Quantcast
Channel: Mdimu's Blog
Viewing all 1295 articles
Browse latest View live

DC NZEGA AFUNGUKA: Bila Sayansi, kilimo si kitu

$
0
0
 Na Dotto Mwaibale, Nzega Tabora
MKUU wa Wilaya ya Nzega mkoani Tabora, Godfrey Ngapula amesema Sayansi na Teknolojia haiwezi kuepukika katika kilimo nchini.

Ngapula ameyasema hayo leo kwenye uzinduzi na kukabidhi mbegu bora za Mahindi ya Wema 2109, mihogo na Viazi lishe kwa ajili ya kuanzisha mashamba darasa katika vijiji vya Shila, Iyombo, Upungu, Lububu na Kapanga wilayani humo.

Mkuu huyo wa wilaya alisema ili kufanya kilimo chenye tija sayansi na teknolojia haiwezi kuepukika kutokana na changamoto mbalimbali zilizopo.

Alisema kilimo cha kisayansi kina tija kwani mkulima anaweza kulima eneo dogo na kupata mavuno mengi kuliko kilimo cha mazoea ambacho mkulima hulima shamba kubwa mazo kidogo.

Ngapula aliipongeza Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kuwapelekea mbegu hizo kwa kushirikiana na Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB) 

Akizungumzia matumizi ya mbegu zilizozalishwa kwa teknolojia  ya uhandisi jeni (GMO) alisema hayakwepeki kwa kuwa mbegu hizo zinasifa ya kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo ukame na wadudu waharibifu wa mazao.

Alisema wilaya hiyo kupelekewa mbegu hizo kwao ni fursa kubwa na kwa kushirikiana na wakulima na maofisa ugani atahakikisha mashamba darasa hayo yanatunzwa vizuri na kuwa ndio chanzo za kutoa mbegu nyingi na kuzisambaza katika maeneo mengine.

Mtafiti wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku mkoani Kagera, Jojianas Kibura aliwaambia wakulima hao kuwa hekta moja ya mihogo iwapo watalipa kwa kufuata ushauri wa wataalamu wataweza kupata tani 25 hadi 32 kwa zao la mihogo na viazi lishe watapata tani 7 hadi 9 kwa hekta moja.

Alisema matokeo hayo watayapata endapo watafuata kanuni bora za kilimo cha mazao hayo kwa kuzingatia nafasi kati ya mche na mche na mstari kwa mstari na matumizi ya mbolea hivyo wataweza kuongeza uzalishaji zaidi tofauti na sasa ambapo kwenye hekta moja ya mihogo wanapata tani nane hadi kumi wakati kwenye viazi lishe wanapata tani moja hadi 3.

Mtafiti huyo alisisitiza kuwa mbegu hiyo ya Mihogo ya Mkombozi imefanyiwa utafiti na kuonekana kustahimili magonjwa hatari ya mihogo ya batobato kali na michirizi ya kahawia ambayo imekuwa ikiwapatia hasara kubwa wakulima wengi na kupoteza hadi asilimia 90 za mazao.

Akizungumzia kuhusu mbegu Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH ambaye ni Ofisa Mwandamizi wa COSTECH, Audax Mutagwa, alisema mbegu hizo ya mihogo aina ya Mkombozi imefanyiwa utafiti na kuonekana ina uwezo mkubwa wa kustahimili magonjwa kama ya batobato kali na michirizi ya kahawia ambayo imekuwa ikiwapatia hasara kubwa wakulima na ya mahindi ikistahimili hali ya ukame na kutoa mazao mengi.

Mutagwa aliwaomba wakulima hao kuyatunza mashamba hayo ambayo yamegharimu fedha nyingi hadi kukamilika kwake hivyo wayaendeleze kwa ajili ya kuja kutoa matunda kwa wakulima wa wilaya hiyo na kupata chakula cha kutosha na ziada kuuza.

Aliongeza kuwa kazi kubwa ya COSTECH ni kuishauri serikali katika masuala mbalimbali ya sayansi na teknolojia na kuhakikisha matokeo ya tafiti zinazofanyika nchini yanawafikia walengwa ambao ni wakulima.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Shila ambayo ni shule pekee iliyopata baada ya kuwa na shamba darasa la mihogo katika wilaya hiyo,  Gunguti Awadh Mzee alisema shamba hilo litakuwa la mfano na kuwa mradi huo utasaidia kuwapatia wanafunzi wake chakula wakiwa shuleni hapo.

PICHANI JUU: Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Shila Wilayani Nzega mkoani Tabora wakiwa wamebeba mbegu ya Viazi lishe wakielekea kwenye shamba darasa wakati wa uzinduzi wa shamba hilo wilayani humo leo. Shule hiyo ni shule pekee wilayani humo kupata bahati ya kuanzisha shamba hilo.
 Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH ambaye ni Ofisa Mwandamizi wa COSTECH, Audax Mutagwa (kulia), akimkabidhi mbegu ya mihogo Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Godfrey Ngapula kwa ajili ya kupandwa katika mashamba darasa katika uzinduzi wa mashamba hayo ya mbegu wilayani humo leo. 
 Wanafunzi wa Shule ya Shila wakiwa shambani wakati wa uzinduzi wa shamaba darasa hilo.
 Ofisa Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Said Babu akizungumza kabla ya kuanza uzinduzi huo uliofanyika katika Wilaya hiyo Shule ya Msingi, Shila.
 Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH ambaye ni Ofisa Mwandamizi wa COSTECH, Audax Mutagwa, akizungumza katika uzinduzi huo.
 Mtafiti wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku mkoani Kagera, Jojianas Kibura, akielezea ubora wa mbegu ya mihogo iliyofanyiwa utafiti kabla ya uzinduzi wa shamba darasa katika Shule ya Msingi ya Shila.
 Kaimu Ofisa Ugani wa Halmshauri ya Wilaya ya Nzega, Hassan Mtomekela akizungumza katika uzinduzi huo.
 Mtafiti wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku mkoani Kagera, Jojianas Kibura, akielekeza jinsi ya kupanda mbegu ya mihogo hiyo kiutaalamu.
 Mtafiti wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku mkoani Kagera, Jojianas Kibura, akimuonesha mbegu hiyo mkuu wa wilaya hiyo.
 Mkuu wa Wilaya hiyo akizindua shamba darasa hilo kwa kupanda mbegu ya mihogo katika Shule ya Msingi ya Shila.
 Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Gunguti Awadh Mzee akipanda mbegu hiyo.
 Dada Mkuu wa Shule ya Shilwa, Maria Kulwa akipanda mbegu hiyo.
 Upandaji ukiendelea katika shamba hilo.
 Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Gunguti Awadh Mzee, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu bahati iliyopata shule yake kwa kupatiwa mradi huo wa shamba la mbegu.
 Mkulima wa Kijiji cha Shila, Zainabu Kanijo akizungumza na wanahabari.
 Wanawake wa Kikundi cha Wasafi Camp Imala Makoye kilichopo Kijiji cha Iyombo Kata ya Utwigu wakiwa wamebeba mbegu ya Viazi lishe wakielekea kupanda katika shamba darasa.
 Mtafiti wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku mkoani Kagera, Jojianas Kibura, akiwaelekeza wanakikundi hicho jinsi ya kupanda mbegu hiyo.
 Wanawake wa Kikundi cha Wasafi Camp Imala Makoye kilichopo Kijiji cha Iyombo Kata ya Utwigu wakipanda mbegu hiyokatika shamba lao.
 Wanawake wa Kikundi cha Wasafi Camp Imala Makoye kilichopo Kijiji cha Iyombo Kata ya Utwigu wakiimba nyimbo za kabila la kisukuma kufurahi mbegu hiyo.
Mtafiti wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku mkoani Kagera, Jojianas Kibura, akiwaelekeza wakulima wa Kijiji cha Upungu Kata ya Puge jinsi ya kupanda mbegu ya mihogo



SOMA: Yaliyosemwa katika semina ya kuwapiga msasa Jumuiya ya hifadhi ya wanyamapori

$
0
0

Na Fredy Mgunda,Mbalali
Shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na uhifandhi shirikishi wa wanayama pori (WCS) limeipiga msasa jumuiya ya hifadhi ya wanyamapori WAGA kwa lengo la kuhakikisha kuwa wanawalinda wanyama pori na kunufaika na uwepo wa wanyama pori hao.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri William aliwakata wanajumuiya ya hifadhi ya wanyamapori WAGA kuyatumia vizuri mafunzo waliyopata kulinda rasilimali za wanyama pori.

“Nawaombeni tumieni vizuri mafunzo haya kwa kuwa yatawasidia katika swala zima la uhifadhi ambalo ndio jukumu lenu la kwanza kabla hamjaangalia nini mnapata kama faida kwa kufanya hivyo WAGA itakuja kuwa jumuiya kubwa sana” alisema William

William aliwaomba jumuiya hiyo kutojihusisha na ujangili kwa kuwa wanaelimu ya uhifadhi na kuhakikisha wanyama pori wanalindwa kwa faida za taifa.

