Singida kuanzia msimu huu wa kilimo ikiwa ni moja ya juhudi za kuhamasisha na kufufua kilimo hicho mkoani hapa.  

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bodi ya Pamba nchini, Marco Mtunga ameeleza hayo juzi katika vijiji vya Kinyangiri na Lyelembo wilayani Mkalama katika siku ya kwanza ya ziara yake ya siku mbili kuhimiza Kilimo cha pamba mkoani Singida. 

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, Kampuni ya Biosustain iliyopo mjini hapa imepewa jukumu la kuleta na kusambaza mbegu na madawa yote yahusuyo kilimo cha pamba bure na kwamba gharama ya pembejeo hizo italipwa na Serikali. 

Kutokana na hilo, Mkurugenzi huyo amewataka Wakulima kutumia vyema fursa hiyo kwa kulima mashamba makubwa zaidi lakini pia kwa kuzingatia tija na ubora wa pamba. 
Amesema kuwa Wakulima wataweza kufanya hivyo tu iwapo pia watawatumia kikamilifu wataalamu wao wa kilimo na kufuata Kanuni na Taratibu za kilimo bora. 

“Mmepewa upendeleo maalum, kazi yenu sasa ni kulima tu, malipo ya mbegu na viuatilifu vyote italipwa na Serikali. Hapa hakuna kisingizio cha kushindwa kulima”, amesema Mtunga na kuongeza;

“Pandeni vizuri ili wakati mnatumia dawa, kiwango kikubwa cha dawa kisipotee bure maana kama hukupanda kwa mstari lazima kutakuwa na ugumu wa kupulizia mimea yako. Jengeni utamaduni wa kuwatumia wataalamu wa kilimo kama ilivyo kwa wafugaji mifugo yao inapopatwa na maradhi”.  

Aidha, amewataka wakulima wa zao hilo kuhakikisha wanang'oa masalia yote ya misitu ya pamba na kuichoma moto kwa kuwa, kwa kuacha kufanya hivyo wanaruhusu wadudu waliomo kwenye masalia kuendelea kunenepeana na hivyo kuhatarisha mazao mapya yanayopandwa.  

Mkurugenzi huyo amewasihi wakulima kuacha kuchanganya kilimo cha pamba na mazao mengine akisema kuwa tafiti zinaonesha pamba iliyochanganywa na mazao mengine hutoa vitumba vitatu tu ikilinganishwa na vitumba 10 kwa kilimo cha pamba iliyolimwa peke yake. 

Wakulima wa zao hilo wamemueleza Mkurugenzi huyo kuwa, moja ya sababu za kushuka kwa uzalishaji pamba kwenye maeneo yao ni pamoja na bei kuwa ndogo kwa kisingizio cha Soko la Kimatafa kushuka na kuchezewa mizani wanazotumia kupima mazao yao, hali inayowapunja kimapato.  

Hata hivyo, wamejibiwa kuwa suluhisho la kuchezewa mizani lipo mikononi mwao ili mradi tu wajenge tabia ya kuhoji mara moja wanapoona mambo yanaenda isivyo badala ya kusubiri hadi siku ya vikao. 

Wakati huohuo Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi amewataka watendaji wote wa serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Singida kulima ekari moja ya pamba kila mmoja ili kuamsha hamasa kwa wananchi wengine.

Dkt Nchimbi ameongeza kwa kuwataka watendaji hao kuliweka zao la pamba kama ajenga katika vikao vyao, huku akiwataka viongozi wa dini na vikundi vya kwaya kuonyesha mfano kwa kulima vizuri pamba.

Ameongeza kuwa vijana wanaocheza vijiweni ‘pooltable’ waache mara moja na kujikita katika kilimo cha pamba kwa kuwa ni chanzo kikubwa na cha uhakika cha kujipatia fedha na hivyo kuchangia kukuza uchumi. 

Aidha amewataka wakulima wa pamba kuwasikiliza wataalamu na sio kupanda kwa mazoea huku akishauri kuwa mikutano yote inayohusu kilimo cha pamba ifanyike katika mashamba ya wakulima.

Dkt Nchimbi ameeleza kuwa kauli mbiu mpya ya kilimo cha pamba kwa Mkoa wa Singida ni, ‘Singida Mpya, kwa Pamba yenye Tija’. 

PICHANI JUU: Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi (katikati) akimkabidhi mmoja kati ya wa wakulima wa Pamba wa kijiji cha Kinyangiri Wilayani Mkalama kilo kumi za mbegu za zao la pamba zilizotolewa bure na Serikali kwa wakulima hao. Kushoto kwa Mkuu wa Mkoa ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bodi ya Pamba nchini, Marco Mtunga.
 Mkulima wa Pamba Bi Johari kutoka kijiji cha Kinyagiri Wilayani Mkalama akibeba mbegu za Pamba kilo kumi alizokabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi, mbegu hizo zimetolewa bure kwa wakulima wa Pamba Mkoa wa Singida
Mama Devid Mkulima wa Pamba wa Kijiji cha Kinyangiri Wilayani Mkalama akijifunza kwa vitendo namna ya kuandaa kamba inayotumika kuonyesha vipimo vya upana na urefu katika kupanda pamba badala ya kilimo cha mazoea cha kumwaga mbegu bila kufuata kipimo chochote.
 Wakulima wa Pamba wa Kijiji cha Lyelembo Wilayani Mkalama wakiwasikiliza Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bodi ya Pamba nchini Marco Mtunga (hawapo pichani) kabla ya kupewa mbegu za pamba zilizotolewz bure.
Wakulima wa pamba wa kijiji cha Kinyangiri Wilayani Mkalama wakimfuatilia kwa makini mtaalam kutoka Bodi ya Pamba Nchini akiwaelekeza namna ya kupuliza dawa ya kuuwa wadudu waharibifu wa pamba, viuatilifu hivyo vitatolewa bure na serikali kwa wakulima wote wa pamba Mkoani Singida.


