Madaktari wa Kenya wamelegeza msimamo wao baada ya mazungumzo ya miezi mitatu kuhusu nyongeza ya mshahara, baada ya serikali kuamua kujitoa kwenye mazungumzo hayo ya kuwaamuru magavana waandike barua za kuwatimua kazi madaktari watakaokataa kurudi kazini.
Mjumbe wa chama cha madaktari cha Kenya Bw Lukoye Atwili amesema makubaliano tayari yamefikiwa, kilichobaki ni kusainiwa, na kuchagua njia ya madaktari kurudi kazini kwa utaratibu mzuri.
Jumanne Rais Uhuru Kenyatta alilitaka baraza la magavana ambalo ni waajiri wa madaktari hao kuacha mazungumzo, na mazungumzo yaliendelea na viongozi wa dini ili kufikia makubaliano.
Serikali ya Kenya imewataka madaktari kurudi kazini, na kusema kila mmoja anatakiwa kujadili maswala yake na mwajiri wake.