“Kuna jumuiya nyingi zimekuwa na migogoro kutokana na baadhi ya wajumbe kujihusisha na ujangili na kusababisha wanyamapori wengi kukimbia katika maeneneo ya hifadhi na kuwapunguzia kipato kwa wanajumiya hivyo nendeni mkatoe elimu kwa wananchi wengine kwa kuwa nyinyi mshapata elimu hiyo” alisema William

Aidha William alisema kuwa jumuiya ya WAGA bado ni changa hivyo wanatakiwa kuheshimu utawala bora ili kufikia malengo ambayo wamejiwekea kwa kunufaika na pori ambalo serikali imewapatia kwa ajili ya kufanya maendeleo ya vijiji.

“Najua kuwa mmeenda kujifunza kwenye jumuiya nyingine na mmeona kuna jumuiya zinamigogoro mingi hadi serikali huwa inaingilia kati na kuna jumuiya ambazo zinaendeshwa kwa kufuata utawala bora hivyo nawaomba mjifunze kufanya kazi kwa kufuata utawala bora” alisema William

William alilipongeza Shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na uhifandhi shirikishi wa wanayama pori (WCS) kwa mikakati wanayoifanya ya kuhaikisha jumiya ya WAGA inaendeshwa kisasa kwa manufaa ya taifa kwa kulinda wanyama pori ambao ndio hazina ya taifa katika kukuza pato la taifa.

Kwa upnde wake mratibu wa shughuli za uhifadhi kwa jamii katika shirika lisilo la kiserikali (WCS) Anna Kimambo alisema lengo la shirika hilo ni kuhakikisha jamii zinasimamia vilivyo rasilimali za wanyama pori,misiti na vyanzo vya maji ili baadae weweze kuona faida ya vitu wanavyo vitunza.

“Unajua kila siku nasema kuwa mtu akitunza rasilimali za wanyama pori nauhakika faida yake ni rahisi kuipata kutoka na kupata wawekezaji wengi ambao watakimbila eneo hilo kwa kuwa limehifadhiwa vizuri na litakuwa na wanyama pori wengi” Kimambo

Kimambo alisema kuwa WCS iliamua kuanza kuisaidia jumuiya hii ya WAGA kwa kutumia fedha za msaada kutoka USD ambazo zimetumika kutoka mwanzo mwa mchakato huu hadi hapa ulipofikia hivyo bila msaada wa USD wasingefika hapo walipofika.

“Kuunda jumuiya na kuisimamia hadi ilipofika hapa sio jambo dogo wangekuwa wananchi pekee yao wasingefanikiwa kutokana na mchakato huu kuhitaji fedha nyingi sana na kwa wananchi kingekuwa kitendawili” alisema Kimambo

Kimambo alisema kuwa WCS ilipita kijiji kimoja hadi kingine kutoa elimu ya uhifadhi wa wanyama pori ili wananchi wajue umuhimu wa uhifadhi wa wanyapori na ndio maana kukaundwa hii jumuiya ya WAGA inajumuisha vijiji vitano.

Lakini Kimambo alivitaja vijiji ambavyo vitanufaika na jumuiya ya hifadhi ya wanyamapori WAGA ni kijiji cha Nyakadete ambapo ndio makao makuu ya jumuiya hiyo,kijiji cha Nyamakuyu,kijiji cha Igomaa, Ihanzutwa na kijiji cha Mahoninga.

“Ukiangalia vijiji hivyo utagundua kuwa vimezunguka katika wilaya kuu tatu ambazo ni wilaya ya Mufindi, Iringa DC na wilaya ya Mbalali ambapo wilaya hizozipo katika mikoa miwili ya Iringa na Mbeya” alisema Kimambo

Naye afisa wanyamapori wilaya ya Mufindi Recho Nambo alisema kuwa katiba ya jumuiya ya WAGA imetengenezwa kwa mfumo ambao hautasababisha migogoro kama ilivyokuwa kwenye katiba za jumuiya nyingine.
“Kwa kweli katika jumuiya hii ya WAGA hatutegemei migogoro tena kwa kuwa tumetengeza katiba kwa ushirikiano wa wataalam wengi wenye weledi wa maswala ya katiba hivyo napenda kuwaambia kuwa jumuiya ya WAGA itakuwa ya mfano hapa nchini” Nambo

PICHANI JUU: Mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri William aliwakata wanajumuiya ya hifadhi ya wanyamapori WAGA kuzitunza rasilimali za wanyama pori kwa faida ya sasa na vizazi vijavyo kama wao walivyotunziwa na wananchi waliokuwepo miaka ya huko nyuma
Mratibu wa shughuli za uhifadhi kwa jamii katika shirika lisilo la kiserikali (WCS) Anna Kimambo alisema lengo la shirika hilo ni kuhakikisha jamii zinasimamia vilivyo rasilimali za wanyama pori,misiti na vyanzo vya maji ili baadae weweze kuona faida ya vitu wanavyo vitunza.



PICHA: Za hitimisho ya Promosheni ya Nunua Ushinde ya tiGO

$
0
0

Meneja Mauzo Mkoa wa Mtwara-Lilian Mwalongo akitoa maelezo kwa mteja wa Simu aina ya Tecno R6 kwa Faraji Said Lembe Mkazi wa Masasi katika Duka la Huduma kwa Wateja lililopo Masasi Mkoani Mtwara Simu ya Tecno R6 inauzwa shilingi laki moja na tisini na Tano kama Promotion.

Meneja Mauzo Mkoa wa Mtwara-Lilian Mwalongo akikabidhi simu aina ya Tecno S1 kwa mteja Faraji said Lembe mara baada ya kupata maelezo katika Duka la Huduma kwa wateja lililopo Masasi Mkoani Mtwara.

Meneja Mauzo Mkoa wa Mtwara-Lilian Mwalongo Akikabidhi Kofia Ngumu na Funguo ya pikipiki kwa mshindi wa shindano la Nunua Ushinde Saudi Chimatilo Mkazi wa Chiungutwa,Masasi Mkaoni Mtwara Shindano hilo ni kwa wanunuzi wa Sim aina ya Tecno R6 na Tecno S1 ambapo washindi walikabidhiwa Seti za Television pamja na Pikipiki.

Mshindi wa Shindano la Nunua USHINDE Saudi Chimatilo akiwa katika Pikipiki yake mara baada ya kushinda promosheni hiyo inayojumuisha Simu aina ya Tecno R6 na Tecno S1 8


PICHA ZA RAIS MAGUFULI: ..na ujumbe wake walipokutana na ujumbe wa Uganda Ikulu ya Masaka Uganda

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kuwasili katika Ikulu ndogo ya Masaka nchini Uganda.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu mara baada ya kuwasili katika Ikulu ndogo ya Masaka nchini Uganda.
 Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika eneo la mkutano baina ya wajumbe wa nchi mbili za Tanzania na Uganda katika Ikulu ya Masaka nchini Uganda.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja aliombatana nao katika Mazungumzo na ujumbe wa Uganda uliokuwa ukiongozwa na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni katika Ikulu ya Masaka nchini Uganda.
 ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo wa pamoja na ujumbe wa Uganda.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akicheza ngoma na kikundi cha Ngoma za Asili cha Cranes Performance mara baada ya dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa na mwenyeji wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni katika Ikulu ya Masaka nchini Uganda.
 Kikundi Cranes performance kikitumbuiza katika dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa kwa ajili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Ikulu ya Masaka Uganda. 
 PICHA NA IKULU