USHAISKIA? Programu mpya ya U900 kutoka Airtel ya kuboresha huduma za Intaneti

$
0
0



Airtel Tanzania Plc kampuni ya mawasiliano iliyojikita katika huduma zenye ubunifu wa teknolojia zaidi nchini, leo katika muendelezo wake wa kutimiza dhamira yake ya kuwa mtandao bora zaidi imetangaza na kuzindua rasmi programu yake ya maboresho ya huduma za mtandao wake kupitia teknolojia ya iliyopewa jina la ‘Mradi wa U900’ ukiwa na lengo la kuimarisha ubora wa mtandao na kutoa huduma bora kwa wateja wake mahali popote nchini.
Mradi wa U900 ni uwekezaji mkubwa unaolenga kuhakikisha uhakika wa upatikanaji wa huduma ya 3G, ujazo wa data kamili pamoja na kuongeza kasi ya intaneti kwa kutumia teknolojia hii ya mawimbi ya mawasiliano ya masafa ya 900 Mhz. Teknolojia hii itaongeza upatikanaji wa mtandano wa 3G kwa Asilimia 50 zaidi pamoja kuongeza ubora wa upatikani wa intaneti bila kujali maeneo mteja alipo, Popote utapata Intaneti bora. 

Akiongea leo jijini Dar es Salaam wakati wa kutangaza huduma hiyo, Meneja Ubora wa huduma za Mtandao Airtel, Emanuel Luanda alisema kuwa Airtel imewekeza kwenye kuimarisha huduma ya mtandao kutokana na ongezeko la matumizi ya simu za smartphone na pia kutokana na uhitaji wa huduma mpya za ziada. Kutokana na uboreshaji wa mtandao wetu, wateja wote nchini watakuwa wakitapa huduma yenye kasi na hivyo kuwa na uhakika na huduma bora kutoka Airtel wakiwa popote.

Bw, Luanda alidokeza “ripoti ya hivi karibuni ya TCRA inayotoa mchanganuo wa matumizi ya huduma za Intaneti (Data) inaweka wazi kuweko kwa ongezeko la watumiaji wa huduma za intaneti kutokea 34% kwa mwaka 2015 na kupaa hadi 40% kwa mwaka 2016. Hali hiyo ndio inatoa msukumo hata kwetu Airtel kuendelea kuwekeza zaidi katika teknolojia mpya ili kuwapatia wateja wetu huduma bora zaidi”.

“Tayari tushafanya maboresho kwenye miji ya Dar es Salaam, Arusha na Mwanza huku maboresho mengine yakiendelea kufanyika Dodoma, Morogoro na miji mingene yenye uhataji mkubwa wa huduma zetu hapa Tanzania.” Alieleza Luanda

Kwa upande wake, Meneja wa Masoko Airtel Tanzania Arnold Madale alisema, “kwa kuwa Airtel tunatambua mahitaji ya wateja wetu, hali ya soko tumekuwa tukifanikiwa kuleta bidhaa zenye ubunifu na mpangilio wa huduma zinazozingatia mahitaji ya mteja, hii ni hatua kubwa sana hasa kwenye ushindani wa biashara.

Tunao wateja ambao wanatumia mtandao wetu kwa ajili ya intaneti tu, lakini pia kuna wale wanaotumia kwa kupiga na kupokea simu, tunazo bidhaa na huduma ambazo zinakidhi matakwa ya wateja hao kwa muda wote wakiwa mahali popote.

Kwa sasa hivi tunaendelea pia kuboresha huduma yetu ya 2G ili kutoa huduma yenye uhakika wa hali ya juu ikiwemo huduma ya Airtel Money ili kuendelea kuwafikia Watanzania wengi waishio pembezoni huduma za kibenki na huku tukitimiza sera ya serikali ya kushiriki katika uboreshaji wa huduma bora za kifedha vijijini.”

“Tunapotangaza huduma hii muhimu ya kuboresha mtandao wetu, tunayo furaha kutangazia huduma ya Bando la OFA KABAMBE ambayo inapatika kwa urahisi na kumfanya mteja kuwa na Uhuru zaidi wa kutumia Intaneti yenye kasi kwa muda mrefu zaidi kwa kuwasiliana na ndugu, marafiki au wadau katika biashara mahali popote. Wateja wetu wataweza kufaidi huduma hii ya bando kwa kupiga *150*60# na kujipatia 1GB, dakika150 kupiga mitandao yote na kudumu nazo kwa muda wa siku saba, aliongeza Madale.

