Mahakama ya rufaa nchini Sweden imeamua kuwafukuza wakimbizi vijana watano kutoka Afghanistan wanaotuhumiwa kuhusika na ubakaji wa makundi dhidi ya mvulana mmoja mwenye umri wa miaka 15 mwezi Oktoba mwaka jana.
Mahakama hiyo ilifuta hukumu ya mwanzo ya kifungo cha zaidi ya mwaka mmoja, na kuamua kuwafukuza kutoka nchini humo na kuwapigia marufuku kuingia Sweden kwa kipindi cha miaka 10 ijayo.