DK NDUMBARO: Upandishwaji vyeo serikalini uzingatie utendaji kazi

$
0
0
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro amehimiza suala la upandishwaji  vyeo kwa Watumishi wa Umma lizingatie utendaji kazi wa mtumishi husika na si suala la sifa ya kimuundo pekee kwa maana ya muda wa kutumikia miaka mitatu mitatu  kama wengi wanavyodhani.
Dkt. Ndumbaro  amesema hayo kwa nyakati tofauti katika Halmashauri za Wilaya ya Nyasa, Namtumbo na Manispaa ya Songea mjini katika ziara yake ya kikazi ya siku tano ya kuhimiza uwajibikaji mkoani Ruvuma, na kusisitiza kuwa mtumishi anayewajibika vizuri katika utendaji kazi wake  wa kila siku ndiye atakayepandishwa cheo na si vinginevyo.
Dkt. Ndumbaro amelazimika kutoka ufafanuzi huo, kufuatia baadhi ya watumishi katika Halmashauri hizo kulalamika kutopandishwa madaraja (vyeo) kwa wakati  kwa muda mrefu sasa wakati wenzao walioanza nao kazi wameshapandishwa vyeo, hivyo kupelekea  uwepo wa tofauti kubwa ya mishahara  baina yao .
“Haiwezekani Serikali ikapandisha mishahara kwa watumishi  wasiowajibika, walevi  na wasio na nidhamu na uadilifu  katika utendaji wao wa kazi, atakayewajibika katika utendaji wake ndiye atakayepandishwa ngazi ya mshahara”, Dkt. Ndumbaro amesisitiza.
Dkt. Ndumbaro ameainisha kuwa, malalamiko mengi ni ya Walimu ambao wamekuwa wakidhani kuwa kila baada ya miaka mitatu lazima wote wapandishwe vyeo (madaraja) hata kama hawajawajibika ipasavyo, suala ambalo si sahihi.
“Haiwezekani  Mwalimu anayefundisha vizuri darasani na  wanafunzi wake wanafaulu vizuri  masomo yake  akapandishwa daraja  sawasawa  na yule ambaye ufundishaji wake hauridhishi na ni mlevi wa kupindukia hali inayochangia wanafunzi wengi kutofaulu somo lake”, Dkt. Ndumbaro amefafanua.
Aidha, Dkt. Ndumbaro amesema, hivi karibuni, ofisi yake inatarajia kukutana na Tume ya Utumishi wa Walimu na kuzungumza na Walimu ili kutoa elimu na ufafanuzi yakinifu wa vigezo vya msingi vinavyozingatiwa katika   suala la upandishaji vyeo kwa watumishi wa umma  nchini  kwa lengo la kuepukana na malalamiko yasiyo ya lazima. 

Dkt. Ndumbaro anaendelea na ziara ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji mkoani Ruvuma katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru.

PICHANI JUU: Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa akiwa katika ziara yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji mkoani Ruvuma.
 Baadhi ya watumishi wa Hamashauri ya Wilaya ya Nyasa wakisikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) akiwa katika ziara yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji mkoani Ruvuma.
 Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akisalimiana na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo mara baada ya kuwasili katika Halmashauri hiyo katika ziara yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji mkoani Ruvuma.
 Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma, Bw. Hassan Bendeyeko akitoa taarifa ya utekelezaji wa masuala ya kiutumishi kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro aliyewasili mkoani humo kwa ziara yake ya  kikazi ya siku tano.
Baadhi ya watumishi wa Hamashauri ya Wilaya ya Songea wakisikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) wakati akifafanua masuala mbalimbali ya kiutumishi  katika ziara yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji mkoani Ruvuma.  
Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Bi. Luckness Adrian Amlima akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa masuala ya kiutumishi kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro aliyewasili katika wilaya hiyo kwa ajili ya ziara yake ya kikazi.

SHUHUDIA: We CARE na TPB walivyofanikisha kampeni za uchangiaji ya Niokoe Niishi

$
0
0

Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya TPB wakichangia damu katika viwanja vya CCM Ruanda Nzovwe jijini Mbeya Nov 11 mwaka huu

Zoezi la kuchangia damu likiendelea ..........

Afisa Oparesheni Benki ya TPB Nduguustafa Mmanga akichania Damu katika viwanja vya CCM Ruanda Nzovwe tamasha hilo la uchangiaji Damu limeandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la WE CARE TANZANIA lenye makao makuu yake jijini Mbeya na kudhaminiwa na Benki ya TPB Mkoa wa Mbeya Nov 11 mwaka huu ambapo kauli mbiu ya tamasha hilo ''NIOKOE NIISHI ''.

Meneja benki ya TPB Mkoa wa Mbeya Ndugu Humphrey Julius akipokea cheti shukrani kutoka kwa Mkurugenzi wa shirika la WE CARE Bi,Elizabeth Maginga kwa katambua mchango wa benki hiyo katika kufanikisha zoezi la uchangiaji Damu jijini Mbeya .

Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika tamasha hilo la uchangiaji damu katika viwanja vya CCM Ruanda Nzovwe jijini Mbeya Nov 11 ,2017.

Mkurugenzi shirika la WE CARE Bi, Elizaberth Maginga akizungumza katika Tamasha hilo la uchangiaji damu katika viwanja vya CCM Ruanda Nzovwe jijini Mbeya .

Zoezi la Uchangiaji likiendelea


TPB wakisakata rumba

Benki ya TPB katika picha ya pamoja na Meza kuu..

Vijana wa Boda boda katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa TPB .Picha Mr pengo na JMblog

Mhandisi Mtiguwe aipa changamoto Bodi ya Kahawa

$
0
0

Na Mathias Canal, Kilimanjaro
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe ameitaka Bodi ya Kahawa ambayo ni Taasisi ya serikali iliyopewa jukumu la kusimamia sekta ya Kahawa nchini kuongeza ufanisi katika uzalishaji wa Kahawa nchini kwani Kahawa ni miongoni mwa mazao ya kipaumbele.

Mhandisi Mtigumwe ametoa Rai hiyo wakati akizungumza na Wafanyakazi wa Bodi ya Kahawa Mara baada ya kutembelea Ofisi za Bodi hiyo zilizopo Mtaa wa Railway, Kata ya Mawenzi Katika Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Alisema kuwa Mwaka 2011 wadau waliandaa na kupitisha mkakati wa miaka 10 wa maendeleo ya Kahawa ambayo lengo kuu ilikuwa ni kuongeza uzalishaji hadi kufikia Tani 80,000 Mwaka 2017 na Tani 100,000 Mwaka 2021 lengo ambalo halijafikia na bado uzalishaji ni mdogo hivyo kuongeza uzalishaji linapaswa kuwa jambo la haraka iwezekanavyo.

Katibu Mkuu Alimuelekeza Kaimu Mkurugenzi Mkuu/Mkurugenzi wa Ubora wa Kahawa na uhamasishaji Masoko Kufanya Utafiti ili kubaini nini chanzo cha uzalishaji mdogo wa Kahawa iwapo wananchi kutotunza vizuri kahawa yao, Hali ya hewa na udongo au mbegu sio nzuri zinazotumika.

Aliongeza kwa kusema kuwa Serikali inajipanga kwa kampeni kubwa kutoa elimu kwa wananchi juu ya kufahamu umuhimu wa kulima kwa wingi mazao ya Chakula na Biashara ikiwemo zao la Kahawa.

Hata hivyo Katibu Mkuu huyo, Alisema miongoni mwa sababu ambazo huchangia uzalishaji mdogo katika mazao mbalimbali nchini huwa ni pamoja na Wananchi kuchanganya mazao wakati wa kupanda jambo ambalo sio rafiki sana katika Kilimo, sambamba na Kutoacha nafasi kati ya mche na mche.

Mhandisi Mtigumwe aliitaka Bodi ya Kahawa Kufanya Utafiti wa maeneo ambayo Kahawa inastawi kwa wingi ili kuongeza sehemu za kuzalisha Kahawa kufikia uzalishaji wa kiwango kikubwa tofauti na ilivyo hivi sasa.

Hata hivyo amesema kuwa atazishughulikia haraka iwezekanavyo Changamoto za Uzalishaji, Changamoto za Ubora, Changamoto za Masoko sambamba na Changamoto za Sekta.

Majukumu ya Bodi ya Kahawa ni pamoja na usimamizi wa sheria namba 23 ya marekebisho yake ya Mwaka 2009 na kanuni za Kahawa 2013 sambamba na kuratibu Majukumu shirikishi (Shared Functions) Baina ya serikali na wadau.

PICHANI JUU: Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akikagua kiwanda kidogo cha uzalishaji wa kahawa katika Bodi ya Kahawa mara baada ya kuwasili Ofisi hizo kwa ziara ya kikazi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akikagua namna Kahawa inavyohifadhiwa tayari kwa kuingia sokoni.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akisikiliza maelezo ya kitaalamu kuhusu mchakato mzima wa kupaki kahawa na soko lake kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu/Mkurugenzi wa Ubora wa kahawa na uhamasishaji masoko.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe alipotembelea chumba cha kuchotea Sampuli zinazopelekwa ambazo ni kilo 8 na kuchotea Gramu 300 kwa Loti.

Muonjaji katika Maabara ya Kahawa Bi Regina Mushi Daud akiendelea na majukumu yake katika maabara ya Kahawa.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu/Mkurugenzi wa Ubora wa kahawa na uhamasishaji masoko Kutoka Bodi ya Kahawa akielezea mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe namna wanunuzi wanavyokabiliana katika ununuzi wa Kahawa

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akizungumza na wafanyakazi wa Bodi ya Kahawa mara baada ya kuwasili kwa ziara ya kikazo

Baadhi ya wafanyakazi wa Bodi ya Kahawa wakifatilia kikao kilichoongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe katika Ukumbi wa Bodi hiyo.