‘Nia yetu ni kuendelea kukua kupita Maelezo huku tukitengeneza ujuzi wa kuaminiwa na wateja wetu kwa kuwa na gharama nafuu. Mradi wa U900 unadhihirisha kuwa Airtel imeamua kuinua taifa letu kufikia lengo la kuishi kidigitali kwa kuwepo na huduma za kidigitali, aliongeza Madale.

PICHANI JUU: Meneja Chapa na Masoko Airtel Tanzania Anorld Mandale akishika bango baada ya kuzindua huduma ya Bando la OFA KABAMBE ambapo wateja wataweza kufaidi huduma hii kwa kupiga *150*60# na kujipatia 1GB, dakika150 kwa muda wa siku saba. Kushoto ni Meneja Ubora wa huduma za Mtandao wa Airtel Tanzania Emmanuel Luanda na Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando

Meneja Uhusiano wa AIRTEL Tanzania Jackson Mmbando akizungumza na waandishi wa habari leo katika uzinduzi wa programu mpya ya Airtel U900 ambao lengo lake kuu ni kuimarisha ubora wa mtandao na kutoa huduma bora kwa wateja wake mahali popote nchini. Mradi Tayari ushazinduliwa na kuwasha mitambo kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza na Arusha. Kulia ni Meneja Ubora wa huduma za Mtandao Emmanuel Luanda
Meneja Ubora wa huduma za Mtandao wa Airtel Tanzania Emmanuel Luanda akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam baada ya kuzindua programu mpya ya Airtel U900 ambao lengo lake kuu ni kuimarisha ubora wa mtandao na kutoa huduma bora kwa wateja wake mahali popote nchini. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Jackson Mmbando. Teknolojia hii itaongeza upatikanaji wa mtandano wa 3G kwa Asilimia 50 zaidi pamoja na kuongeza ubora wa upatikaniji wa intaneti bila kujali maeneo mteja alipo.

Meneja Chapa na Masoko Airtel Tanzania Anorld Mandale baada ya kuzindua programu mpya ya Airtel U900 ambao lengo lake kuu ni kuimarisha ubora wa mtandao na kutoa huduma bora kwa wateja wake mahali popote nchini. Kampuni hiyo pia huduma ya Bando la OFA KABAMBE ambapo wateja wataweza kufaidi huduma hii kwa kupiga *150*60# na kujipatia 1GB, dakika150 kwa muda wa siku saba

Mfumo wa kutengeneza na kusambaza filamu za Kitanzania (Bongohoodz) wazinduliwa

$
0
0


Kampuni za utengenezaji filamu za Mashauri Studios na Novitech kwa kushirikiana na Clouds Plus pamoja na Shirikisho la Filamu Tanzania imezindua rasmi mfumo wa kutengeneza, kutangaza, kuonyesha na kusambaza filamu za kitanzania ujulikanao kama Bongohoodz.

Akizungumza na waandishi wa habari, mwanzilishi mwenza wa Bongohoodz ambaye pia ni mtayarishaji wa filamu na Mkurugenzi wa Mashauri Studios, Paul Mashauri, mfanyabiashara ambaye katika miaka ya hivi karibuni alimua kuwekeza katika filamu alisema Bongohoodz inakuja kuwasaidia waandaaji wa filamu nchini kutatua tatizo la wizi wa kazi za sanaa hasa DVDs kutokana na usambazaji wa sinema feki unaofanywa na baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu.

“Baada ya kutoa sinema kazaa sokoni ikiwa ni pamoja na One Month Date mwaka 2014, Maisha ni Siasa na Bongo na Fleva mwaka 2015 tumegundua kuwa wizi wa kazi za sanaa ‘piracy’ ni mkubwa sana. Lakini kupitia Bongohoodz, watayarishaji wa sinema nchini hawatahitaji tena kusubiri mapato yao au uwekezaji wao urudi kwa kuuza DVDs,

"Kimsingi hata katika nchi zilizopiga hatua katika sinema unazungumzia Hollywood (Marekani), Bollywood (India), China Film Industry (China) na Nollywood (Nigeria), mapato makubwa yanatokana na uonyeshaji wa sinema katika majumba ya sinema au ‘theaters’ wao wanaita ‘Box Office’. Kwa sababu wizi wa kazi za sanaa upo dunia nzima," alisema Mashauri na kuongeza.

"Lakini mapato ya kwanza wanayopata waandaaji wa sinema au ‘production houses’ yanatoka ‘Box office’ au katika nyumba za kuonyesha sinema. Ndio maana sisi tutasema, kwanini tusionyeshe sinema hizi nchi nzima katika matamasha makubwa ambapo watanzania watapata kuona sinema zinazoburudisha na kufundisha kwa bei nafuu kabisa huku wakifurahia vyakula mbalimbali, muziki, kisha filamu?”

Mashauri alisema kuwa wameanza jitihada za makusudi za kutangaza sinema hizi ikiwa ni pamoja na kuwatangaza wasanii na wazalishaji wa sinema,“Dunia nzima waigizaji wenye majina makubwa ndio wanaovutia walaji au wanunuzi wa filamu, hata kwetu imezoeleka hivyo. Lakini ili muigizaji awe mkubwa lazima kazi yake ionekana.

