Rais wa Marekani Donald Trump amesaini nyaraka mbili za urais za kulifanyia mabadiliko baraza la usalama wa taifa na lile la usalama wa ardhi na pia kuitaka wizara ya ulinzi ya Marekani kutoa mpango wa kupambana na kundi la IS nchini Syria na Iraq ndani ya siku 30.
Kwa mujibu wa nyaraka hizo, madhumuni ya mabadiliko hayo ni kuongeza uwezo wa serikali kukabiliana na vitishio vya kidijitali.
Pia zimesema Marekani haitavumilia kuwepo kwa kundi la IS na kwamba itaimarisha muungano wa kimataifa wa kupambana na kundi hilo na kudhoofisha uwezo wake wa kukusanya fedha.