Picha ya pamoja wafanyakazi wa Bodi ya Kahawa pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe.

TBL yapewa tunzo ya matumizi bora ya malori ya Mercedes Benz

$
0
0
 KAMPUNI ya bia nchini ya TBL imepewa tuzo ya kwanza ya matumizi bora ya magari makubwa ya mizigo ya Mercedes Benz Actros ambayo yametimiza zaidi ya kilomita milioni moja huku yakiwa bado katika hali bora. 

TBL ina magari kumi ya aina hiyo ambayo yamefanya kazi kwa miaka 17.Tuzo hiyo imetolewa na DAIMLER kwa kushirikiana na kampuni tanzu ya CFAO nchini Tanzania ambayo ndiyo mawakala pekee wa magari ya Mercedes Benz nchini Tanzania. 

Tuzo hiyo Mercedes-Benz Actros yenye kubeba jina la ‘Mileage Millionaire’ kutokana na kupita kilomita milioni moja, imetolewa kuonesha kuridhishwa kwa watengenezaji wa magari hayo juu ya uimara wake. TBL ina magari zaidi ya 80 ya Mercedes Benz. Magari yote hayo yamefikisha kilomita milioni 11 katika miaka 17 ya kuwa barabarani. 

Kilomita hizo ni sawa na kuzunguka dunia mara 275. Gari linaloongoza katika ‘Mileage Millionaire’ ni Actros modeli ya 3340, ambalo limefikisha kilomita 1,519,459 tangu lilipoingizwa TBL mwaka 2000. Magari mengine ni Actros za mwaka 2002,2003 na 2004 zikiwa na wastani wa kilomita kati ya kilomita milioni 1.02 na 1.5. 

Magari hayo yamekuwa yakitumika katika njia zote za Tanzania kupeleka vinywaji kutoka Dar es salaam, Arusha na Mwanza kwenda maeneo mbalimbali ya Tanzania.Kwa mujibu wa taarifa magari yote hayo yalinunuliwa moja kwa moja kutoka CFAO Motors Tanzania. 

  Bosi wa magari ya kibiashara ya Daimler upande wa Afrika, Naeem Hassim alisema katika kukabidhi tuzo hizo kwa TBL kwamba kuwa na magari ya aina hiyo katika kampuni yake kufikisha zaidi ya kilomita milioni 1 na bado yakiwa ‘vijana’ si jambo la kushtusha kwa Mercedes-Benz Actros

Alisema Actros yamejitanabaisha kwa ubora wake na kuaminika kwake:” ni dhahiri kuwa na magari kama haya ni uwekezaji wenye maana kubwa, ni vyema wateja wakayambua kwamba Actros ni gari la kuaminika.”  

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Tanzania, Marius Prinsloo alisema katika utoaji tuzo huo kwamba wanafurahi sana kusherehekea kilomita zaidi ya milioni moja ya magari ya ACTROS.Alisema ni mafanikio makubwa kuwa na magari hayo na hiyo inamaananisha kwamba ni imara na yanayoaminika yakiwa yametengenezwa kuhimili hali mbaya zaidi na kwamba wateja wanaweza wakawategemea kwa huduma bora za mauzo na pia uhudumiaji wa gari lenyewe ili liweze kudumu zaidi. 

Akipokea tuzo hiyo mwakilishi wa Tanzania Breweries Limited, ambaye ni meneja wa lojistiki wa Afrika Mashariki James Nyoike alisema kwamba amefurahi sana kuwa sehemu ya simulizi lenye mafanikio katika uendeshaji wa kampuni kwa kuwa na magari yenye sifa kubwa wa uimara. 

Alisema anafurahia huduma ya matengenezo inayopata magari yake kila yanapotakiwa kutengenezwa, pamoja na mafunzo kwa madereva hali iliyowezesha kuwapo kwa udumu zaidi kwa magari. 

“Tuna zaidi ya magari 80 ya Mercedes Benz kuanzia modeli za 2000 hadi 2016. Magari haya yamethibitisha ubora wake kazini na kuwa sehemu muhimu sana ya kazi zetu hasa za usambazaji wa bidhaa” alisema Nyoike.

Katika mahojiano alisema kwamba gari lililopitisha kilomita milioni 1.5 T 418 AAT limeendeshwa na dereva mmoja Moses Ulenga kwa miaka 10. “Nasikitika kwamba hakuhudhuria sherehe hizi, yuko safari” alisema Nyoike ambaye alisema pamoja na kufuata utaratibu wa service wa gari pia wamekuwa wakifanyia matengenezo ya kuzuia uharibifu na kwamba madereva wake wamefunzwa na zipo taratibu za kufuata zenye kuonesha nidhamu ya barabara. 

Naye Tharaia Ahmed Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko amesema kwamba wamemua kutoa tuzo hiyo kwa TBL kama sehemu ya kuonesha namna gani ushirikiano kuanzia mauzo hadi matunzo unavyoweza kumnufaisha mtu ambaye ananunua magari hayo kutoka CFAO. 

Alisema TBL imeonesha ubora wa magari hayo na kuaminika kwake katika safari ambazo wakati mwingine ni ngumu sana kwa kuzingatia mazingira vyetu. CFAO Motors Tanzania ambayo zamani ilijulikana kama DT Dobie ni kampuni tanzu ya kundi la makampuni ya CFAO ya Ufaransa. CFAO Motors iliundwa 1952na ni wakala wa magari mbalimbali Mercedes-Benz ya kibiashara, ya abiria na ya binafsi. 

PICHANI JUU: Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Tanzania, Marius Prinsloo akisalimiana na kuwakaribisha baadhi ya wageni waalikwa waliowasili kwenye hafla ya tuzo ya Mileage Millionaire kwa kampuni ya bia ya TBL. Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Regency-The Kilimanjaro.Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa CFAO Motors Tanzania Bi. Tharaia Ahmed (katikati) akifurahi jambo na mmoja wa wageni waalikwa kabla ya kuanza kwa hafla ya utoaji tuzo ya Mileage Millionaire. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Tanzania, Marius Prinsloo na kulia ni Mwakilishi wa CFAO, Simon Faraldo.Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Tanzania, Marius Prinsloo (kushoto) akifafanua jambo kwa mmoja wa wageni waalikwa kwenye hafla ya kuitunuku kampuni ya TBL tuzo ya Mileage Millionaires baada ya magari yake 10 aina ya Mercedes Benz Actros kupitisha kilometa zaidi ya milioni moja na yakiwa bado ni imara. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam katika Hotel ya Hyatt Regency - The Kilimanjaro. Mgeni rasmi katika hafla ya kuitunuku kampuni ya bia TBL tuzo ya Mileage Millionaires, Mkuu wa kampuni ya Daimler Commercial Vehicles Africa, Naeem Hassim (kulia) akibadilishana mawazo na baadhi ya wageni waalikwa kwenye hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Hyatt Regency-The Kilimanjaro.Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Tanzania, Marius Prinsloo akizungumza katika hafla ya kuitunuku kampuni ya TBL tuzo ya Mileage Millionaire baada ya magari yake 10 aina ya Mercedes Benz kupitisha kilometa zaidi ya milioni moja na yakiwa bado ni imara. Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam katika Hotel ya Hyatt Regency - The Kilimanjaro.Mgeni rasmi katika hafla ya kuitunuku kampuni ya bia TBL tuzo ya Mileage Millionaire, Mkuu wa kampuni ya Daimler Commercial Vehicles Africa, Naeem Hassim akizungumzia ubora wa magari ambayo yanauzwa na CFAO Motors na mipango ya kampuni hiyo kuendelea kuuza magari imara kwa mazingira ya Afrika.Picha ya pamoja kabla ya kukabidhi tuzo ya Mileage Millionaire.Mkuu wa kampuni ya Daimler Commercial Vehicles Africa, Naeem Hassim (wa pili kulia) akimkabidhi tuzo ya Mileage Millionaire mwakilishi wa kampuni ya bia TBL, Denis Dismas (katikati). Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Tanzania, Marius Prinsloo.Pichani juu na chini ni baadhi ya wageni waalikwa ambao ni wateja wa CFAO Motors Tanzania waliohudhuria hafla hiyo ya kuitunuku kampuni ya bia TBL tuzo ya Mileage Millionaire. [caption id="attachment_3153" align="aligncenter" width="1404"] Mgeni rasmi katika hafla ya kuitunuku kampuni ya bia TBL tuzo ya Mileage Millionaires, Mkuu wa kampuni ya Daimler Commercial Vehicles Africa, Naeem Hassim (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Tanzania, Marius Prinsloo (kushoto) katika picha ya pamoja na wawakilishi wa kampuni ya bia ya TBL mara baada ya kukabidhi tuzo hiyo.[/caption] [caption id="attachment_3144" align="aligncenter" width="1404"]Picha ya pamoja ya Uongozi wa CFAO Motors Tanzania na ugeni kutoka makao makuu ya kampuni hiyo.[/caption] [caption id="attachment_3145" align="aligncenter" width="1404"]Uongozi wa Kampuni ya CFAO Motors Tanzania na mgeni kutoka DAIMLER katika picha ya pamoja mbele ya gari moja kati ya 10 aina ya Mercedes Benz Actros ya kampuni ya bia ya TBL iliyopitisha kilometa 1,519,459 na kupelekea kukabidhiwa tuzo ya Mileage Millionaire. Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Regency-The Kilimanjaro.[/caption] [caption id="attachment_3138" align="aligncenter" width="1404"]Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa CFAO Motors Tanzania Bi. Tharaia Ahmed akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu tuzo ya Mileage Millionaire iliyotolewa na CFAO Motors Tanzania kwa kampuni ya bia TBL.[/caption] [caption id="attachment_3139" align="aligncenter" width="1404"]Mkuu wa (Logistics Services) wa kampuni ya bia TBL, James Nyoike akizungumza na waandishi wa habari namna TBL imefanikiwa kutunza magari yake aina Mercedes Benz Actros na kuweza kufikisha kilometa 1,519,459.[/caption] [caption id="attachment_3140" align="aligncenter" width="1404"]Wawakilishi wa kampuni ya bia TBL, James Nyoike (wa pili kushoto) na Denis Dismas (wa pili kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi katika hafla ya kuitunuku kampuni ya bia TBL tuzo ya Mileage Millionaire, Mkuu wa kampuni ya Daimler Commercial Vehicles Africa, Naeem Hassim (wa kwanza kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Tanzania, Marius Prinsloo (wa kwanza kulia).[/caption] KAWAIDA KAMPUNI ya bia nchini ya TBL imepewa tuzo ya kwanza ya matumizi bora ya magari makubwa ya mizigo ya Mercedes Benz Actros ambayo yametimiza zaidi ya kilomita milioni moja huku yakiwa bado katika hali bora. TBL ina magari kumi ya aina hiyo ambayo yamefanya kazi kwa miaka 17. Tuzo hiyo imetolewa na DAIMLER kwa kushirikiana na kampuni tanzu ya CFAO nchini Tanzania ambayo ndiyo mawakala pekee wa magari ya Mercedes Benz nchini Tanzania. Tuzo hiyo Mercedes-Benz Actros yenye kubeba jina la ‘Mileage Millionaire’ kutokana na kupita kilomita milioni moja, imetolewa kuonesha kuridhishwa kwa watengenezaji wa magari hayo juu ya uimara wake. TBL ina magari zaidi ya 80 ya Mercedes Benz. Magari yote hayo yamefikisha kilomita milioni 11 katika miaka 17 ya kuwa barabarani. Kilomita hizo ni sawa na kuzunguka dunia mara 275.