"Kwa msingi huo na kwa ushirikiano wa vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na wadau wetu Clouds Plus, tumeanzisha ‘reality show’ ijulikanayo kama ‘The Producers’ inayoruka Clouds Plus kupitia king’amuzi cha Azam Tv kila siku jumatatu hadi ijumaa saa moja mpaka saa moja na nusu usiku na marudio siku ya jumapili kuanzia saa nne asubuhi ambapo watanzania wataweza kuona namna sinema zinavyotengenezwa na wasanii wanavyofanya kazi zao," alisema Mashauri.

Mashauri alisema kupitia kipiendi hicho watu mbalimbali ambao wanandoto za kuwa waigizaji watajua nini wa natakiwa kufanya kwani wataona fursa ziliziopo katika tasnia ya uigizaji na changamoto zinazowapata waandaji na waigizaji. "Tunategemea kufanya kazi na waandaaji kumi kwa mzunguko wa miezi sita sita na kila Producer atatakiwa kuzalisha sinema ndani ya miezi sita na mchakato wa sinema yake utaonyeshwa katika reality show, sinema yake itatangazwa na kupelekwa sokoni," alisema Mashauri.

Naye Meneja wa Clouds Plus, Ramadhani Bukini, alisema Clouds Plus imeungana na Bongohoodz katika kufanikisha ukuaji wa soko la filamu nchini kwa kutoa fursa kwa wazalishaji wa sinema kuonyesha kazi zao na kuzipeleka sokoni kupitia matamasha.

Tumeungana na Bongohoodz tukiamini kuwa lazima kuwe na mbinu mbadala za kuuza sinema. Dunia imebadilika sana na huwezi kutegemea chanzo kimoja cha mapato. Mfano, katika dunia ya leo, aina ya kompyuta zinazoongoza kwa kuuza duniani ni za Apple. Watumiaji wa ‘computer’ hizi hawahamasiki kutumia DVDs. Inamaana tunakoelekea hata wenye deki za kuangalia DVDs ni wachache,

"Watu wako kwenye simu za mikononi, ndio maana Clouds Plus ikaamua kuungana na Bongohoodz kuja na vyanzo vipya vya mapato kwa tasnia ya filamu Tanzania ikiwa ni pamoja na matamasha makubwa ya kuonyesha filamu. Kama imewezekana katika muziki tunaamini kabisa inawezekana katika filamu," alisema Bukini.

Naye mwanzilishi mwenza wa Bongohoodz ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya Novitech ambayo inashirikiana na Mashauri Studios katika kutayarisha sinema, Mary Mgurusi alisema watanzania wasubirie kwa hamu kazi nzuri za filamu.

“Tumeandaa sinema nzuri za kitanzania zenye maudhui tofauti tofauti ambazo tunaamini zinaburudisha na kufundisha. Tayari sinema ya Tatu Chafu imekamilika na tunatarajia kuizindua tarehe 16/12/2017 Mlimani City pamoja na Dar Live Mbagala. Baada ya uzinduzi huo, tunatarajia kuonyesha sinema hii nchi nzima katika mikoa mbalimbali. Zaidi ya Tatu Chafu zipo sinema nyingi katika maandalizi, mfano Tajiri kutoka India, What is Marriage, Rashid Snake Boy Matumla na School Bus," alisema Mgurusi.

MSIOGOPE: Deni la Taifa ni himilivu

$
0
0
Benny Mwaipaja, Dar es Salaam
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James amewatoa hofu watanzania kuhusu ongezeko la Deni la Taifa akisisitiza kuwa Deni hilo ni himilivu.

Bw. James amesema hayo Jijini Dar es Salaam kwa vyombo vya habari wakati wa hafla fupi ya kutia saini Mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa Shilingi bilioni 340 uliotolewa na Benki ya Dunia kwa ajili ya Mradi wa kuendeleza utalii kwa vivutio vilivyoko katika ukanda wa kusini mwa Tanzania ujulikao kama Resilient Natural Resource for Tourism and Growth (REGROW)

Alikuwa akitolea ufafanuzi kuhusu baadhi ya watu na vyombo vya habari vinavyozungumzia Deni la Taifa kwa kutumia neno Deni la Taifa “linapaa”

Katibu Mkuu huyo ambaye pia ndiye Mlipaji Mkuu wa Serikali alisema kuwa Deni la Taifa ni himilivu kwa kutumia viwango vya kitaifa na kimataifa kwamba ili nchi iwe katika hatari ya kukua kwa Deni lake la Taifa inabidi lifikie asilimia zaidi ya 50 lakini kwa Tanzania kiwango cha deni hilo ni asilimia 32.

“Deni letu lingekuwa linapaa, hata Benki ya Dunia wasingekubali kutukopesha kwa maana hiyo tukitaka kukopa tutafanya hivyo kwa kuwa tuko chini katika viwango vya ukopaji kwa asilimia zaidi ya 18” alisema Bw. Doto James.

Kwa hiyo nawaomba hili mlichukue muuelimishe umma wa watanzania kwamba deni la Taifa ni stahimilivu, nchi inakopesheka vizuri.