HIZI HAPA: Shamra shamra za tiGO Marathoni huko Dodoma

$
0
0

Wafanyakazi wa Tigo walioshiriki katika mbio ndefu za Tigo Dodoma Half Marathon wakiwa na bango linalosema 'Tumekusoma' kabla ya kuanza kwa mbio hizo ndefu jijini Dodoma leo. Tumekusoma ni kampeni mpya ya Tigo inayolenga kuwapa wateja wake urahisi wa kutumia huduma za simu pamoja na faida zaidi za bonasi kila watakapotumia namba mpya ya *147*00# kununua muda wa maongezi, bando, data na kufanya miamala ya fedha.
Mshindi wa mbio ndefu za Tigo Dodoma Half Marathon, Dickson Marwa akimaliza mbio hizo zilizofanyika mjini Dodoma hapo jana.

Baadhi ya waheshimiwa wabunge wa bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na medali na vyeti walivyotunukiwa kwa kushiriki mbio ndefu za Tigo Dodoma Half Marathon zilizofanyika katika jiji la Dodoma jana.

Naongoza kwa mfano na vitendo. Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dr Hamisi Kigwangala akimalizamio ndefu za Tigo Dodoma Half Marathon zilizofanyika katika jiji la Dodoma jana. Mhe Dr. Kigwangala alishiriki katika mbio za kilometa 21.

Mshindi wa mbio za Tigo Dodoma Half Marathon (wanaume), Dickson Allan wa Mara akipokea zawadi zake za ushindi kutoka kwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Juliana SHoza baada ya kumalizika kwa mbio hizo jijino Dodoma jana.

Mshindi wa mbio za Tigo Dodoma Half Marathon, Dickson Allan wa Mara akipngezwa na Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Aidan Komba baada ya kumalizika kwa mbio hizo jijini Dodoma jana.

Mshindi wa mbio za Tigo Dodoma Half Marathon kwa wanawake, Noela Remi Khaday akipokea medali kutoka kwa Mkurugenzi wa Tigo, Kanda ya Kaskazini, Henry Kinabo baada ya kumalizika kwa mbio hizo jijini Dodoma jana.

Mshindi wa mbio za Tigo Dodoma Half Marathon kwa wanawake, Noela Remi Khaday akipokea zawadi zake kutoka kwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Juliana Shoza baada ya kumalizika kwa mbio hizo jijini Dodoma jana.

Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Mhe Vumilia Nyamoga akimtunuku Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Juliana Shoza zawadi ya medali baada ya kushiriki mbio ndefu za Tigo Dodoma Half-Marathon zilizofanyika katika mji wa Dodoma jana.

HABARI: ...ya tiGofiesta Mtwara unayo?

$
0
0

Msanii Jux akitoa burudani kwenye tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara usiku wa kuamkia jumapili.

Janjaro akitumbuiza katika tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara usiku wa kuamkia jumapili.

Genevieve Mpangala akitumbuiza katika jukwaa la TIgo fiesta mapema usiku wa uamkia jumapili katika viwanja vya Nangwanda Sijaona

Aslay akiimba na mashabiki zake katika jukwaa la Tigo Fiesta mapema usiku wa kuamkia jumapili.

Chege akitumbuiza katika jukwaa la tigoFiesta mkoani Mtwara

Msanii Snura akitumbuiza katika jukwaa la Tigo Fiesta mapema usiku wa kuamkia jumapili.

Lulu diva akiwa katika jukwaa la Tigo fiesta amasha la Tigo Fiesta lililofanyika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara usiku wa kuamkia jumapili.

Madee akitumbuiza katika jukwaa la Tigo Fiesta tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara usiku wa kuamkia jumapili.

UNA HABARI?; Lulu amehukumiwa kwenda miaka miwili jela

$
0
0
Staa wa filamu nchini, Msanii Elizabeth Michael amehukumiwa kwenda jela miaka miwili baada ya kupatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba, katika hukumu iliyosomwa na Jaji wa Mahakama Kuu Mheshimiwa Sam Rumanyika.

Kwa muda wa miaka mitano mfululizo Lulu alikuwa akikabiliwa na kesi ya kumuua mpenzi wake Steven Kanumba bila kukusudia, kinyume cha kifungu cha 195 cha kanuni za adhabu (PC), Aprili 7, 2012, Sinza Vatican jijini Dar es Salaam kufuatia ugomvi wa kimapenzi ulioibuka baina yao.


UTAFITI KUHUSU NGONO: Ina uhusiano gani na mshtuko wa moyo?

$
0
0
Mshutuko wa ghafla wa moyo unaotokana na tendo la ngono unaweza kutokea zaidi miongoni mwa wanaume kuliko kwa wanawake, kwa mujibu wa utafiti.

Lakini hata hivyo pia kuna uwezekano mdogo kwa ngono kusababisha mshutuko wa moyo

Ni asilimia 34 ya visa 4,557 vya mshutuko wa moyo vilivytokea wakati wa tendo la au baada ya saa moja ya ngono na 32 kati ya wale walioathiriwa walikuwa ni wanaume.

Dr Sumeet Chugh, kutoka taasisi ya moyo ya Cedars-Sinai, anasema utafiti huo ndio wa kwanza kubaini ikiwa tendo la ngono linaweza kusababisha mshtuko wa moyo.Hali hiyo hutokea wakati moyo unakumbwa matatizo na kuacha kupiga.

Dr Chugh na wenzake huko California walikagua rekodi za hospitali kuhusu kesi za mshutuko wa moyo kwa watu wazima kati ya mwaka 2002 na 2015 huko Portland, Oregon.

Ngono ilichangia chini ya asilimia moja ya visa hivyo. Wengi walikuwa ni wanaume walio katika umri wa makamo.

- BBC Swahili

33 wafariki kwenye ajali ya treni DRC

$
0
0

Radio ya umoja wa mataifa nchini DRC imesema takriban watu 33 wamefariki katika ajali ya treni.

Ajali hiyo imetokea katika mji wa Buyofwe Kusini mwa jimbo la Lualaba.

Taarifa kutoka Radio Okapi zinasema treni hiyo ilianguka kisha kuwaka moto.

Gavana wa jimbo la Lualaba Richard Muyej ameiambia BBC kwamba kuna ajali iliyotokea lakini haifahamiki ni watu wangapi waliofariki.

- BBC Swahili

Emirates imenunua ndege 40 kutoka Boeng

$
0
0
Boeng imeanzisha maonyesho yake ya ndege huko Dubai kwa kutangaa mauzo makubwa mapya katika maonyesho hayo ya siku tano, ilitangaza kuwa Shirika la ndege la UAE la Emirates limeagiza ndege 40 za Boeng 787 Dreamliners, katika mkataba wa thamani ya dola bilioni 15.

Mwenyeki wa shirika hilo Sheikh Ahmed bin Saeed al-Maktoum, amesema kuwa Boeng imechaguliwa badala ya Airbus A350.

Sheikh Ahmed bin Saeed al-Maktoum alitarajiwa kutoa tangazo kubwa la kuagiza ndege za Airbus A380 superjumbo wakati wa mkutano wa waandishi wa habari.

Airbus inatarajia ndege zake za A380 kuagizwa zaidi zikiwa ndizo ndege kubwa zinazotumika kwa sasa.

Emirates ndilo shirika la ndege kubwa zaidi mashariki ya kati likiwa mnunuzi mkubwa zaid ya Boeng 777 na lina ndege 165 zinazohudumu likiwa tena limeagiza ndege 164.

- BBC Swahili

Trump atjitolea kupatanisha Bahari ya Kusini ya China

$
0
0

Rais Donald Trump wa Marekani (Pichani) amejitolea kuwa mpatanishi wa mzozo wa Bahari ya Kusini ya China inayowaniwa na mataifa sita ya kusini mwa Asia, huku China ikisema itashirikiana na wenziwe kuutatua mzozo huo.

Akizungumza katika mkutano wake na Rais Tran Dai Quang mjini Hanoi hivi leo (Novemba 12), Rais Trump alisema kama akiombwa, basi yuko tayari wakati wowote "kuwa mpatanishi" wa mzozo huo.

Vietnam imekuwa mkosoaji mkubwa dhidi ya madai ya China kwamba ndiyo pekee yenye umiliki wa Bahari ya Kusini ya China, na hasa hatua ya taifa hilo kubwa kwenye eneo hilo kujenga visiwa vya kubuni na kuweka vituo vya kijeshi kwenye bahari hiyo, ambayo hutumika kusafirisha bidhaa za dola trilioni 3 kwa mwaka.

Hata hivyo, Trump alikiri kwamba msimamo wa China kwenye mzozo huo umekuwa tatizo kubwa, lakini anaweza kutumia ushawishi wake na wa nchi yake kufikia suluhisho. "Mimi ni mpatanishi na msuluhishaji mzuri," alijisifia.

Vietnam pia imeshaichukuwa ardhi inayozunguka miamba na visiwa vya Bahari ya Kusini, ingawa si kwa kiwango ambacho China imefanya. Sambamba na Vietnam na China, mataifa ya Brunei, Malaysia, Ufilipino na Taiwan nayo pia yana madai kama hayo kwenye bahari hiyo.

China yasema itashughulika yenyewe
Rais Donald Trump wa Marekani akiwa na mwenyeji wake, Rais Xi Jinping, wakati wa siku za kwanza za ziara yake nchini China.

Kwa upande wake, Rais Xi Jinping wa China amesema nchi yake itashirikiana na mataifa ya kusini mwa Asia kulinda amani kwenye bahari hiyo. Akizungumza na mwenzake wa Ufilipino, Rodrigo Duterte, kandoni mwa mkutano wa kilele wa Ushirikiano wa Kiuchumi wa Asia na Pasifiki (APEC) nchini Vietnman, Rais Xi alisema China inahitaji kuona amani, utangamano na maendeleo kwenye eneo hilo la Bahari ya Kusini.

Rais Duterte, ambaye nchi yake iliwahi kupeleka kesi kwenye Mahakama ya Kimataifa dhidi ya China juu ya mzozo huo, amesema watalishughulikia suala hilo baina yao.

Bahari ya Kusini ya China ilijadiliwa mjini Beijing katika siku ya kwanza ya ziara ya Trump ya siku 12 barani Asia na waziri wake wa mambo ya nje, Rex Tillerson, alisema Marekani na China ziliambizana ukweli wa wazi.

Marekani imeikasirisha China kwa kuendeleza doria ya manuwari na ndege karibu na visiwa vinavyomilikiwa na China.

Mnamo mwezi Agosti, mawaziri wa mambo ya nje wa kusini mashariki mwa Asia na China walianzisha utaratibu wa mazungumzo juu ya Bahari ya Kusini ya China, hatua iliyopongezwa kama ya maendeleo, lakini inayoonekana na wengine kama mbinu ya China kuvuta muda wa kuimarisha nguvu zake baharini.

Mwandishi: Mohammed Khelef/Reuters
Mhariri: Yusra Buwayhid
- DW

ZEE LA NYETI: ...unakomaaje na Bata wakati laifu yenyewe utata?

$
0
0
Jana ilikuwa siku ya mfanano wa kuzaliwa ya mwanangu mwenyewe Mohamed Change, Dj Mzee aliyegoma kukua tauni, anakomaa tu na ishu za naniliu, humu humu tunapigana vkumbo lakini haniwezi, mwenyewe hajui haniwezi kwenye nini, ila anajitahidi kunipiga majungu lakini wapi, …napenya.

Eneweiz mchizi pati yake ilikuwa na mademu kibao mwanangu mwenyewe, kama we mtu wa kumaindi zile ishu ungeibuka, lazima ungeibuka na zigo, gambe zilikuwa za kutosha, watt walipiga kinywaji mpaka wakazima kudadadeki, mwanetu alijipanga.

Umri bwana ukiusherehekea, unapendeza, hata kama sio miaka mia tisa…

Sasa babaako si nikazamia ule mnuso, nikakutana na wazamiaji wenzangu kama nane vivi, walikuwa kwenye meza ya nyuma yangu, mademu flani hivi wenye uspuni tauni, watu wa kusukuma mandinga ya kukodi na pamba kaliiii, za bei ya laki kwenda mbele, ambao ukijimiksi ukakaa nao meza moja unalo. 

Uliza haukamz?

..lazima uachiwe bili hiyo mwanangu, na hawa mademu wanakuwaga fulltaimu wameinama kwenye simu wako bize balaa, na ni bora habari zao za Simu tupotezee maana ukitaka kujua huwa wanaandika nini unaweza ukawachapa vibao kudadadeki.

We si unajifanya jentromeni? Mwenzako anakuona bwege tu..
..ndio bwege, kwani mini babu, unaumia wakati ukweli?
..na kama umemaindi narudia tena unaonekanaga Bwege tu!

Ukiingia tu mezani kwake ukamuuliza kistaarabu kama naweza kukujoini anakukaribisha, halaf anazama wasapu, anawashtua washkaji zake, baada ya muda anaibuka moja moja na vigauni vaya vaya siku hizo kama blauzi.

Mchana wanavivaaga na skintaiti chini, usiku taiti inatupwa, Mzee unafaidi nyama, na mwanangu mwenyewe ninavyokujua lazima uoneshe ujentromeni hapo, watoto wakali tena? zitakuja bili mpaka upagawe, ..si bwege? 

Ujue washkaji tauni hapa wanadhani ujetromeni ni kuvaa fresh, kunukia na kuzama kiwanja, halaf ukiwakuta mademu uwe unapiga raundi. Kumbe mademu wenyewe wana picha tofauti na hão majentromeni, demu wa tauni hataki mambo za kistaarabu sijui Ouganda na mtu, Sao pela pela tu.

Na ndio maana leo ukimuibukia demu sijui umwambie mambo ya ficha yake, umfungulie biznes ya faida kilo kwa wiki anakuona mbwiga tu, kwa sababu mwenyewe akitega tu kiwanja hiyo kilo anaweza kuibabua kwa danga dakika tano tu.

Sasa haukamz umpe mpango wa kumuweka mahala kwa kilo?

Sista dua utamkuta homu ana pamba za Bei mbaya, kiatu kirefu mpaka kule, viwanja anavyopita babu yangu we mwenyewe unajifikiria mara mbili mbili kuibuka, ila sasa kamsachi, ana mkwanja mrefuuuu, sana sana unamkuta na fifte labda, tena wachaaaache.

Huyo sista sasa apate msala labda augue ghafla halaf labda mumrudishe homu, utakoma mwanangu mwenyewe na roho yako, chini utakuta godoro, ndio kitu utakachokielewa labda hivi vingine mpaka uambiwe hiki ni nini.