Novemba 7, 2017, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akiwasilisha Bungeni mjini Dodoma Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maanndalizi ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka 2018/2019 alisema kuwa Deni la Taifa limefikia dola za Marekani milioni 26,115.2 mwezi Juni mwaka 2017.

Dkt. Mpango alieleza kuwa ongezeko hilo ni sawa na asilimia 17 ikilinganishwa na dola milioni 22,320.76 katika kipindi kama hicho mwaka 2016.

Alisema ongezeko hilo lilichangiwa na mikopo mipya iliyochukuliwa ili kugharamia miradi ya maendeleo kama vile: Standard Gauge Railway; Strategic Cities; mradi wa usafirishaji Dar es Salaam (DART) na kupanua upatikanaji wa maji safi Dar es Salaam. 

Deni hilo la Taifa linajumuisha deni la Serikali lililofikia dola za Marekani milioni 22,443.70 na deni la sekta binafsi la dola za Marekani milioni 3,671.50. Pamoja na ongezeko hili, viashiria vyote bado vinaonesha kuwa deni la Taifa ni himilivu kwa kipindi cha muda mfupi, wa kati na mrefu huku uwiano kati ya deni na Pato la Taifa umefikia asilimia 31.2 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 56.

Obama ajitokeza kufanya kazi ya mzee wa baraza Chicago

$
0
0
Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama(Pichani juu) alifika katika majengo ya mahakama moja Chicago kuitikia wito wa kuhudumu kama mzee wa baraza la mahakama.

Hata hivyo, jaji alimwamuru aondoke bila kuhudumu.

Umati wa watu ulikusanyika katika jengo la manispaa la Daley Center kumuona rais huyo wa 44 wa Marekani, ambaye ana nyumba katika jiji la Illinois.

Bw Obama aliondoka kwake nyumbani mwendo wa saa tatu unusu saa za huko siku ya Jumatano na aliondoka majengo ya mahakama saa sita hivi mchana.

Kila mtu aliyekabidhiwa wito wa kuhudumu kama mzee wa baraza mahakamani hupokea hundi ya $17.20 (£13.11) kutoka kwa wilaya hiyo.

Helikopta za wanahabari zilitumiwa kupiga picha kutoka juu angani huku msafawa wa Bw Obama wa walinzi wa rais na marais wastaafu maarufu kama Secret Service ukipita kutoka nyumbani kwake mtaa wa Kenwood hadi kwenye jengo hilo la manispaa.

Obama alifika akiwa amevalia jaketi lakini bila tai, kisha ataingia kwenye lifti na kupanda hadi ghorofa ya 17.

Huko, alikutana na wazee wengine wa baraza la mahakama

Baada ya kutazama video ya "kupashwa mengi zaidi kuhusu kazi ya wazee wa baraza la mahakama," Jaji mwandamizi wa wilaya ya Cook Timothy Evans alimwamuru Bw Obama kuondoka.

Baadaye, Bw Obama alitoa hotuba ya kulipwa katika kampuni ya uwekezaji ya GCM Grosvenor, kwa mujibu wa gazeti la Chicago Sun-Times.

-BBC Swahili

BAADA YA KUFUTWA KAZI: Emmerson Mnangagwa aikimbia Zimbabwe

$
0
0
Aliyekuwa makamu wa rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa (Pichani Juu) ambaye alifutwa kazi siku ya Jumatatu amelitoroka taifa hilo kufuatia vitisho vya kifo , kulingana na washirika wake.

Rais Mugabe mwenye umri wa miaka 93 amemshtumu aliyekuwa makamu wake kwa kupanga njama za kuchukua mamlaka kutoka kwake.

''Alienda katika kanisa moja na Apostolic kujua ni lini Mugabe atafariki. Lakini aliambia kwamba atafariki wa kwanza'' , Mugabe aliwaambia wafuasi wake sikju ya Jumatano.

Mke wa Rais Grace Mugabe sasa ndio aliye kifua mbele kumrithi Urais mumewe

Bi Mugabe amekuwa akipigania kung'atuliwa kwa makamu huyo katika mkutano maalum wa chama tawala cha Zanu-PF mwezi Ujao.

Chama cha Zanu PF kilimfukuza uanachama Mnangagwa katika chama hicho siku ya Jumatano.


- BBC Swahili

Trump na Xi Jinping waanza mazungumzo China

$
0
0


Rais wa Marekani, Donald Trump amewasili China na tayari ameanza mazungumzo Rais wa nchi hiyo Xi Jinping, huku ajenda kuu ya mazungumzo yao ikiangazia zaidi mzozo wa silaha za nyuklia wa Korea Kaskazini na masuala ya kibiashara.

Trump amewasili tango jana kwenye mji mkuu wa China, Beijing akiwa na mkewe Melania na kupokelewa kwa bendi ya jeshi kabla ya kuelekea Forbidden City ambako kuna makumbusho ya kasri la kifalme, mji ambao anakutana na Rais Xi pamoja na mkewe Peng Liyuan.

Saa chache kabla ya kuwasili mjini Beijing, Trump aliitolea wito China kusaidia katika kukabiliana na uchokozi unaofanywa na Korea Kaskazini kutokana na mpango wake wa nyuklia. Ikulu ya Marekani imesema Trump ataitumia ziara hiyo kuiomba China kusitisha uhusiano wake wa kifedha na Korea Kaskazini na kuheshimu vikwazo vya Umoja wa Mataifa. China ni mshirika mkubwa wa kibiashara na Korea Kaskazini.

Akiwa Korea Kusini kiongozi huyo wa Marekani alizitaka China na Urusi kusaidia kuiwekea shinikizo Korea Kaskazini kusitisha kutengeneza silaha za nyuklia na kuileta nchi hiyo katika meza ya mazungumzo. Akizungumza katika Bunge la Korea Kusini mjini Seoul, Trump ametoa onyo kali kwa kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un ambapo amemtaka asiwadharau na wala asiwajaribu.

''Hatuwezi kuruhusu Marekani au washirika wetu kushambuliwa. Hatuwezi kuruhusu miji ya Marekani itishiwe na silaha za maangamizi. Hatutoogopa. Na hatutoruhusu ukatili mwingine ujirudie katika historia, kwenye ardhi hii ambayo tuliipigania na kufa kwa ajili ya kuilinda,'' alisema Trump.

Trump akilihutubia bunge la Korea Kusini
Rais Trump amezitaka Urusi na China kusitisha uhusiano wowote na Korea Kaskazini, ukiwemo ule wa kidiplomasia. Aidha, amesema muda wa kutoa sababu na visingizio umekwisha na kwamba sasa ni wakati wa kuwa imara, kwani mtu anayetaka amani lazima asimame imara wakati wote.

Wizara ya mambo ya nje ya China imesisitiza kwamba nchi hiyo imewahi kutekeleza kikamilifu maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Korea Kaskazini, lakini imesema itachunguza iwapo kuna shughuli ambazo zinakiuka maazimio hayo. Kwa mujibu wa wizara hiyo, China bado ina matumaini ya kuutatua mzozo uliopo kwa njia ya mazungumzo.

Kwa upande wa masuala ya kibiashara, Trump bado yuko katika shinikizo kubwa kutoka kwa mashirika ya biashara ya Marekani katika kutatua malalamiko ya kibiashara na China. Marekani imeishutumu China kwa kurudia ahadi yake ya kufungua masoko yake. Wiki iliyopita Trump alisema kulikuwa na hasara ya kibiashara ya Dola bilioni 347 kati ya nchi hiyo na China na kwamba hatua hiyo ni mbaya na inatia aibu.

China ni kituo cha tatu cha ziara ya siku 12 ya Trump barani Asia ambayo itamfikisha pia Vietnam na Ufilipino. Tayari kiongozi huyo wa Marekani ameizuru Japan na Korea Kusini.

Mwandishi: Grace Patricia Kabogo/DPA, AP, http://bit.ly/2iDsZsU
Mhariri: Josephat Charo

Mkurugenzi Mkuu Bodi ya Sukari kutolewa kazini

$
0
0

Na Mathias Canal, Dodoma
Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba amemuagiza Katibu mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe  kumsimamisha kazi mara moja Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania Ndg Henry J. Semwanza(Pichani juu) kuanzia leo Novemba 9, 2017.

Kwa agizo hilo lililotolewa na Waziri wa Kilimo Dkt Tizeba, Mkurugenzi huyo atatakiwa kurejea kwa mwajiri wake ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo kwa ajili ya kupangiwa kazi nyingine.

Simwanza anasimamishwa kazi kutokana na mwenendo wake wa utendaji akiwa Msimamizi Mkuu wa Bodi ya Sukari kutoridhisha.

Simwanza amehudumu katika nafasi hiyo akiwa Mkurugenzi wa Bodi ya Sukari tangu mwaka 2011.

MWISHO

PICHA TANO: Za Makamu wa Rais katika kilele cha Maadhimisho ya miaka kumi ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua gwaride maalum la polisi wanawake kwenye kilele cha Maadhimisho ya miaka kumi ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania yalioyofanyika kwenye Chuo Cha Taaluma ya Polisi, Kurasini
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo juu ya umuhimu wa alama za barabarani kutoka kwa Koplo Faustina Nduguru wa Kitengo cha Usalama Barabarani Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo juu kamera kugundua wanaoendesha kwa mwendo mkali kutoka kwa Konstabo Sharifa Ismail wa Kitengo cha Usalama Barabarani Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Kamishna wa Polisi Jamii Mussa Ali Mussa ambaye alimkaimu Mkuu wa Jeshi la Polisi 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aakihutubia wakati wa kilele cha Maadhimisho ya miaka kumi ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania yalioyofanyika kwenye Chuo Cha Taaluma ya Polisi, Kurasini, Dar es Salaam. 
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