Haps ndio Zee linachukua apatyuniti na kuongea na masista zeta sasa kuhusu hizi Bata za tauni, mnafkiri zinaisha? Haziishi, miili yenu itazeeka, bata mtaziacha na sisi madanga pia mtatuacha tunadangwa na wanenu. Sasa fainali inafika wakati mnakuwa hamjaweka akiba hata buku, mnabaki kutuachia lawama.

Uso unakuwa ushaweka makunyazi, unafkiri Henry Kibodya atakupigia simu? Lazima akupotezee…
Anakuwa anawapigaia wajukuu zako, ndio anakula nao bata, kwa hiyo shtuka sistaangu, piga Bata huku unajiandalia maisha ya baadae.

Inaitwa laifu afta Bata!

Mama baada ya gambe uwe na pa kulala pasipokuwa na distabansi za Baba mwenye nyumba wala nini, halafu na Akiba uwe nano mwanangu, na Hawa wanaokufadhili kwee kinywaji wape maneno ya maana.

Mtu anakupiga gambe unamwita buzi?

Acha zako sistaangu, eneweiz, mtakuwa mmenielewa kama sio wengi baadhi au sio? Basi tutaonana Jumatatu ijayo, mstue na mshkaji kwamba Zee liso laivu kila Jumatatu lina mwezi sasa, changamkia topiki, na kisha ukishasoma acha komenti


Usisahau lakini ukijifanya jentromeni we bwege tu

MAKAMU WA RAIS: Katika mkutano wa pili wa Biashara, Ujasiriamali na Maonyesho wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo amefungua mkutano wa pili wa Biashara, Ujasiriamali na Maonyesho wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulioandaliwa na Baraza la Biashara la Afrika Mashariki.

Katika mkutano huo ambao unazikutanisha sekta Serikali na Sekta binafsi kutoka nchi wanachama, Makamu wa Rais alisisititiza kuwa pamoja na kuelekea kwenye kujenga Afrika Mashariki ya Viwanda ni muhimu viwanda hivi vitumie malighafi zinazozaliwa ndani ya Afrika Mashariki.

Makamu wa Rais alisema kujenga uchumi wa viwanda uendani na maboresho ya sera ya viwanda ili itoe uwanja mpana wa kuajiri vijana wengi zaidi.
Makamu wa Rais alihimiza kuwa Viwanda vitakavyojengwa viende sambamba na kilimo kwani kwa pamoja ndipo tunaweza ona mafanikio na ukuaji wa uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa Ujumla.

Makamu wa Rais alimalizia kwa kusema kuwa Serikali na Sekta binafsi zinawajibu kushirikiana katika kuandaa mazingira mazuri ya kuelekea kwenye uchumi wa viwanda.

PICHANI JUU: Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Biashara la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akijadiliana jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Biashara la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

MSAADA WA KIBAJETI: Sweden yaipatia Tanzania 435.79 Bilioni

$
0
0
Sweden imeipatia Tanzania Msaada wa jumla ya Fedha ya Sweden SEK. Bilioni 1.64 ambayo ni sawa na takribani Sh. bilioni 435.79 kwa ajili ya Msaada wa kibajeti na kusaidia mpango wa elimu. 

Makubaliano ya msaada huo yamesainiwa Jijini Dar es Salaam kati ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James na Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Maendeleo wa Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Ulf Kallsting.
Bw. James alisema kuwa imesainiwa Mikataba mitatu ya msaada huo ambayo ni; mkataba kwa ajili kusaidia Bajeti ya Serikali wa kiasi cha SEK milioni 600 ambazo ni sawa na Sh. bilioni 159.59 kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2017/18 hadi 2019/2020, ambapo kwa mwaka wa fedha 2017/2018 watatoa takribani Sh. bilioni 53.20.

Alisema fedha hizo zitaelekezwa katika kuboresha uhalisia wa Bajeti ili kuweza kutimiza majukumu ya kisera, kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani ya kikodi na yasiyo ya kodi na pia kusaidia Serikali kutoa huduma nzuri kwa wananchi kupitia taratibu za manunuzi.

Mkataba mwingine ni kwa ajili ya kusaidia Mpango wa Elimu kwa Matokeo (EPforR) wa kiasi cha Fedha ya Sweden SEK milioni 885 ambayo ni sawa na Sh. bilioni 235.40 kuanzia mwaka 2017/18 hadi 2020/2021.

“Lengo la msaada huu ni kusaidia Mpango wa Elimu kwa Matokeo ambapo tunapimwa namna ambavyo tumeweza kutimiza wajibu wetu tuliojiwekea katika bajeti. Baada ya ya Serikali kutimiza wajibu wake wa kupeleka fedha katika Sekta ya Elimu kwa wakati, wameamua kutupatia fedha hizo ambazo Serikali tunazipangia kazi kulingana na vipaumbele”, alieleza Bw. James.

Alieleza kuwa Mpango wa Elimu kwa Matokeo ulianza mwaka 2015/ 2016 na katika kipindi hicho yamepatikana maendeleo makubwa katika ujenzi wa miundombinu ya madarasa, vyoo, mabweni. Utekelezaji wake umefanywa katika shule 361 kwenye Halmashauri 129 nchini.

“Katika Mpango huo Vyuo 17 vya Walimu vimekarabatiwa ikiwa ni pamoja na kununua Kompyuta 260, Magodoro 6,730 na viti 1,976. Mpango huu unafanikiwa kutokana na dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuweka mkazo katika Sekta ya Elimu hivyo kupeleka fedha kwa wakati jambo linalosababisha washirika wa maendeleo wazidi kutuamini” alifafanua Bw. James.

Mkataba wa tatu ni Marekebisho ya Mkataba wa Mpango wa Kusoma, Kuhesabu na Kuandika ambao una kiasi cha Dola za Marekani 94.8 zilizotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Global Partnership for Education (GEP) na kukabidhiwa kwa nchi ya Sweden ili iweze kuusimamia.

Akifafanua kuhusu Mkataba huo Bw. Doto James alisema kuwa Serikali ili saini Mkataba huo na Sweden Mei, 2015 na muda wa utoaji wa fedha hizo ulikwisha Agosti, 2016 na kubakia kiasi cha Dola milioni 18.3 ambazo zitapatikana baada ya kusainiwa kwa mkataba huo.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Maendeleo katika Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Ulf Kallsting amesema kuwa nchi yake imedhamiria kuhakikisha inajenga uwezo na ujuzi kwa watanzania kuanzia elimu ya Awali kwa kuwa nchi yake inathamini sana elimu.

Bw. Kallsting alisema kuwa Tanzania imekuwa na uhusiano mzuri na Sweden na inatekeleza kwa ufanisi miradi mbalimbali hivyo nchi yake itaendelea kuisaidia Tanzania katika maeneo mbalimbali ya Maendeleo ili kufanikisha mipango yake.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James ameishukuru Sweden kwa niaba ya Serikali kwa kuendelea kuisaidia Tanzania katika kutekeleza bajeti yake.
 Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia)na Mkuu wa Kitengo cha  Ushirikiano na Maendeleo wa Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Ulf Kallsting (kushoto) wakisaini Makubaliano ya Msaada wa jumla ya Sh. bilioni 435.79 kwa ajili ya Msaada wa kibajeti na  kusaidia mpango wa elimu, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Maendeleo wa Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Ulf Kallsting (kushoto) wakiwa wameinua juu Mkataba wa Msaada wa wa jumla ya Sh. bilioni 435.79 kwa ajili ya Msaada wa kibajeti na kusaidia mpango wa elimu, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Maafisa waandamizi kutoka Ubalozi wa Sweden Nchini Tanzania wakishuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Msaada wa wa jumla ya Sh. bilioni 435.79 kwa ajili ya Msaada wa kibajeti na kusaidia mpango wa elimu, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi Amina Khamis Shaaban (Kushoto), Kamishna Msaidizi wa Fedha za Nje wa Wizara hiyo Bi. Mamelta Mutagwaba na wengine wakishuhudia utiaji saini wa Mkataba wa  Msaada wa wa jumla ya Sh. bilioni 435.79 kwa ajili ya Msaada wa kibajeti na  kusaidia mpango wa elimu, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James akizungumza na waandishi wa habari kuhusu msaada wa jumla ya Sh. bilioni 435.79 kutoka Sweden kwa ajili ya Msaada wa kibajeti na kusaidia mpango wa elimu, ambapo amesema msaada huo unatoa fursa kwa  Serikali kupeleka fedha zilizotakiwa kutekeleza majukumu hayo maeneo mengine ya Maendeleo ya Wananchi, hafla iliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Maendeleo wa Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Ulf Kallsting (kushoto) wakibadilishana Mkataba wa  Msaada wa wa jumla ya Sh. bilioni 435.79 kwa ajili ya Msaada wa kibajeti na  kusaidia mpango wa elimu, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa pili kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Maendeleo wa Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Ulf Kallsting (wapili kulia) pamoja na Maafisa waandamizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na Ubalozi wa Sweden wakiwa katika Picha ya pamoja baada ya kusainiwa  Mkataba wa  Msaada wa wa jumla ya Sh. bilioni 435.79 kwa ajili ya Msaada wa kibajeti na  kusaidia mpango wa elimu, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.