MCHAKATO UNAENDELEA: Kufanikisha uwepo wa Mfumo wa soko la bidhaa

$
0
0

Na Mathias Canal, Dodoma
Serikali inaendelea na mchakato wa kufanikisha uwepo wa Mfumo wa soko la bidhaa (Commodity Exchange) ambapo miongoni mwa kazi za Mfumo huo utalenga kupunguza gharama za uendeshaji wa masoko ya mazao yote ya chakula na biashara ili kuwawezesha wakulima kupata bei nzuri na yenye tija.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Machuche Mwanjelwa Bungeni Mjini Dodoma Wakati akijibu swali la Mbunge wa Lulindi Mkoani Mtwara Mhe JEROME DISMAS BWANAUSI aliyetaka kufahamu ni lini Serikali itaanzisha mfumo wa “Commodity Exchange” ili kuwasaidia wananchi wanaolima Korosho kupata bei nzuri katika misimu husika.
Mhe Naibu Waziri alisema kuwa Maandalizi ya Soko la Bidhaa (Commodity Exchange) yalianza tangu mwaka 2011 kwa lengo la kufanya biashara ya mazao kuwa ya wazi na yenye ushindani kulingana na nguvu ya soko.
Mhe Mwanjelwa alizitaja hatua ambazo zimechukuliwa na serikali mpaka hivi sasa kuwa ni pamoja na kupitishwa kwa Waraka wa Soko hilo, Kuundwa kwa Bodi ya Soko, kutungwa kwa Sheria ya mwaka 2015 ya Soko la Bidhaa pamoja na kanuni zake, Kufanya uzinduzi wa kuanzisha Soko hilo, Kutoa mafunzo kwa Madalali watakaoendesha soko hilo na Kutoa mafunzo kwa baadhi ya viongozi wa Serikali na Sekta Binafsi ili kujenga uelewa wa pamoja.
Alisema, Ofisi na Jukwaa la soko hilo vimefunguliwa katika jengo la LAPF lililoko Kijitonyama jijini Dar es Salaam ambapo kazi za uwekaji wa vifaa katika Ofisi na Jukwaa hilo zinaendelea.
Mhe Mwanjelwa alisema, Elimu ya Soko la Bidhaa inaendelea kutolewa kwa baadhi ya viongozi wa ngazi za Mkoa na Wilaya na Maafisa Kilimo, Ushirika, Biashara na Maendeleo ya Jamii katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Morogoro, Dodoma na Singida.
Aidha, elimu hiyo imekwisha kutolewa kwa Viongozi wa Vyama Vikuu vya Ushirika na Viongozi wa Vyama vya Msingi na Vyama visivyokuwa vya Kiserikali ili kujenga uelewa wa soko hilo. Pia, elimu itaendelea kutolewa kwa wakulima na wananchi kwa ujumla ili wadau waufahamu mfumo huo wa soko.
Kuhusu suala la kodi kwa wakulima wa korosho Mhe Naibu Waziri alisema kuwa Katika mwaka wa fedha 2017/2018, Serikali imeondoa ushuru na tozo na kubakiza makato ya usafirishaji korosho kulingana na umbali halisi, mchango wa kuendeleza zao na ushirika na kuondoa shilingi 50 kwa kila kilo zilizokuwa zinatozwa kwa ajili ya kufungashia korosho. 

Aidha, Serikali imepunguza ushuru kwa Halmashauri za Wilaya kutoka asilimia 5 hadi 3.
Sambamba na hayo pia Naibu Waziri Mhe Mwanjelwa akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Busokelo Mhe Fredy Atupele Mwakibete Mkoani Mbeya kuhusu ujenzi wa chuo cha kilimo na mifugo Kata ya Lufilyo alisema kuwa Wizara ya Kilimo ina jukumu la kusimamia na kuviendeleza Vyuo vya Kilimo hapa nchini.

Alisema, Kwa mujibu wa maelezo ya Afisa Kilimo wa Wilaya ya Busokelo, Chuo kilichotajwa na Mhe. Mbunge sio Chuo cha Kilimo na Mifugo bali ni Kituo kidogo cha kutoa mafunzo ya kilimo kwenye Skimu za Umwagiliaji (Ward Agricultural Resource Centre). Kituo hicho kilijengwa kwa jitihada za aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Rungwe Mashariki Mheshimiwa Profesa Mark Mwandosya ambapo mwisho alikabidhi kituo hicho kwa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe ili wakamilishe sehemu iliyobaki.

Aliongeza kuwa Wizara inatambua uwepo wa kituo hicho na inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo ili kupata fedha za kukamilisha ujenzi wa majengo hayo kwa ajili ya kutumika kama ilivyokusudiwa.

Vyuo vya Kilimo vinavyosimamiwa na Wizara ya Kilimo viko 14. Vyote hivyo vimejengwa muda mrefu na hivi sasa vinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na uchakavu wa miundombinu ikiwemo Ofisi za Walimu, Madarasa, Mabweni, Maabara, Nyumba za walimu, Maktaba na Karakana. Changamoto zingine ni uhaba wa Wakufunzi na Watumishi wa kada zingine pamoja na vifaa vya kufundishia.

Aidha, Kutokana na changamoto hizo Wizara imeweka kipaumbele cha kuboresha Vyuo vilivyopo badala ya kufikiria kuongeza Vyuo vingine.

Mhe Mwanjelwa alisisitiza kuwa Vyuo hivyo vikiakarabatiwa vitaweza kuchukua wanafunzi wengi hivyo kuwezesha Serikali kufikia lengo la kuwa na mtaalamu mmoja wa kilimo katika kila kijiji na pia kuzalisha Maafisa Ugani wenye uwezo wa kutoa huduma bora kwa wakulima.

Aidha, katika mwaka huu wa fedha wa 2017/2018 Serikali imeshatenga shilingi 773,208,000/= kwa kuanzia kwa ajili ya kufanya ukarabati katika Vyuo vya MATI.

Moyes adhamiria kuonesha makubwa West Ham

$
0
0
Meneja mpya wa West Ham David Moyes amesema kwamba anataka kutuma ujumbe fulani na kwamba anataka pia kujenga upya sifa zake katika klabu hiyo.

Meneja huyo wa zamani wa Everton na Manchester United alichukua nafasi ya Slaven Bilic, aliyefutwa Jumatatu klabu hiyo ikiwa eneo la kushushwa daraja kwenye jedwali.

"Nina jambo nahitaji kuthibitisha. Wakati mwingine inabidi kujaribu kukarabati mambo na nina mambo mengi nafaa kukarabati," amesema Moyes.

"Ni fursa nzuri kwangu, nimerejea na ndilo jambo ninalopenda kulifanya. Ninataka kufanya vyema na ninataka timu ifanye vyema pia."

Moyes, 54, amekuwa hana kazi tangu Mei alipojiuzulu wadhifa wake kama meneja wa Sunderland baada ya klabu hiyo kushushwa daraja.

"Ni jambo zuri kwa West Ham, wanampata meneja mzuri," amesema.

Moyes, ambaye alianza kazi ya umeneja Preston North End, alishinda tuzo ya Meneja wa Mwaka wa LMA mara tatu akiwa Everton kati ya 2002 na 2013.
Katika miaka 11 aliyokuwa nao, walimaliza katika nane bora mara tisa.
Alitia saini mkataba wa miaka sita kumrithi Sir Alex Ferguson katika Manchester United mwaka 2013 lakini akafutwa miezi 10 baadaye.
Moyes kisha alienda Uhispania na kuwa meneja wa Real Sociedad lakini akafutwa Novemba 2015 mwaka mmoja baadaye.
Alichukua hatamu Sunderland Julai 2016 lakini akajiuzulu Mei 2017 baada ya klabu hiyo kumaliza ikiwa inashika mkia Ligi ya Premia.
'Kibarua changu cha kwanza ni kushinda mechi'
Mechi zijazo za West Ham
19 NovembaWatford (Ugenini); 24 NovembaLeicester City (Nyumbani); 29 Novemba: Everton (Ugenini)
3 DesembaManchester City (Ugenini); 9 Desemba: Chelsea (Nyumbani); 13 DesembaArsenal (Ugenini)
West Ham wamo nafasi ya 18, baada ya kushinda mechi mbili pekee Ligi ya Premia msimu huu.
Walitumia jumla ya £42m majira ya joto kuwanunua wachezaji wakiwemo mshambuliaji Marko Arnautovic kutoka Stoke City kwa rekodi ya klabu ya £20m na mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Javier Hernandez kutoka Bayer Leverkusen kwa £16m.
-BBC Swahili

PICHA ZA RAIS MAGUFULI: Katika shughuli ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Bomba la Mafuta ghafi litakalo toka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Tanga

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akishikana mkono na kupongezana na Mwenyeji wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Bomba la Mafuta ghafi litakalo toka Hoima nchini Uganda hadi eneo la Chongoleani mkoani Tanga. Sherehe za uwekaji wa jiwe hilo zimefanyika katika eneo la Mutukula Wilayani Kyotera nchini Uganda

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Mwenyeji wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakisikiliza maelezo ya namna ya bomba hilo la mafuta ghafi litakavyojengwa na kuanza kufanyakazi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Mwenyeji wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta wakijadiliana jambo mara baada ya kupewa maelezo ya mradi huo mkubwa wa bomba la mafuta ghafi.
 Jiwe hilo la Ufunguzi la Ujenzi wa Bomba hilo la Mafuta ghafi 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Mwenyeji wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakiondoka katika eneo la Mutukula mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi la bomba la mafuta.
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwasili pamoja na Mke wa Rais wa Uganda Mama Janeth Museveni katika eneo la mpaka wa Tanzania Mutukula kabla ya ufunguzi wa Kituo cha pamoja cha huduma za mpakani kwa upande wa Tanzania na Uganda.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kuwasili upande wa Tanzania kabla ya ufunguzi wa Kituo cha pamoja cha huduma za mpakani kwa upande wa Tanzania na Uganda.
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwasili pamoja na Mke wa Rais wa Uganda Mama Janeth Museveni wakiangalia ngoma katika eneo la Mutukula upande wa Uganda.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakati wa nyimbo za mataifa ya Tanzania na Uganda zikipigwa katika eneo la Uganda.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakifungua Ofisi za Kituo cha pamoja cha huduma za mpakani kwa upande wa Tanzania. Wanne kutoka kushoto ni Mke wa  wa Rais Mama Janeth Magufuli akishuhudia pamoja na Mke wa Rais Museveni Mama Janeth Museveni wa kwanza kushoto.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakizungumza na mamia ya wananchi hawaonekani pichani katika eneo la Kyatera nchini Uganda mara baada ya ufunguzi wa Bomba la Mafuta. PICHA NA IKULU

Viewing all 1295 articles
Browse latest View live