TRA imeongeza ufanisi Latina ufanisi wa kodi

$
0
0
Serikali imesema mapato yatokanayo na kodi ya majengo yanayokusanywa na Serikali yameongezeka baada ya jukumu hilo kukabidhiwa kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ikilinganishwa na ilivyokuwa chini ya Halmashauri.

Hayo yameelezwa Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb)(Pichani juu), alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Bukoba Mhe. Wilfred Lwakatare (CHADEMA), aliyetaka kujua Serikali inazipa Halmashauri ushauri gani wa kitaalam wa hatua za kuchukua ili kuziba pengo la kibajeti.

Katika swali hilo Mhe. Lwakatare aliuliza kuwa Serikali haioni kuwa uamuzi wa kuipa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kukusanya kodi hiyo ya majengo ni kuzidi kuipa mzigo mkubwa ambao hawatauweza.

Dkt. Kijaji alisema kuwa baada ya makusanyo yatokanayo na kodi za majengo kuanza kukusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA katika Halmashauri za Miji, Manispaa na Majiji 30, yalipanda hadi kufikia Sh. bilioni 34.09 mwaka wa fedha  2016/2017 ikilinganishwa na Sh. bilioni 28.28 zilizokuwa zimekusanywa na Serikali za Mitaa mwaka wa fedha 2015/2016.

“Makusanyo hayo ni sawa na ongezeko la asilimia 20.6 ya makusanyo halisi yaliyopatikana kutoka Halmashauri husika kabla ya kodi hiyo kuhamishiwa TRA hali inayodhihirisha kuwa, TRA imefanya kazi nzuri katika kukusanya mapato ikilinganishwa na kiasi kilichokusanywa na Halmashauri hizo 30 katika mwaka wa fedha 2015/16.”. alisema Dkt. Kijaji.

“Katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2017/18 Julai hadi Septemba, TRA, ilipangiwa kukusanya kodi ya majengo ya kiasi cha Sh. Bil 11.9 na kufanikiwa kukusanya kiasi cha Sh. Bil. 13.2 ikiwa ni ufanisi wa asilimia 111”.  Aliongeza Dkt. Kijaji.

 “Hatua ya Serikali ya kukasimu jukumu la ukusanyaji wa kodi za majengo kwa TRA, haikulenga kuzinyang’anya Halmashauri vyanzo vya mapato bali ni kuimarisha ukusanyaji wake”. alisema Dkt. Kijaji.

Aliongeza kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kunakuwepo ufanisi katika ukusanyaji na matumizi ya kodi zote zinazokusanywa ndani ya Serikali na kwamba Halmashauri zote zinapata mgao wa fedha kwa kuzingatia makisio ya bajeti zao na makusanyo ya mapato yote ya Serikali.

Aidha, Dkt. Kijaji alisema kuwa Serikali inatambua kuwa kodi ya majengo imekuwa ikichangia kwa sehemu kubwa mapato ya Halmashauri za Miji, Manispaa na Majiji katika kutekeleza mipango na utoaji wa huduma na maendeleo kwa wananchi.

Katika swali la nyongeza Mhe. Lwakatare alihoji kwa nini Serikali isichukue maoni yake ya baadhi ya majengo makubwa yatozwe kodi na TRA na yale madogo yatozwe kodi na Halmashauri kwa kuwa kumekuwa na changamoto kwa TRA katika ukusanyaji wa kodi hiyo na kuwatumia Maafisa Watendaji wa Kata katika kukusanya kodi hizo ambao wameajiriwa na Halmashauri.

Akijibu swali la nyongeza Dkt. Kijaji amesema kuwa Serikali na Bunge lilipitisha sheria ya fedha kwamba kodi ya majengo ikusanywe na TRA kwa lengo la kuimarisha ufanisi wake katika ukusanyaji na matumizi.

“Serikali itaendelea kusimamia sheria hiyo na kuhakikisha lengo la kuchukua kodi hiyo linafanikiwa na wananchi wanapata huduma stahiki”. aliongeza Dkt. Kijaji.

TANESCO imetoa Shilingi Milioni 10 kusaidia watoto wenye matatizo ya moyo

$
0
0



Na Khalfan Said
SHIRIKA la Umeme Tanzania, (TANESCO), limetoa msada wa Shilingi milioni 10 kusaidia matibabau ya watoto wanaougua maradhi ya moyo kwenye Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), jijini Dar es Salaam leo Novemba 14, 2017.

Akikabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Meneja Mwandamizi wa TANESCO Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Mhandisi Mahende Mgaya alisema, baada ya kusikia kupitia vyombo vya habari kuwa Taasisi hiyo inahitaji msaada ili iweze kuwafanyia upasuaji watoto ambao wazazi wao hawana uwezo wa kugharamia matibabu hayo, uongozi wa TANESCO ulisikia maombi hayo. Kwa kawaida upasuaji kwa motto hugharimu kiasi cha Shilingi Milioni 2.

“Tumekuwa na uhusiano mzuri na Taasisi yako, kwa hivyo japo hatuna uwezo mkubwa lakini Mkurugenzi Mtendaji aliona ni vema tutoe msaada wa kuwezesha upasuaji wa watoto watano, na leo tutakabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10.” Alisema

Mhandisi Mgaya katika hafla ya kukabidhi hundi hiuyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa JKCI, Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Aidha Mhandisi Mgaya alisema mbali na msada huo wa fedha, TANESCO pia imeondoa tatizo la upatikanaji wa umeme wa kutosha kwenye taasisi nhuyo kwa kuwawekea huduma maalum ili kuhakikisha umeme unapatikana bila ya shida yoyote.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakayab Kikwete, Profesa Mohammed Janabi, alisema ili kuenzi msada huo wa TANESCO, mmoja wa watoto watakaofaidika na msada huo atapewa jina la TANESCO.

“Tutawaalika katika hatua ya mwamzo kabla ya upasuaji ili muone hali halisi ya mgonjwa na baada ya upasuaji na tutamuita TANESCO motto huyo.” Alisema Profesa Janabi wakati akitoa shukrani zake.

Naye Daktari bingwa wa moyo kwa watoto, Dkt. Naiz Majani alisema kwa mwaka Taasisi hupokea wagojwa wanaohitaji upasuaji kiasi cha 200,000, kwa hivyo msada huo na minbgine kutoka kwa wasamaria husaidia pakubwa katika kuokoa maisha ya watoto wa Kitanzania.

“Tunawashukuru sana kwa msada wenu na tunaomba muendelee kusaidia jamii katika kuhakikisha watoto wa Kitanzania wanapatriwa matibabu ya moyo hata kama uwezo wao ni mdogo.” Alisema Dkt. Majani.

Katika hatua nyingine wafanyakazi wa TANESCO wametoa msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto waliolazwa kwenye taasisi hiyo wanaosubiri kufanyiowa upasuaji.

PICHANI JUU: Meneja Mwandamizi wa Shirika la umeme nchini, TANESCO, Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Mhandisi Mahende Mgaya, (wapili kushoto), na wafanyakazi wenzake, kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, akikabidhi hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 10, kwa Mkurugenzi Myendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, (JKCI), Profesa Muhammed Janabi, (mwenye miwani), katika hafla fupi iliyofanyika leo Novemba 14, 2017. Msaada huo w afedha utawezesha matibabu ya moyo kwa watoto watano waliolazwa kwenye taasisi hiyo.



Mhandisi Mgaya na Profesa Janabi, wakimsikilzia Mwenyekiti wa TUICO, Tanesco, Bw.Hassan J.M Athumani, wakati akitoa shukrani.

Profesa Janabi (kulia), akimkabidhi jarida la taasisi hiyo, Mhandisi Mgaya

Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, (kulia), akisalimiana na Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto, Dkt. Naiz Majani.

Bi. Muhaji akikabidhi msada wa maji, na mahitaji mengine, kwa muuguzi wa zamu wa wodi ya watoto wanaougua maradhi ya moyo, Bi.Joyce Mtanga

Mwenyekiti wa TUICO Tanesco, Bw. Hassan J.M Athjumani, (kulia), akikabidhi maji kwa mzazi wa mtoto aliyelazwa JKCI akisubiri kufanyiwa upasuaji wa moyo.


Mtoto MrishoHaidari(Miezi 7), ambaye anasumbuliwa na maradhi ya moyo akiwa wodini akisubiri kufanhyiwa upasuaji.
Viewing all 1295 articles
Browse latest View live